Mfanyakazi CRDB afikishwa Mahakamani kwa kumuibia mteja zaidi ya Tsh milioni 100 na kuzitakatisha

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Messages
488
Points
1,000

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2018
488 1,000
WhatsApp-Image-2019-09-27-at-11.29.47.jpeg
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Ubungo, Andrew Babu (27) na wafanyabiashara watatu, wameshtakiwa kwa kula njama, kughushi Tembo kadi ya mteja, wizi wa zaidi ya Sh milioni 100 na kutakatisha fedha hizo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, William Sige (52), Justina Boniphace (49) na Alli Tutupa (35) wote wanaishi jijini Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mbando alidai kati ya Oktoba 2018 na Aprili 19, 2019 washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka jingine imedaiwa, Oktoba 29, mwaka jana katika benki ya CRDB tawi la Ubungo, ndani ya manispaa ya Ubungo, mshtakiwa Babu peke yake kwa nia ya kulaghai au kudanganya, alighushi sahihi ya Charles Kihamia katika fomu ya maombi ya Tembo card.

Pia mshtakiwa Babu anadaiwa, Novemba 6, 2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika kitabu cha usajili kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Babu anadaiwa Novemba 5, 2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika usajili wa kadi ya visa ya Tembo, kwa madhumuni ya kuonesha kuwa sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Inadaiwa Novemba 6,2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika kitabu cha usajili wa uelekezaji kwenye fomu ya maombi kwa madhumuni ya kuonesha kuwa, sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Babu pia anadaiwa, Oktoba 29, 2018 huko katika benki ya CRDB, alitoa fomu ya kughushi ya maombi ya Tembo kadi kwa ofisa wa banki hiyo aitwaye Omary Mduyah kwa dhumuni la kuonesha kuwa fomu hiyo imetolewa na kusainiwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la mwisho, imedaiwa kati ya Novemba 7,2018 na Aprili 29,2019 washtakiwa hao kupitia kadi ya gold ya Visa, walijipatia sh. 106,267,907/- kutoka kwa Charles Kihamia kupitia Visa gold card huku wakijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kughushi na wizi.

Hata hivyo wa washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 10, mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi
 

Oii

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2017
Messages
2,918
Points
2,000

Oii

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2017
2,918 2,000
Milioni 100 kwa watu watatu ni hela ndogo mno,kushiriki wizi wa hivyo ni kujitumbukiza shimoni. Tena hela yenyewe hawajaipiga kwa pamoja,wameipiga kidogo kidogo,kuna uwezekano mkubwa mpaka wanakamatwa hawana kitu. Hiyo hela inatakiwa unaipiga mtu mmoja tu,tena kwa pamoja. Ktk maisha yangu nimejifunza sana hii kitu. UKITAKA KUFANIKIWA KATIKA JAMBO LAKO LOLOTE LIFANYE PEKE YAKO.
Sio SI unit kwamba ukilifanya peke yako utafanikiwa. Kuna vitu huwezi tusua kivyako vyako
 

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Messages
335
Points
500

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2019
335 500
Field ya Bank ni ngumu sana kufanya kazi ukiwa si mtu mwenye mikakati binafsi na uadilifu wa hali ya juu.
Nafanya kazi kati Bank nina mwaka wa tatu sasa kwenye International Bank na uzuri zaidi nilianza kazi kama Cashier nilihudumu kwa muda wa mwaka mmoja tu.Kabla ya yote naomba hili litukae akilini kuna tofauti kubwa sana ya controls/procedures kati ya hizi bank za kimataifa na hizi za nyumbani,international bank wamekeza sana kwenye controls na system ambazo zinammbana mfanyakazi asiweze kuathiri pesa za wateja wenzetu wanajali sana reputation yani hata kama ulikuwa una attempt kufanya tukio ambalo lingeigharimu bank hakuna excuse ni mwendo wa TM tu ukasalimie Mwakaleli.
CASHIERS
Hawa ni wafanyakazi muhimu sana kwenye taasisi za kifedha lakini ni watu wanaoongozwa kulipwa mishahara duni na ni wafanyakazi wa daraja la chini hivyo huwafanya wawe na ugonjwa uitwao inferiority complex na wanapojaribu kuprove wrong ndipo hujikuta wamejiingiza kwenye hekaheka kama walizoziainisha wadau hapo juu (wizi,kushirikiana na majambazi n.k).
Nakumbuka nikiwa cashier niliipenda sana hii kazi japo nilijiwekea malengo kwamba sitafanya kwa zaidi ya mwaka natakiwa niwe nime grow sikuwahi kuwa na ndoto ya kuwa na mpira mkali ama mjengo kwani nilijua kwa ule mshahara wangu ungekuwa uongo so nilifanya kazi kwa bidii na uadilifu wa hali ya juu na kuwaheshimu wateja hiyo ilinipa credit na vilevile ukiwa cashier mwaminifu hukosi tip za 10k up to 50k jitahidi sana kuwa mwaminifu sometimes mteja anakuja amezidisha pesa maksudi anaona je utamrudishia?? nilikuwa muoga sana yani bora nihesabu mara kumi kumi lakini niwe na uhakika kuliko kumpunja mteja ama kujipunja mm mwenyewe, vyuma vinakaza kuna muda nilikua nabeba msosi kutoka home though nilichekwa ila nilijali zaidi mipango yangu na sikumaliza mwaka nilipata kazi nyingine.
●SYSTEM AND CONTROLS( Mifumo na taratibu)
International Banks wana mifumo mizuri iko very secured ni ngumu mtu ku access kirahisi, nilishangaa siku moja nimeenda kufungua account kwenye Bank ya bwana BABU nikaona ATM card inatengenezwa na kuwa authrorized na mtu mmoja yani yy mwenyewe ni Maker,checker and authrorizer niliona hili shipa sijawahi kuitumia hyo account hadi leo. Kwenye controls wajaribu kuiga international bank wana kitu inaitwa Duo control hapa inamaana kila kinachofanyika lazima kipitie kwenye mikono ya watu wawili hadi watatu kidogo inaondoa risk ya mtu mmoja mwenye tamaa kufanya yake.Kwa mfano nimesoma gapo juu kuwa mastermind aliprint ATM card, alighushi saini ya mteja hii kitu kwa baadhi ya bank hakiwezekani kabisa kwanza anaetunza card(custodian) ni mtu mwingine,ana initiate process ya kupewa card(maker) mwingine,anaechek kama kweli huyu mteja ni mwenyewe na kila kitu kipo sawa (cheker) ni mtu mwingine na kuna Authrorizer baada ya hawa watatu kufanya yote hayo then mtu wa mwisho ana authrorize mteja kupewa card jamani mchakato wote huo unafanywa within 5mins hii inasaidia zaidi local bank igeni hili muepukane na kadhia mnazowapa wateja wenu.

