Mfanyakazi CRDB afikishwa Mahakamani kwa kumuibia mteja zaidi ya Tsh milioni 100 na kuzitakatisha

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
753
3,096
WhatsApp-Image-2019-09-27-at-11.29.47.jpeg
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Ubungo, Andrew Babu (27) na wafanyabiashara watatu, wameshtakiwa kwa kula njama, kughushi Tembo kadi ya mteja, wizi wa zaidi ya Sh milioni 100 na kutakatisha fedha hizo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, William Sige (52), Justina Boniphace (49) na Alli Tutupa (35) wote wanaishi jijini Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mbando alidai kati ya Oktoba 2018 na Aprili 19, 2019 washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka jingine imedaiwa, Oktoba 29, mwaka jana katika benki ya CRDB tawi la Ubungo, ndani ya manispaa ya Ubungo, mshtakiwa Babu peke yake kwa nia ya kulaghai au kudanganya, alighushi sahihi ya Charles Kihamia katika fomu ya maombi ya Tembo card.

Pia mshtakiwa Babu anadaiwa, Novemba 6, 2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika kitabu cha usajili kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Babu anadaiwa Novemba 5, 2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika usajili wa kadi ya visa ya Tembo, kwa madhumuni ya kuonesha kuwa sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Inadaiwa Novemba 6,2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika kitabu cha usajili wa uelekezaji kwenye fomu ya maombi kwa madhumuni ya kuonesha kuwa, sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Babu pia anadaiwa, Oktoba 29, 2018 huko katika benki ya CRDB, alitoa fomu ya kughushi ya maombi ya Tembo kadi kwa ofisa wa banki hiyo aitwaye Omary Mduyah kwa dhumuni la kuonesha kuwa fomu hiyo imetolewa na kusainiwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la mwisho, imedaiwa kati ya Novemba 7,2018 na Aprili 29,2019 washtakiwa hao kupitia kadi ya gold ya Visa, walijipatia sh. 106,267,907/- kutoka kwa Charles Kihamia kupitia Visa gold card huku wakijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kughushi na wizi.

Hata hivyo wa washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 10, mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi
 
Haya mabank ukiwa unatoa pesa nyingi usipokuwa makini wanakuliza, kuna siku nimeenda CRDB kutoa 9mill na laki7 nimehesabiwa tu nikaweka kwenye bag bila kuzihahikisha nikarudi mtaani kulipia biashara zangu hapo ndipo nilipogundua hakuna laki2 unusu pumbafu sana hawa jamaa
 
Huwezi ukaiba kitu ambacho kikipotea mtu atanotice. Kama unaiba milioni 100 hii inamaanisha unayemuibia ana zaidi, unless kama ulipanga kumuua ili asilalamike na usifuatiliwe.

Pia wazee wanaonyesha ni wazoefu ndiyo maana huyu dogo anaonekana yupo maeneo mengi. Hukumu kwao yaweza kua ndogo kushinda hata kwa huyo dogo. Askari wakifanya kumhoji dogo kwa utulivu atabreak easily.

Aliyewachoma hawa atakua mfanyakazi mwenzao au cctv cameras. I mean wao wamechongesha Atm card yenye access na akaunti ya mteja wameghushi sahihi n.k na wakaweza hadi kuchota pesa. Mteja angeenda lalamika angeonyeshwa utitiri wa docs na miamala aliyofanya kwa atm. Hapo ni ama cctv zimeibua maswali yaliyomchoma Babu au coworker kauza CD
 
Back
Top Bottom