Mfanyabiashara na Kanisa wameuza kiwanja cha msikiti Buguruni Malapa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfanyabiashara na Kanisa wameuza kiwanja cha msikiti Buguruni Malapa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sharrif2, Jan 3, 2009.

 1. s

  sharrif2 Member

  #1
  Jan 3, 2009
  Joined: Sep 5, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waislamu wa MMmasjid Hawa Buguruni wanadai kwamba kuna njama imefanyika kati ya Kanisa na mfanyabiashara mmoja jijini ambaye kauziwa kiwanja kilichokuwa sio mali ya Kanisa ili kuepusha kujengwa msikiti karibu na eneo hilo.

  Ingawa mahakama tayari imetoa oda (injunction) ya kusimamisha ujenzi wa Kituo cha Mmafuta kinachojengwa na mfanyabiashara huyo pembeni ya ule mfereji maafufu wa maji machafu pale malapa bado mfanyabiashara huyo anaendelea na ujenzi.

  Inavyoonekana ni kuwa mfanyabiashara huyo akitumia maofisa wa juu jijini amekuwa na jeuri na kiburi ya kuendelea na ujenzi huo kwa sababu nyeti za ukaribu wake na wakubwa nchini.

  Hivi sasa Waislamu hao wanafuatilia kwa karibu madai yao na ajabu ya kuona amri ya mahakama inadharauliwa na mahakama haichukui hatua zozote!
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mods peleka hii kwenye Udaku na Kuvunja Mbavu..
   
 3. a

  akili Member

  #3
  Jan 3, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi sasa Waislamu hao wanafuatilia kwa karibu madai yao na ajabu ya kuona amri ya mahakama inadharauliwa na mahakama haichukui hatua zozote!

  Hizi ni habari za uhakika na inavyoelekea mfanyabiashara huyo ana 'tafu' kubwa toka juu maana amedharau kabisa injunction na hakuna Meya, Mkuu wa wilaya wala wa mkoa ambaye ameagiza ashughulikiwe ipasavyo. Kiasi ambacho msikiti unatafuta mlango wa kuingia kwa Waziri Mkuu Pinda kumfahamisha juu ya hili.

  Maana sio tu kuwa wameibiwa kwa kuzungukwa bali peteroli stesheni yenyewe inajengwa katika maeneo nyeti ya makazi ya watu na sehemu ya kituo cha basi na shule kadhaa zenye maelfu ya wanafunzi!
   
 4. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  The information contained in this thread is defacto, ad infinitum.

  Mwandishi ameshindwa kusema ni Kanisa gani limeuza kiwanja cha Msikiti au Waislam. Mwandishi ameshindwa kusema mnunuzi ni nani. Mwandishi ameshindwa kusema, ni kwanini Waislam hawakufungua kesi ya kuuza mali ya wizi against the Church. Mwandishi ameshindwa kusema ni kwanini Waislam hawakufungua kesi against the purchaser kwa ununuzi wa mali ya kitapeli.

  Hakuna njama yeyote hapa zaidi ya kutaka uchochezi wa kidini, kamailvyo utamaduni na jadi ya Waislam.

  Mwisho, habari hii haina uhusiano na Wanasiasa wala siasa au Kanisa, kama kichwa cha habari kinavyo dai.
   
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naomba mkuu alieleta hii mada hapa airipoti vema, maana kuripoti vibaya ni kuleta implication tofauti na Tukio au Hali Halisi ya mahala Husika.
   
 6. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,703
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mimi nina maswali yafuatayo:

  1) Kanisa litafanyaje njama ya kuuza kiwanja ambacho si chake? Ninavyojua mimi kanisa lina sehemu kubwa sana pale Buguruni. Kama ni sehemu ya eneo lake, sioni sababu ya wao kufanya njama kuiuza maana ni haki yao. Kama si chao, sioni watafanyaje njama kuiuza! Watakachokua wamefanya ni aidha ushauri ( si kosa) au utapeli ( kosa la jinai). Kutusaidia, aliyeleta taarifa angesema bayana kiwanja kilikuwa cha nani? Au kilikuwa hakina mwenyewe bali ilikuwa ni sehemu ya wazi kwa matumizi ya jamii yote? Basi aelezee.

  2) Ni nani aliyelalamika mahakamani na kuhusu nini? Na ni mahakama ipi iliyotoa court injuction? Kwa nini mlalamikaji asi-appeal kwa mahakama ya juu yake kama anaona hiyo iliyotoa hiyo injuction haina meno?

  3) Hao waislamu wanaofuatilia kwa karibu wanahusika vipi na kiwanja hiki? Ni cha kwao? Kwa ujumla wao au cha mmoja wao?

  4) Hao walikusudia kujenga huo msikiti walionyeshaje kusudio lao? Jee waliisha tayarisha michoro na kuwasilisha kwenye mamlaka husika ili wapate kibali cha ujenzi?

  5) Je huyo anayeendeleza ujenzi ana kibali cha ujenzi? Kama anacho basi ni lazima aliwasilisha ushahidi wa kumilki ile sehemu wakati anaomba kibali cha ujenzi.

  Kwa jinsi hili suala lilivyoletwa limekaa kizushi. Kuna haja ya kutoa ufafanuzi zaidi.

  Amandla.....
   
 7. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Asante Mkuu. Jamma hawana ufafanuzi, ni wazushi na waongo wa kawaida.
   
Loading...