Mfanyabiashara Said Mohammed Saad wa Home Shopping Center (GSM Foundation) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfanyabiashara Said Mohammed Saad wa Home Shopping Center (GSM Foundation)

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mongoiwe, Jun 1, 2012.

 1. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

  Utangulizi

  Mfanyabiashara Said Mohammed Saad anamiliki Kampuni ya Home Shopping Center iliyopo Kariakoo Mtaa wa Swahili na Msimbazi katika Jengo la Ghorofa lenye vioo vilivyochorwa picha za waigizaji wa Kikundi cha Orijino Commedy kinachorusha vipindi vyake Televisheni ya taifa ya TBC1.

  Mfanyabiashara huyu ambaye ana uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na Saud Arabia, anafanya uhalifu na kuhujumu uchumi nchi kwa kushirikiana na wafanyabiashara wengine wakubwa

  Tuhuma

  Mfanyabiashara Said Mohammed ameshiriki katika matukio mengi ya kihalifu yakiwamo ya kupiga risasi watu na kesi zake zimekuwa zikifunguliwa na baadaye anazizima kwa kutoa rushwa polisi.

  Moja ya matukio hayo ni kumpiga risasi mfanyakazi wake mwaka 2005 wakati akishusha bidhaa za kuuza dukani kutoka katika gari lake, kumpiga risasi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Vingunguti, Deo Vicent Agosti 15, 2006 saa 1:00 usiku Mtaa wa Msimbazi na Swahili Kariakoo jijini Dar es Salaam.

  Mfanyakazi wake alimpiga baada ya kumbishia Said kwamba hawezi kumpiga risasi kwa sababu anajua sheria za nchi haziruhusu kufanya hivyo. Alimpiga kuonyesha kwamba yeye yupo juu ya sheria za nchi. Kesi hiyo nayo aliimaliza kimya kimya kwa kumpa hela mfanyakazi huyo na ndugu zake na polisi.

  Mtoto Vicent yeye baada ya kupigwa risasi aliliripoti Polisi na baadaye alilazwa katika Wodi namba 17 Moi kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Alipigwa risasi ya mguuni wakati akipita karibu na duka la Said baada ya mashabiki wa Simba waliokuwa wakisherekea ushindi wa timu yao kupita katika eneo hilo.

  Hata hivyo, alimaliza kesi hiyo nje ya mahakamani kwa kuwapa hela wazazi wa mtoto huyo.

  Pia anamiliki genge la Wahalifu ambalo analitumia kumlinda na kuwaadhibu wapinzani wake au maadui zake akishirikiana na mdogo wake Ghalib Mohammed Saad.

  Kundi hilo linalojulikana kama Ze Popobawa ndilo ambalo Agosti mwaka huu lilitumika kumteka nyara Mlebanoni mfanyabiashara ambaye ana duka la vitu vya ndani Mtaa wa Morogoro karibu na makutano ya barabara za Morogoro na Bibi Titi na baadaye kumwingilia kinyume cha maumbile kisha kumpeleka kwa nguvu Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kumrejesha kwao Yemen kinyume cha taratibu.

  Kisa kilichofanya mfanyabiashara huyo ambaye yupo nchini kisheria ni kumpa mimba mdogo wa Said anayeitwa Salha bila ya kuoana kama zilivyotaratibu za mila zao za Yemeni.

  Mfanyabiashra huyo wa Mlebanoni ambaye awali alikuwa rafiki yake mkubwa na Said, amemfanya tangu tukio hilo litokee kuishi kwa kujificha kwa kuhofia kufanyiwa unyama mwingine na Said ambaye anaendelea kumtisha.

  Unyama mwingine

  Baada ya kumfanyia unyama mfanyabiashra Mlebanoni , Said hakuishia hapo bali aliamua kumwadhibu dada yake Salha kwa kumpiga. kumnyoa nywele zake zote na kumnywesha vidonge ambavyo havijulikani aina yake na alimpa kwa sababu zipi?

  Salha baada ya kufanyiwa nyama huo nyumbani kwao Msasani wilaya Kinondoni aliamua kwenda kuripoti polisi kituo cha Osterbay ambako lilifunguliwa jalada la kesi namba OB/RB/13915 ambayo ilifunguliwa Agosti 5 mwaka huu.

  Hata hivyo, mbali ya polisi kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini wanashangaa tangu Salha aripoti tukio hilo, hajarudi kituoni hapo wala simu yake mkononi ambayo aliicha namba zake kituoni hapo wakati akiandikisha maelezo haipatikani, kitu ambacho kinawapa wasiwasi.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye anasema huenda suala hilo wamelimaliza kifamilia. Ingawa kuna tariafa kuwa msichana huyo amewekwa kizuizini chumbani ambako haruhusiwi kutoka nje. Polisi kituo cha Oysterbay hawajafuatilia suala hilo kutokana na kupozwa kwa kupewa kitu kidogo rushwa na Said ili kuzima suala hilo.

