Mfanyabiashara wa Madini Arusha atekwa Akiwa mortuary..

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite jijini Arusha,Jeremiah Simion(49)Mkazi wa Sekei wilayani Arumeru,ametoweka katika mazingira ya kutatanisha na inahofiwa kutekwa na watu wasiofahamika.

Simoni ambaye pia ni mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa madini(Brokers) Mkoani hapa,anadaiwa kutekwa na watu wasiofahakika siku ya jumatatu ,January 28 mwaka huu majira ya jioni.

Kwa mujibu wa Mke wake aitwaye,Janet Jeremia,alidai kuwa mumewe alichukuliwa na watu hao wasiofahamika na kumfunga kitambaa cheusi usoni wakati akiwa katika eneo la Mochwale katika hospital ya mkoa ya Mount Meru alipokuwa akifanya maandalizi ya kununua jeneza la marehemu.

Amedai kuwa katika tukio hilo mbali ya mumewe kutekwa ,mtu mwingine aitwaye, Loth Greyson ambaye ni jirani yake naye alitekwa na watu hao wakiwa na Gari aina ya Rand cruiser Nyeupe ,hata hivyo baada ya siku moja Loth aliachiwa kwa sharti la kutozungumza chochote juu ya tukio hilo.

Janet amesema kuwa tangu siku hiyo hadi sasa hajui Mume wake alipo ila siku ya jumanne,January 29 mwaka huu,Simioni alimpigia Simu na kumweleza kuwa yupo salama na baada ya hapo hakuweza kupatikana tena kupitia mawasiliano hayo.

"Niliamua kwenda Polisi kutoa taarifa za kupotelewa kwa mume wangu na mpaka sasa sijuli alipo na ninasubiria vyombo vya dola kuweza kufanya uchunguzi" Amesema Janeth

Awali shuhuda wa tukio hilo ambaye ni Fundi wa kutengeneza Majeneza eneo hilo,Salimu Mzirai amesema kuwa tukio hilo limetokea siku ya jumatatu ya January 28,majira ya saa 5 asubuhi ,ambapo ilikuja gari aina ya Landcruser yenye rangi Nyeupe na waliteremka watu wapatao watatu na kuwachukua watu wawili akiwemo mfanyabiashara hiyo.

"Nikiwa kwenye eneo langu la kazi walikuja watu wawili wanaulizia jeneza na wakati wakiendelea kuchagua ghafla ilitokea gari nyeupe ,Rand cruiser na watu watatu waliteremka na kuwafuata wateja wangu na kuwachukua hadi kwenye Gari yao na kuondoka kwa mwendo kasi" Alisema Mzava

Naye kaimu kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani hapa,Longinus Tibushubwamu,amethibitisha tukio hilo na kueleza wapo katika hatua ya uchunguzi ila mfanyabiashara huyo yupo mikono salama.

"Nikweli tukio hilo lipo ila tambueni kuwa mfanyabiashara huyo yupo kwenye mikono salama " Amesema kaimu kamanda.

Naye kaka wa mfanyabiashara huyo aitwaye Joseph Simion,mkazi Simanjiro ,Manyara alisema ,alipata taarifa za kutoweka kwa mdogo wake siku ya jumatatu jambo ambalo limewaumiza sana na mwaka sasa familia haijui ndugu yao alipo.

Hata hivyo Loth alipopatikana hakuweza kuzungumzia tukio.hilo japo alithibitisha kutekwa na watu wasiojulikana na hakutambua walipelekwa wapi kwakuwa alikuwa amefungwa kitambaa usoni.

Habari za kuaminika zilizopatikana Jana jioni ni kwamba mfanyabiashara huyo amekutwa ametelekezwa jijini dar es salaam ikiwa ni siku kumi tangia kutekwa kwake akiwa na majeraha makubwa mwilini kwa kipigo na hivi sasa amelazwa katika hospital ya muhimbili kwa matibabu
FB_IMG_1549100413155.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana na moshware na mochwale

Inakuwaje awe ametekwa wakati kaimu kamanda, Tibushubwamu amethibitisha kwamba mtu yupo mikono salama?
 
Yaani haya mambo ombea yasikukute tu. Binamu yangu alichukuliwa na wasiojulikana mwezi wa kwanza lakini walimwacha huru baadaye. Hivyo ninavyohisi mimi ni kuwa wanaochukuliwa ni wengi ila wanaotangazwa ni wachache. Mwisho tuombe Mungu arudishwe salama.
 
Hivi kweli kp ww mtumishi wa Mungu kweli kuna faida gani mnateka watu mnawaua na kuwafanyia kila unyama ipo siku mtakuja pata adha hii iwe kwenu ama vizazi vyenu. Mmeua wangapi na mpk sasa hamjaridhika bado tu. Mtasingizia rogue elements ndani ya idara lkn mnafaham ukweli na unyama wenu
 
"Katekwa akiwa mochwari akinunua majeneza"
inamaana majeneza yanauzwa mochwari?
 
Back
Top Bottom