Mfanyakazi CRDB afikishwa Mahakamani kwa kumuibia mteja zaidi ya Tsh milioni 100 na kuzitakatisha

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Messages
488
Points
1,000

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2018
488 1,000
WhatsApp-Image-2019-09-27-at-11.29.47.jpeg
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Ubungo, Andrew Babu (27) na wafanyabiashara watatu, wameshtakiwa kwa kula njama, kughushi Tembo kadi ya mteja, wizi wa zaidi ya Sh milioni 100 na kutakatisha fedha hizo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, William Sige (52), Justina Boniphace (49) na Alli Tutupa (35) wote wanaishi jijini Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mbando alidai kati ya Oktoba 2018 na Aprili 19, 2019 washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka jingine imedaiwa, Oktoba 29, mwaka jana katika benki ya CRDB tawi la Ubungo, ndani ya manispaa ya Ubungo, mshtakiwa Babu peke yake kwa nia ya kulaghai au kudanganya, alighushi sahihi ya Charles Kihamia katika fomu ya maombi ya Tembo card.

Pia mshtakiwa Babu anadaiwa, Novemba 6, 2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika kitabu cha usajili kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Babu anadaiwa Novemba 5, 2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika usajili wa kadi ya visa ya Tembo, kwa madhumuni ya kuonesha kuwa sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Inadaiwa Novemba 6,2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika kitabu cha usajili wa uelekezaji kwenye fomu ya maombi kwa madhumuni ya kuonesha kuwa, sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Babu pia anadaiwa, Oktoba 29, 2018 huko katika benki ya CRDB, alitoa fomu ya kughushi ya maombi ya Tembo kadi kwa ofisa wa banki hiyo aitwaye Omary Mduyah kwa dhumuni la kuonesha kuwa fomu hiyo imetolewa na kusainiwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la mwisho, imedaiwa kati ya Novemba 7,2018 na Aprili 29,2019 washtakiwa hao kupitia kadi ya gold ya Visa, walijipatia sh. 106,267,907/- kutoka kwa Charles Kihamia kupitia Visa gold card huku wakijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kughushi na wizi.

Hata hivyo wa washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 10, mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi
 

Heijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,252
Points
2,000

Heijah

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,252 2,000
Mwizi na mghushi sahihi ni mtu wa bank, kwani unadhani ye ni fala hata asijue SMS alert? Si una disable tu sms alert the deal done
[/QU
Kama unavyosema ni rahisi kihivyo kuwa mtu ana disable tu rahisi basi tatizo la kiusalama ni kubwa sana, ndio maana nimesema Bank lazima zieleze security control ikoje ile tujuwe pesa zetu ziko salama. Katika shirika lolote security ni top kunanakuwa inazibwa mianya. kwa unayosema ni rahisi hivyo basi hakuna alie salama.
 

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Messages
335
Points
500

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2019
335 500
Halafu kwanza kwanini haya matukio ya wateja kuibiwa na wanafanya kazi mara nyingi huwa nayaskia tu kwenye hizi Benjamin za kibongo!!? sijui CRDB sijui NBC, sijui NMB etc! Kwanini ni kwenye banks za kibongo tu!? Ni kwamba hizo ndio zina security system mbovu? Au ndio zina wafanya kazi wengi wasiokuwa waadilifu na wenye njaa?

Kwanini matukio kama haya ni nadra sana kuyaskia kwenye hizi international banks kama Barclay's, FNB, Standard chartered, Equity?
hivi kuna taratibu gani kufungua account kwenye hizi international banks?? inabidi tuhame tu
 

Swet-R

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Messages
1,674
Points
2,000

Swet-R

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2018
1,674 2,000
Milioni 100 kwa watu watatu ni hela ndogo mno,kushiriki wizi wa hivyo ni kujitumbukiza shimoni. Tena hela yenyewe hawajaipiga kwa pamoja,wameipiga kidogo kidogo,kuna uwezekano mkubwa mpaka wanakamatwa hawana kitu. Hiyo hela inatakiwa unaipiga mtu mmoja tu,tena kwa pamoja. Ktk maisha yangu nimejifunza sana hii kitu. UKITAKA KUFANIKIWA KATIKA JAMBO LAKO LOLOTE LIFANYE PEKE YAKO.
 

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Messages
335
Points
500

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2019
335 500
Duuhhh!! Bata lote hili Halafu mshaara probably haufiki hata milioni kwa mwezi. Mastermind indeed.

Hapo unakuta kuna vijana wa chuo wakiona maisha yake wanakuwa inspired wanapiga msuli wa kufa mtu hili wapate maGPA makubwa hili waje waajiriwe na wao CRDB.

Naamini hili sio tukio lake kwanza huyu mchizi kupiga hela za wateja.

Hii CRDB na bank zingine za kibongo sio za kuifadhi pesa ndefu kabisa. Ni banks za ovyo sana zenye wafanya kazi wa ovyo.

Binafsi mimi kama nna hela nyingi ni heri nizihifadhi kwenye Netteller au Skiril na sio kuzikabidhi midomoni mwa hawa akina Babu.
netteller ndo nini mkuu, naomba elimu hapo
 

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Messages
335
Points
500

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2019
335 500
Ndio maana mimi hizi banks zenu za kiswahili nilishazikimbia siku nyingi sana ni heri tu niendelee kuifadhi visenti vyangu kwenye Tigo pesa au Aitel money maana ndio naona kuna uafadhari mwingi kulinganisha na huko NMB.

Mimi kama nitahiji huduma za kibank basi ni Satanbic,FNB na Barclay's basi. Haijalishi hata kama wana tawi moja tu mkoa mzima.

My banking services orientation has been internationally upgraded. Bleep all local banks!
kweli aisee,wana taratibu gani kufungua account??
 

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Messages
335
Points
500

Tajiri wa Magomeni

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2019
335 500
Milioni 100 kwa watu watatu ni hela ndogo mno,kushiriki wizi wa hivyo ni kujitumbukiza shimoni. Tena hela yenyewe hawajaipiga kwa pamoja,wameipiga kidogo kidogo,kuna uwezekano mkubwa mpaka wanakamatwa hawana kitu. Hiyo hela inatakiwa unaipiga mtu mmoja tu,tena kwa pamoja. Ktk maisha yangu nimejifunza sana hii kitu. UKITAKA KUFANIKIWA KATIKA JAMBO LAKO LOLOTE LIFANYE PEKE YAKO.
hata mia yenyewe kwa mtu mmoja ndogo hata nyumba ya maana hujengi
 

Forum statistics

Threads 1,343,339
Members 515,022
Posts 32,781,310
Top