  Ushirika wa kihalifu

  Kutokana na kushirikiana vyema katika shughuli za dawa za kulevya na kutorosha nyara za taifa wakimtumia Mfanyabiashara huyu, Said, Manji ameamua kumpa vijana wake wa Orijino Commedy kuwapa ufadhili wa kutangaza bidhaa zake anazoingiza nchini za mashuka na nguo.

  Hivi karibuni baada ya Manji kushiriki katika kuigiza mchezo wa kikundi cha Orijino Comedy kama mfanyabishara ambaye alikuwa akihitaji msaada wa kupata fedha za kufadhili Klabu ya Yanga na kuwapa wagizaji wa kikundi hicho kutumia ofisi yake kuigiza, Said naye wiki iliyofuatia aliwapa wana kikundi hicho nafasi kuingiza katika ofisi yake na kuwapa gari lake kulitumia.

  Wizi wa makontena bandarini

  1. Mfanyabiashara huyu anamiliki kampuni nyingi za Clearing and Forwarding ambazo hutumika kuiba makontena ya bidhaa anazoziingiza nchini kutoka nje na akishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa TRA.

  Hata hivyo, Kampuni hizi zimefungiwa baada ya kubaini kuhusika na wizi huo wa makontena, lakini kila inayofungiwa husajili nyingine Brela akitumia majina feki.

  Kampuni ambazo zimefungiwa na TRA kwa kuhusika na wizi wa makontena zaidi ya 30 kila moja ni Mbasi Clearing and Fowarding, Clinton Clearing and Forwarding, London Freight Forwarding, Exceptional Freight Forwaders na Upland Clearing and Forwarding.

  TRA imethibitisha kuzifungia kampuni hizo kufanya kazi ya Clearing and Fowading, kwa kutumia kifungu 145 (3) cha sheria ya Jumuia ya Afrika Mashariki ya utawala wa Forodha ya mwaka 2004.

  Hata hivyo, wamekataa kutaja majina ya wamiliki wa kampuni hizo wakisema Brela ndio wenye jukumu hilo. Ingawa wamekuwa wakikubali kuendelea kumhudumia mteja huyo huyo ambaye anaiba makontena na kufungiwa kampuni zake kisha anafungua nyingine chap chap kama uyoga.

  Hata hivyo, Brela kuna kumbukumbu ya kampuni mbili tu ambazo ni London Freight Fowarders Ltd yenye usajili namba 39834 iliyosajiliwa Agosti 15, 2000 ikionyesha wamiliki wake ni Angelo Peter mwenye hisa 2000, Richard Mulenga mwenye hisa 1500 na Abdulkarim Zaharan Salim mwenye hisa 1500. Kampuni hiyo ilianzishwa ikiwa na mtaji wa sh milioni 10.

  Kampuni nyingine za kwake zenye kumbukumbu Brela ni Exceptional Freight Fowarders Ltd ambayo wamiliki wake ni Lumba Nguku mwenye hisa 5,000 na Salim Suleiman mwenye hisa 5,000. Kampuni ilianzishwa ikiwa na mtaji wa sh milioni 10.

  Dawa za kulevya na kutorosha nyara

  Mfanyabiashara huyu anajihusisha na uingizaji wa dawa za kulevya nchini kwa kushirikiana na mfanyabiashara Manji wakitumia kampuni zake za Clearing and Fowarding ambazo huiba makontena yenye dawa hizo yanapoingia bandarini.

  Mfanyabiashara huyu ni mmoja wa watu waliotajwa katika orodha ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya iliyowasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2006 akitajwa kama Said Abuu mfanyabiashra wa Kariakoo.

  Nyara za taifa

  Mfanyabiashara huyu amekuwa akitumia kampuni zake kusafirisha makontena yenye nyara za taifa kwenda Vietnam, Philipiness na Malaysia akishirikiana Manji na Rostam Aziz ambaye pia ni mmiliki vitalu vya uwindaji. Kampuni ya Rostam ya Uwindaji inaendeshwa na mdogo wake anayeitwa Akram.

  Ili kufanikisha mtandao wao huo wana watu wao katika sehemu nyeti za TRA, bandari, Polisi na usalama wa taifa unaowalinda kwa hali na mali.

  Utajiri wa kutisha

  Kutokana na Said kujihusisha na biashara hizo haramu kwa muda mfupi tangu mwaka 2004 alipoanza hivi sasa ana utajiri wa kutisha. Anamiliki nyumba sita eneo la Kariakoo pekee.

  1. Moja ipo Swahili na Msimbazi, Ghorofa saba ambayo ameamua kuipangisha watu sehemu ya juu, lakini TRA akidaganya kwamba ni hoteli ili kukwepa kulipa kodi.
  2. Congo na Agrey ghorofa sita,
  3. Uhuru mkabala na shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa bado inajengwa ni ya ghorofa,
  4. Livingstone na Uhuru ipo,
  5. Mkunguni Kariakoo Sokoni karibu na dula la Azam Ice Cream ghorofa sita,
  6. Lumumba karibu na CCM makao makuu limepakana na Hospitali ya Burhan.
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha majungu wala nini.

