Mfanyabiashara Moshi Ajimwagia Petroli na Kujipiga Kiberiti

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,511
lnawezekana likawa tukio baya lililoacha gumzo na simanzi baada ya mfanyabiashara wa mjini Moshi, Romani Shirima (74), kujiua kwa kujilipua kwa petroli nje ya nyumba yake.

Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli na kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake.

Ingawa hakuna taarifa rasmi ya nini kiini cha mfanyabiashara huyo kuchukua uamuzi huo mgumu ulioacha maswali mengi, lakini baadhi walidai ni msongo wa mawazo uliotokana na madeni.

Hili ni tukio la pili kwa mfanyabiashara mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, kwani miaka kadhaa iliyopita, mfanyabiashara anayemiliki hoteli eneo la Marangu alijilipua kwa petroli akiwa katika gari lake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 11.25 asubuhi maeneo ya Mjohotoni.

Alisema, mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa shule ya sekondari ya Merinyo iliyopo mjini Moshi, na kusema kuwa aliamka asubuhi nyumbani kwake na kujimwagia mafuta hayo na kisha kujilipua na kiberiti.

Kamanda Mutafungwa alisema chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika ingawa kuna maneno yanayoongelewa na watu, lakini hawawezi kuyachukua moja kwa moja na kwamba jeshi hilo linachunguza ili kubaini chanzo chake.

Taarifa za tukio hilo la aina yake zimekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na vitongoji vyake, hasa njia aliyoitumia kukatisha uhai wake.

Chanzo: Mpekuzi
 
Ametumia busara ya hali ya juu kujipiga mshkaki nje ya nyumba. Safi kabisa marehemu Shirima RIP.
 
Maamuzi ya jinsi hio husukumwa na nguvu nyingine kubwa nje ya utashi wa kawaida wa kibinadamu
Ni kweli mkuu si kawaida kujiua kwa namna hiyo kisa madeni. Ila nakumba tukio moja lilitokea kwa Mjomba wangu wakati huo, alikuwa anadaiwa na CRDB, NBC, NMB, EXIM BANK na EQUITY BANK. Baadae biashara ziligoma, alikuwa na gari 4 za daladala, shule ya nursery na Maduka makubwa ya vifaa vya ujenzi. Baada ya madeni kuzidi alikimbia mji na kutokomea kusiko julikana, alipatikana baada ya mwaka 1 kukatika akiwa kichaa, mpaka leo hii ajitambui kafilisiwa kila kitu.
 
lnawezekana likawa tukio baya lililoacha gumzo na simanzi baada ya mfanyabiashara wa mjini Moshi, Romani Shirima (74), kujiua kwa kujilipua kwa petroli nje ya nyumba yake.

Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli na kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake.

Ingawa hakuna taarifa rasmi ya nini kiini cha mfanyabiashara huyo kuchukua uamuzi huo mgumu ulioacha maswali mengi, lakini baadhi walidai ni msongo wa mawazo uliotokana na madeni.

Hili ni tukio la pili kwa mfanyabiashara mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, kwani miaka kadhaa iliyopita, mfanyabiashara anayemiliki hoteli eneo la Marangu alijilipua kwa petroli akiwa katika gari lake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 11.25 asubuhi maeneo ya Mjohotoni.

Alisema, mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa shule ya sekondari ya Merinyo iliyopo mjini Moshi, na kusema kuwa aliamka asubuhi nyumbani kwake na kujimwagia mafuta hayo na kisha kujilipua na kiberiti.

Kamanda Mutafungwa alisema chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika ingawa kuna maneno yanayoongelewa na watu, lakini hawawezi kuyachukua moja kwa moja na kwamba jeshi hilo linachunguza ili kubaini chanzo chake.

Taarifa za tukio hilo la aina yake zimekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na vitongoji vyake, hasa njia aliyoitumia kukatisha uhai wake.

Chanzo: Mpekuzi
Naomba tumpe support jaman,maana sept 1 mmh
 
Back
Top Bottom