1kush africa
JF-Expert Member
- Dec 13, 2016
- 9,326
- 12,691
Mkuu umenena vizuri,,Field ya Bank ni ngumu sana kufanya kazi ukiwa si mtu mwenye mikakati binafsi na uadilifu wa hali ya juu.
Nafanya kazi kati Bank nina mwaka wa tatu sasa kwenye International Bank na uzuri zaidi nilianza kazi kama Cashier nilihudumu kwa muda wa mwaka mmoja tu.Kabla ya yote naomba hili litukae akilini kuna tofauti kubwa sana ya controls/procedures kati ya hizi bank za kimataifa na hizi za nyumbani,international bank wamekeza sana kwenye controls na system ambazo zinammbana mfanyakazi asiweze kuathiri pesa za wateja wenzetu wanajali sana reputation yani hata kama ulikuwa una attempt kufanya tukio ambalo lingeigharimu bank hakuna excuse ni mwendo wa TM tu ukasalimie Mwakaleli.
CASHIERS
Hawa ni wafanyakazi muhimu sana kwenye taasisi za kifedha lakini ni watu wanaoongozwa kulipwa mishahara duni na ni wafanyakazi wa daraja la chini hivyo huwafanya wawe na ugonjwa uitwao inferiority complex na wanapojaribu kuprove wrong ndipo hujikuta wamejiingiza kwenye hekaheka kama walizoziainisha wadau hapo juu (wizi,kushirikiana na majambazi n.k).
Nakumbuka nikiwa cashier niliipenda sana hii kazi japo nilijiwekea malengo kwamba sitafanya kwa zaidi ya mwaka natakiwa niwe nime grow sikuwahi kuwa na ndoto ya kuwa na mpira mkali ama mjengo kwani nilijua kwa ule mshahara wangu ungekuwa uongo so nilifanya kazi kwa bidii na uadilifu wa hali ya juu na kuwaheshimu wateja hiyo ilinipa credit na vilevile ukiwa cashier mwaminifu hukosi tip za 10k up to 50k jitahidi sana kuwa mwaminifu sometimes mteja anakuja amezidisha pesa maksudi anaona je utamrudishia?? nilikuwa muoga sana yani bora nihesabu mara kumi kumi lakini niwe na uhakika kuliko kumpunja mteja ama kujipunja mm mwenyewe, vyuma vinakaza kuna muda nilikua nabeba msosi kutoka home though nilichekwa ila nilijali zaidi mipango yangu na sikumaliza mwaka nilipata kazi nyingine.
●SYSTEM AND CONTROLS( Mifumo na taratibu)
International Banks wana mifumo mizuri iko very secured ni ngumu mtu ku access kirahisi, nilishangaa siku moja nimeenda kufungua account kwenye Bank ya bwana BABU nikaona ATM card inatengenezwa na kuwa authrorized na mtu mmoja yani yy mwenyewe ni Maker,checker and authrorizer niliona hili shipa sijawahi kuitumia hyo account hadi leo. Kwenye controls wajaribu kuiga international bank wana kitu inaitwa Duo control hapa inamaana kila kinachofanyika lazima kipitie kwenye mikono ya watu wawili hadi watatu kidogo inaondoa risk ya mtu mmoja mwenye tamaa kufanya yake.Kwa mfano nimesoma gapo juu kuwa mastermind aliprint ATM card, alighushi saini ya mteja hii kitu kwa baadhi ya bank hakiwezekani kabisa kwanza anaetunza card(custodian) ni mtu mwingine,ana initiate process ya kupewa card(maker) mwingine,anaechek kama kweli huyu mteja ni mwenyewe na kila kitu kipo sawa (cheker) ni mtu mwingine na kuna Authrorizer baada ya hawa watatu kufanya yote hayo then mtu wa mwisho ana authrorize mteja kupewa card jamani mchakato wote huo unafanywa within 5mins hii inasaidia zaidi local bank igeni hili muepukane na kadhia mnazowapa wateja wenu.
KIPI KIFANYIKE
Tunafahamu hakuna mshahara unaotosha lakini sector ya mabenk Tanzania local pamoja na international jaribuni kureview salary scale ya wafanyakazi wenu atleast mtu amudu kulipa kodi hata laki mbili kwa mwezi, wapewe trans allowance ili hata kama atajibana in 3yrs amudu hata kununua passo, meal allowance ikiwezekana hata communication allowance jamani wafanyakazi vipato vyetu ni tofauti na mfikiriavyo ninyi ni utanashati tu unatufanya tuonekane tunazo ila mambo sio kivile.
BANKERS acheni tamaa na kutaka kuishi maisha ambayo sio class yako hayo masubaru,crown, mark x bata za kila week end zitatuponza bankers hatuwezi kumudu tusiongopeane tukiforce ndo hayo ya bwana BABU. MUNGU saidia siku nitoke huku.
Ila cha ajabu kuna pipo zitapinga hapa