  Hii habari ni ya kweli. Ninawaomba waandishi wa habari wale ambao huwa hawana tamaa ya mlungula wafuatilie haya mambo polisi na kutafuta wale wahusika wote waliopigwa risasi ili ukweli ujulikane kwa umma. Watu wa aina hii hawatakiwi Tanzania hii.

  Ndiyo maana tunahitaji rais atoke tena chama kingine ili kwanza awashughulikie criminals wote na wahamishwe nchini. Kwanza kabisa waweke katika katiba mpya kuwa investor yeyote akihusika na criminal acticvities apigwe PI na mali zake zichukuliwe na serikali. Mbona huko nchi za wengine PI zipo, Tanzania ni shamba la bibi au.

  Watanzania tuamke, saa ya ukombozi ni sasa! Nimeumia sana kwa kusoma habari hii.

  Goooo night with tears! I love my country!!
   
 3. Shilinde Nicholaus

  Shilinde Nicholaus Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aisee!
   
 4. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Du!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Shughuli pevu iyo! Kwa mantiki nyingine HSC ni biashara anayoitumia kusafisha hela sio?

  Je records zake zinasema hana mkopo benki yoyote?

  Mtaji wa biashara yake ambayo inaonekana ni legit, ambayo ni HSC alipata wapi?

  Idara za juu za TISS zinampango gani na mtu huyu?

  Nzowa anasemaje pia?

  Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo, ila za mwizi arobaini, lazma atanasa tu siku moja!
   
 6. Elisha Ray

  Elisha Ray JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 302
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  si mchezo duh!!
   
 7. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 771
  Trophy Points: 280
  wacha nikagonge castle lite nimeechanganyikiwa vibaya
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Huyu bwana si ndio alikuwa mstari wa mbele kuwasaidia wahanga wa mafuriko uya jangwani?

  Hizi tuhuma naona zinaletwa karibu kila wakati lakini hakuna linaloendelea...si unajua tena tumelala usingizi wa pono
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Twanga twanga mpe makavu mpe makavu jamaa fisadi.
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Umeongea mengi sana kuhusu Said kuna ya ukweli kuhusu majengo lakini mengine naona una sababu zako binafsi...halafu ilo ghorofa unalosema lipo Swahili na Udoe sio Swahili na Msimbazi Mbona huyo RPC wa siku nyingi sana mkuu.

  Mkuu kama mzalendo na unapenda nchi yako kwa nini huu ushahidi wako usipeleke polisi.
   
 11. M

  MTANGANYIKA ORIGINAL Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Majungu tuu na fitina ilovuka mipaka! Kama una ushahidi kwa nini usipeleke kunapohusika ili hatua za isheria zikafuatwa au unatumiwa na mshindani wake wa kibiashara?
   
 12. salito

  salito JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  mhh..naona chenga..
   
 13. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,291
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Watu wanamiliki vikampuni uchwara lakini ni matajiri wa kutupwa, kumbe hivyo vikampuni wanatuzuga, na kumbe wanavitumia kusafishia pesa zao chafu...
   
 14. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  .....................mwenzangu !!!!
   
 15. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ............. mbona imeelezwa hapo kuwa "Ameir Jeshi" anazo taarifa ! Au kuna Polisi anakizidi hicho cheo !? Msiingie humu na "mning'inio"
   
 16. b

  bob68 Member

  #16
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Umeshaandikiwa hapo kwa ufafanuzi wote mtz badala uje na hoja yako ya msingi unasema wivu,majungu,kwa kuangalia typing error tu,si lazima upinge kila kitu na maelezo yameeleka hapo!!
   
 17. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #17
  Jun 3, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  Detailed.....Interesting.....by the way huyu jamaa hana muda mrefu atapita kwenye crosshairs za wakibosho wa kariakoo.....huko hakuna msamaha a watch out
   
 18. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Huyu bwana bado tu anadunda mtaani-hivi uchafu kama huu kwa mtanganyika kama mimi mweusi unaweza kuufanya Yemen au sehem nyingine/na ukawa bado upo tu-kama si kiuwa na viongozi wabovu kwenye kila sekta hapa nchini
   
 19. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,315
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  JAMAA AMEANDIKA

  Kundi hilo linalojulikana kama Ze Popobawa ndilo ambalo Agosti mwaka huu lilitumika kumteka nyara Mlebanoni mfanyabiashara ambaye ana duka la vitu vya ndani Mtaa wa Morogoro karibu na makutano ya barabara za Morogoro na Bibi Titi na baadaye kumwingilia kinyume cha maumbile kisha kumpeleka kwa nguvu Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kumrejesha kwao Yemen kinyume cha taratibu

  RAIA WA LEBANON KARUDISHWA KWAO YEMEN

  KAZI IPO
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Tumechoka na majungu bana wivu wa kike tu.
   
Loading...