Mfanyakazi anayetuhumiwa kuchoma korani huko Morogoro anahitaji msaada wa kisheria

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,585
22,184
Mkoani Morogoro kuna mfanyakazi wa halmashauri anadaiwa kuchoma kitabu cha Korani, katika hali ambayo si yakawaida anashikiliwa na jeshi la polisi na amenyimwa dhamana!

Tukio hili linaonesha serikali ndiye mlalamikaji! Hii si kawaida kwani huko nyuma waislamu walichoma moto kanisa la KKKT Temeke Dar es Salaam na serikali haikuwa mlalamikaji kwenye tukio hilo. Hivyo lilipita tu na kanisa kujigharamia ujenzi.

Kuna matukio ya Kigogo na mengine mengi tu ambayo yalifanywa dhidi ya wakristo lakini serikali haikuwa mlalamikaji!

Ni nini kimenfanya waziri ambaye naye ni muislamu kuamuru harakaharaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya mfanyakazi huyo.
 
Kwa mimi mtu akichana kitabu kitakatifu na kukitoa maana mimi wala siwezi kujali wala kumchukia huyo mtu kamwe ,

Labda huyo Mungu anaehusika hicho kitabu mwenyewe ajue namna ya kumhukumu.

Mungu anatakiwa ajitetee mwenyewe siyo kupiganiwa na wanadamu.

Mimi Mungu anayepiganiwa na wanadamu huwa napata mashaka na uwezo na nguvu zake.

Huyo mtu ni wa kumhurumia tu Mungu mwenyewe atajua naye amhurumie au amfanye nini


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu kuwa kwake ndani ndiyo salama yake !

Hawa wenzetu baadhi yao huwa hawanaga subra,
Ni watu wa visasi,
Swala la kusema ngoja tumwachie Mwenyezi Mungu atajua mwenyewe na mtu wake wengine hawanaga hiyo.

Halafu wengine unaona pengine ni watu wenye uelewa wa mambo lakini ikifika swala kama hilo utashangaa watakwambia jamaa anastahili kuuawa.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom