Mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aua kwa bastola Arusha

Atamnyoosheaje mtoto bastola kama sio alikuwa anataka damu ya mtu ili afanikiwe? ni upuuzi kwa sababu anajua idadi ya risasi alizoweka!? natuone hili igizo litaishia wapi..!!
 
Mamndenyi unachokisema ni kweli.
Mtoto keshakufa sasa, hata tukilia haitasaidia kitu chochote!

Cha msingi hapa ni huyo jamaa kuwajibishwa kisheria na ikiwezekana baba mtoto alipwe fidia.

Halafu inaonekana wakazi wa Arusha wanamiliki sana bunduki, hili nalo inabidi liangaliwe nani ana uhalali kichwani wa kumilikishwa hivi vyombo vya kuondolea uhai.
 
Last edited by a moderator:
nilikua naishi jiran na MANGA nilipanga opp na jumba lake kwakwel jamaa ni bandidu kikuda huwez kunkuta anacheka ni mweusi tii mwenye mwili jumba...matajir wa arusha sijui ni ushamba mana mnaweza mkawa bar akachomoa bastola akapiga hewan bila sababu anafurah kuona mnavyotimua mbio...kingine hiz silaha weng wanazipata kimagendo nlikua na rafik yangu polis field force alikua akinambia kama una laki 7.5 lete tykuuzie pistol nipo store rahis kuichomoa so vijana weng wa mawe wanamilik kijanja janja tu wanauziwa na askar kimagendo
 
Jana jumapili mathias manga na matajiri wa mawe walikwenda eneo la tukio kuwaomba wezee kimasai,Walikuta kundi kubwa la wamasai lika wakimbiza hadi kupotea walikuwa na bahati walikuwa hawakushuka kwenye magari.Mipango inayoendelea hivi sasa ni kumfuata mzee lowassa awatulize masai.
 
Msishangae kumuona huru .kwanza yuko rupango anapata huduma zote .hennesy .au jack daniel ndio kazi ya pesa
 
Money is scarce! Money is never enough. pesa nyingi kwako ni kiasi gani mamndenyi?

Huyu wala haina haja ya kufikiria sana kwamba anatumia nini katika kufikiri!

Mtu yeyote anaporuhusiwa kumiliki silaha nadhani huwa anapewa masharti na vigezo ili chombo hicho kisilete madhara...

Huyo bwana hakutumia akili kabisa katika jambo alilofanya, he deserves facing the law.

Tusubiri mrejesho kutoka mahakamani.

Kwanza ana bahati kwamba Wamasai walimuacha atoke eneo la tukio akiwa salama!!!!

Tiba
 
Mfanyabiashara wa madini ya tanzanite Arusha, Felex Manga amempiga risasi mtoto wa kimasai. Wakati akisherehekea kuuziwa shamba na baba yake eneo la Terati siku ya Jumamosi.

Siku ya tukio mtuhumiwa na familia ya aliyemuuzia shamba walifanya sherehe ya kumkabidhi shamba, ndipo mzee mwenye shamba alipomuuliza hivi vitu mnavyovaa kiunoni vinafanyeje kazi?

Ndipo jamaa akachomoa na kupiga juu kazaa bila kujua kuna iliyobaki akamnyooshea kijana kwenye paji la uso na kumtoa uhai, jamaa mpaka muda huu yupo ndani ndugu zake wakihaha kumtoa.


Kiburi cha pesa, mzaha mzaha hutumbua usaha
 
Back
Top Bottom