Mfanyabiashara: Wateja wengine miyeyusho tu

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,174
4,062
Leo nilienda duka fulani kununua mahitaji niliyokuwa nataka, wakati nachagua vitu akaaga mteja mwingine niliyemkuta kuwa ameona bidhaa atarudi hapo baadae.

Yule mfanyabiashara akasema kwa jazba, wateja wengine miyeyusho tu wanakuja dukani kutia nuksi tu hela hawana hawa ndio wachawi wenyewe hawa.

Mzee mwingine aliyekuwepo dukani akamwambia muuzaji, kuwa na lugha nzuri hiyo inatoa picha kuwa hata sisi tukitoka hapa bila kutimiza lengo ulilokusudia utatamka maneno machafu dhidi yetu, ivyo unanitisha nisiweze kurudi tena hapa.

Nikajiuliza ina maana mtu anayeingia dukani kwake ni lazima anunue bidhaa? Vinginevyo unakuwa nuksi, vipi kama ulichokusudia kununua hujavutiwa na ubora au bei yao imekuwa kubwa kuliko matarajio yako?

Hii ipo sana hata saluni za kike unakuta mteja katoka tu muhudumu wa saluni anaanza kumsema hii inawatisha waliopo wasirudi tena maana nao watasemwa vibaya wakitoka.

Nachotaka kuwashauri wafanya biashara, epukeni kutoa kauli chafu dhidi ya mteja aliyeondoka maana inatoa picha kuwa hata wao utawasemea mabaya tu wakitoka hapo.
 
Sasa kama hununui na bidhaa umeikuta dukani umeingia kufanya nini?nyinyi ndo wachawi wenyewe!$&@;()
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom