Mfanyabiashara wa madini akimbiza jambazi uchi wa mnyama,dunian kuna mambo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfanyabiashara wa madini akimbiza jambazi uchi wa mnyama,dunian kuna mambo

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, Oct 5, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  MFANYABIASHARA wa madini amejikuta akimkimbiza majambazi akiwa uchi baada ya majambazi hao kumpora madini ya dhahabu, fedha taslimu, gari na bastola yenye risasi 24.

  Mfanyabiashara huyo, Kilabasa Muhida ‘Chonza’, inadaiwa alivamiwa na watu watano juzi saa 1.30 usiku nyumbani kwake mtaa Katundu mjini Geita.

  Habari kutoka eneo la tukio zilizothibitishwa na Polisi wilayani hapa, zilisema Muhida alivamiwa wakati akirejea nyumbani kwake.

  Mke wa mfanyabiashara huyo, Milembe Nalya (42), alisema baada ya mumewe kuingia ndani na kupaki gari na kijana wake akirudi kufunga geti, ghafla walijitokeza watu nyuma ya nyumba na kuingia ndani.

  Alisema watu hao watatu ambao wawili kati yao walikuwa na bunduki, walizunguka gari na kusimama kwenye milango ya mbele na kumwamuru mumewe ashuke, huku wengine watatu wakiwa nje ya geti na mapanga na marungu.

  “Ndani ya gari alikuwamo mume wangu na mdogo wake, ambaye naye alikuwa mbele, majambazi walimfuata na kumwamuru afungue milango akatii amri.

  “Baada ya kushuka, walimpiga kwa kitako cha bunduki kichwani, mgongoni na kifuani, huku wakimwamuru atoe fedha na dhahabu alizokuwa nazo.

  “Nilikuwa nasikia wakimwambia ... ‘toa mauzo yote ya jana na leo (Jumamosi na Jumapili)’… lakini yeye alikuwa mbishi hakukubali,” alisema mama huyo.

  Alisema wakati mabishano yakiendelea, alikusanya watoto wote na kuwaficha jikoni na ****** na kusikia majambazi hao wakimwamuru mumewe waingie ndani, walipofika chumbani walitishia kumpiga risasi ndipo alipotoa fedha zote na dhahabu.

  Alisema baada ya mumewe kutoa fedha, majambazi hao walimvua nguo na ndipo bastola aliyokuwa nayo kiunoni ikadondoka.

  “Baada ya kumpora fedha walimvua nguo na kumwacha uchi na cha ajabu baada ya majambazi kuondoka naye alitoka ndani akiwafuatilia huku akisahau kuwa alikuwa uchi na akitwambia tusiwe na wasiwasi ni mzima, nilichukua kitenge nilichokuwa nimejifunga na kumfunga, nadhani alikuwa amechanganyikiwa kutokana na hali hiyo,” alisema mkewe.

  Akizungumza na gazeti hili, mfanyabiashara huyo ambaye alisema yeye na mdogo wake waliporwa Sh milioni 1.6, lakini alipotakiwa kueleza thamani ya dhahabu aliyoporwa alishindwa kuzungumza huku akionekana kulengwa na machozi.

  Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Geita, Paul Kasabago, alithibitisha tukio hilo na kueleza kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Kichunguza vizuri na hili jeshi letu huyo hapo juu ana genji lake nchi hii
   
 3. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hiyo bastola ni machine pistol nini Mkuu? Risasi 24?
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Umeipenda mkuu? Hiyo ngoma ningekuwa nayo mimi hao jamaa kuondoka na kitu ingekuwa utata!
   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nimeshangaa maana bastola ya kawaida haibebi risasi zote hizo. Ikiwa hivyo itahitaji extended magazine kama vile MP5. Bastola yangu inabeba risasi 18, na kitako chake ni kikubwa ili kuweza kuhifadhi magazine. Mtu mwenye mkono mdogo hawezi kuishika vizuri.
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  mpwa tema mate chini inategemea nani atamuanza mwenzake unaweza ukawa nayo ukabakia kuwa msukule na watu kuishia kukuaga kwenye ibada na siku hizi wala awasubiri jumamosi weekdays shwari wanakuchimbia jumamosi tunakula mpunga bana
   
 7. m

  mbezibeach Senior Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisikia Jeshi letu limesema linafanyia kitu uchunguzi...ujue kila kitu kimeishia hapo.
   
Loading...