Mfanyabiashara, raia wa Kenya anayeishi nchini, Raphael Ongangi apatikana akiwa Mombasa nchini Kenya

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,444
3,354
Kwa mujibu wa Mke wake, Veronica Kundya kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram amesema kuwa mume wake Raphael amepatikana leo Mombasa na yupo salama. Amesema hana tarifa zaidi ya hiyo ila pia inatosha sana kwake kujua mume wake yupo salama

=====

Nipo hapa leo nikiwa na furaha kubwa sana sana kuushuhudia UKUU WA MUNGU 🙏🙏🙏
.

My Raphael AMEPATIKANA leo Mombasa na yupo salama , sina taarifa ingine zaidi ya hio ila hio pia INATOSHA sana kwangu 🙏🙏🙏 .

Sina mengi ya kusema zaidi ya KUMSHUKURU MUNGU sana sana kwa kuwa yeye ni Mungu wa miujiza maana ametenda 🙏🙏🙏
.

Napenda KUWASHUKURU WOTE kwa moyo wangu wote kwa niaba ya familia yangu kwa sala na kujitoa kwenu kwa hali na mali kwenye kipindi hiki kigumu .

Mimi na familia yangu tutaishi kutangaza ukuu wa Mungu 💃💃💃💃💃
.

Mungu azidi kutubariki sisi sote na familia zetu 🙏🙏🙏

Zaidi, soma Mfanyabiashara Raphael O. Ongangi atekwa na watu wasiojulikana! Ni aliyekuwa Msaidizi wa Zitto

.
66f22227af8d8d618190594db4183f7f.jpg


12934E7A-ABBF-478C-9DEC-B80A54A31C0F.jpeg
 
Mombasa tena? Wamemvusha kwa kutumia nini? Majini au nchi kavu? Kutoka Masaki hadi Mombasa...Khaaaa! Yani hii nchi kwa sasa ingekua inawezekana kuhama kwa muda mpaka hawa washamba waondoke ningehama aisee...

Kuna mambo yanaendelea huwezi kuamini kama ni Tanzania yetu hii hii tuliyoizoea siku zote... Eeehh Mungu tulinde waja wako
 
Back
Top Bottom