KIPI KIFANYIKE
Tunafahamu hakuna mshahara unaotosha lakini sector ya mabenk Tanzania local pamoja na international jaribuni kureview salary scale ya wafanyakazi wenu atleast mtu amudu kulipa kodi hata laki mbili kwa mwezi, wapewe trans allowance ili hata kama atajibana in 3yrs amudu hata kununua passo, meal allowance ikiwezekana hata communication allowance jamani wafanyakazi vipato vyetu ni tofauti na mfikiriavyo ninyi ni utanashati tu unatufanya tuonekane tunazo ila mambo sio kivile.
BANKERS acheni tamaa na kutaka kuishi maisha ambayo sio class yako hayo masubaru,crown, mark x bata za kila week end zitatuponza bankers hatuwezi kumudu tusiongopeane tukiforce ndo hayo ya bwana BABU. MUNGU saidia siku nitoke huku.
kwenye international banks mtu wa bank anaweza kujua salio la mteja??
 

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Messages
335
Points
500

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2019
335 500
Ndio tatizo letu waafrika, utajiri tunautafuta kwa haraka/kuiba bila kuwa na uvumilivu... Siku zote mali ya wizi haikufikishi popote, mali ya wizi haina baraka na pia inakupa sifa mbaya kwa jamii inayokuzunguka n.k.

Raha ya mali ni ile uloipata kwa njia ya halali, kwanza unakuwa na amani na furaha all the time coz umeipata kwa jasho lako.

MAJAMBAZI...MAFISADI...WIZI...hawana amani wala furaha katika maisha yao mpaka kufa kwao.

Mungu atuepushe kwakweli!
kumbe wezi ni waafrika tu
 

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Messages
335
Points
500

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2019
335 500
Ktk hali ya kawaida, hivi unafikiri ni rahisi sana kuhesabu noti zenye thamani ya Shilingi Milioni Tisa ukiwa KWA cashier's counter? Sema Watz wengi sana ni wazembe sana ktk kuwaeleza bank tellers wahesabu pesa kwenye mashine wanapokwenda kuchukua pesa taslimu banki.

MUHIMU KUZINGATIA:-

Unapokwenda kuchukua pesa taslimu bank, hakikisha cashier WA benki anazihesabu pesa zote/noti KWA kutumia mashine maalumu ya kuhesabia pesa, hii itakusaidia kuepuka kuibiwa pesa zako, pia kuepuka kupewa noti bandia NA cashiers wasio waadilifu
ahaaa!! noted,unaangalia mashine imepiga kelele mara ngapi sio
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2013
Messages
5,472
Points
2,000

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2013
5,472 2,000
Jamaa aliweka fedha kwenye bag akaweka mgongoni huku akitembea hana wasi wakati ameicha Lumumba anashuka na Mafia Str mahanidhi wakaja na pikipiki mmoja akashuka na kisu kikali akalikata mikanda begi akapanda boda wakatembea.

Ilikuwa ni chap kwa haraka ule mtaa una pilika pilika za watu ila walibaki wameduwaa hata aliyeibiwa ali-panic akabaki naye ameduwaa,stuff wa mabank mengi town hapa siyo waaminifu wengi wanashiriki vitendo viovu.
 

Forum statistics

Threads 1,343,415
Members 515,055
Posts 32,784,013
Top