Mfanyakazi aliyepo masomoni Japan kwa miaka 13 kuchunguzwa/kushitakiwa

SUALA la kusaka watumishi hewa limeendelea kushika kasi nchini baada ya mikoa kadhaa kutangaza kuikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza kwa kina huku watendaji waliohusika wakisimamishwa kazi.

Mkoani Kilimanjaro, Mkuu wa Mkoa huo, Said Mecky Sadiki, ameagiza kusimamishwa kazi Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, William Msapali na kutaka Takukuru imchunguze mtumishi Agapit Chuwa aliyepo masomoni nchini Japan kwa miaka 13.

Sadiki, ameagiza Halmashauri ya wilaya ya Mwanga kumsimamisha kazi Msapali kwa madai ya kushindwa kutoa ushirikiano wakati wilaya hiyo ikihakiki watumishi hewa na kuwabaini 21 ambao wameisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 199. Alisema tuhuma nyingine kwa Msapali ni kushindwa kubainisha taratibu zilizomruhusu mtumishi wa sekta ya afya, Chuwa ambaye mwaka 2004 aliomba kibali kwenda masomoni nchini Urusi ambapo alijiongezea muda na sasa yupo nchini Japan huku akilipwa mshahara.

Sadiki aliitaka Takukuru pia kumchunguza mtumishi huyo aliyepo masomoni kwa zaidi ya miaka 13 kwani ameisababishia serikali hasara ya Sh milioni 54. Kutokana hilo, Sadiki alitaka taratibu kufanyika ili kusitisha mshahara kwa mtumishi huyo na kuitaka Takukuru kufanya uchunguzi wa kina ili kujiridhisha na baadaye kumfikisha mahakamani mtumishi huyo aliyepo masomoni na wengine wote walioisababishia serikali hasara.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jamhuri William alisema hakuna kumbukumbu za kutosha za taarifa za Chuwa ingawa alipewa ruhusa ya miaka mitatu kuanzia mwaka 2004.

Alisema mtumishi huyo alikuwa akijiongezea ruhusa kwa kushirikiana na maofisa Utumishi waliokuwapo ingawa baadaye tena alipewa ruhusa nyingine mwaka 2014 hadi 2016 kuendelea na masomo katika mazingira ya kutatanisha.

Alisema barua ya kuomba ruhusa ya mtumishi huyo iliandikwa lugha ya Kijapan lakini pia kwa Kiingereza ambacho hakikuwa kinasomeka vizuri jambo lililosababisha badala ya kupewa ruhusa ya miaka miwili, akapewa ya miaka mitatu.

Awali katika taarifa yake kwa mkuu huyo wa mkoa, Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaibu Ndemanga alisema wilaya hiyo yenye jumla ya watumishi 2,048 ilitambua watumishi hewa 21 walioisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 199.

Alisema walitumia hati ya malipo ya Septemba mwaka jana na kwenda katika kila ofisi kujua kama wahusika wapo ofisini ambapo 17 walikuwa wagonjwa, 14 waliomba ruhusa, 20 walikuwa likizo, 26 watoro, 26 walihama lakini bado walisomeka kwenye hati ya malipo.


CHANZO: Habarileo
ndipo hapo bwana chuwaaaaaaaaaaaaaaaa alipojiongezea likizo ya miaka miwiliiiii kwa barua aliyoandikwa kijapaniiiiiiii ambayo ilikuwa haisomeki vizuriiiiiiii na matokeo yake kuongezewa miaka mitatuuuuu badala ya miwiliiiiiii (nasako akiripoti!) nchi hii vituko havikomi n'gooooo
 
Anaenda Bachelor 3yrs, anaextend for masters 2 years, then PhD 5 years halafu anafanya internship 2 years. Mshahara unaingia. Akimaliza anaajiriwa huko huko
Na siku hizi vyuo vikuu havina noma, hata uwe kilaza kivipi PhD lazima uikwae tu, mradi karo unalipa!
 
tusimlaumu jamaa kwani kutokana na elimu yetu alishauriwa aanze darasa la kwanza hivyo anategemea kumaliza form six this year then atakuja kuripoti kidogo oficn halafu atarud tena kumalizia degree pia kumbuka analipwa mshahara kama kawaida...du nimechoka....
 
Mkuu, Ninasema siyo hoja kwa sababu hata mtoto wa darasa la nne anafahamu haya matatizo yamesababishwa na serikali ya CCM.

Kungekuwa na hoja kama kuna chama kingine kimewahi kushika madaraka ya nchi.
Mkuu tukiacha chama kama msimamizi mkuu wa serikali, kuna wahusika individual ambao ni wanachama wa vyama vyote na wengine hawana habari na chama chochote zaidi ya kuiba tuu. Na sidhani kama kuna mwizi wa watumishi hewa aliagizwa na ccm kufanya hivyo.
Kama kafahamika ni Chakaza au MsemajiUkweli ndio muhusika basi dawa ni mahakamani tuu. Ndio ilikuwa maana yangu
 
Inabidi mtu aliyepo utumishi wa umma akienda masomoni kama yupo sponsored mshahara wake usitishwe mapaka atakaporudi kuondoa double standard.
 
Usijedhani ccm walikuwa na nia ya kushughulika na uchafu huu ila wanaogopa nguvu ya upinzani inayoongezeka kila mwaka wa uchaguzi hawana jinsi
 
Hili zoezi la wafanyakazi hewa tutaona na kusikia mengi!

Kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango kumewaibua Wakuu wa Mikoa ambapo wamefahamu kwa sasa dhana ya business as usual ni historia katika serikali ya Rais Magufuli. You reap what you sow!

Kadri zoezi linavyofanyiwa uchunguzi zaidi ndivyo wafanyakazi hewa wanazidi kuongezeka
Dar wanakagua mtu kwa mtu ofisi kwa ofisi
 
Hili zoezi la wafanyakazi hewa tutaona na kusikia mengi!

Kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango kumewaibua Wakuu wa Mikoa ambapo wamefahamu kwa sasa dhana ya business as usual ni historia katika serikali ya Rais Magufuli. You reap what you sow!

Kadri zoezi linavyofanyiwa uchunguzi zaidi ndivyo wafanyakazi hewa wanazidi kuongezeka
Kuna watu walilaumu hatua ya rais kumfukuza mama Anne Kilango. Eti wanasema angempa onyo. Mimi nafikiri hatua ya kumfukuza imeleta na itazidi kuleta matokeo mazuri kwani tangu afukuzwe kuna wakuu wa mikoa wengine waliamua kurudia tena kusaka wafanyakazi hewa na wakawapata. Naomba sana rasi azidi kukaza uzi. Kuna tofauti kati ya uzembe na bahati mbaya. Wengi wa viongozi wetu wnafanya uzembe na siku zote kwa mtu mwenye akili uzembe hauna nafasi ya kupewa muda!
 
Back
Top Bottom