Mfanyabiashara Maarufu Z'bar Kizimbani kwa "kui-EPA" PBZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfanyabiashara Maarufu Z'bar Kizimbani kwa "kui-EPA" PBZ

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Jul 19, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  WAFANYABIASHARA watano wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kuiibia Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) mamilioni ya fedha akiwemo mfanyabiashara Maarufu Nassor Said Nassir (Bopar) anayemiliki maduka kadhaa ya bidhaa mbali mbali visiwani Zanzibar.
  Mfanyabiashara huyo maarufu Zanzibar Mkaazi wa Kiembe samaki Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja anadaiwa kuiibia Benki ya Watu wa Zanzibar dola 880,000 kwa kushirikiana na mwenzake Sleyum Mbaraka.
  Mwendesha mashitaka katika kesi hiyo iliyosomwa katika mahakama ya Mkoa Vuga Mjini, Khamis Suwedi alisema wafanyabiashara hao wawili walitenda kosa hilo mnamo Machi 11 mwaka huu baada ya kula njama na kuiba fedha hizo kinyume na sheria.
  Bopar ni mfanyabiashara maarufu Zanzibar mwenye asili ya Asia aliyekuwa akiingiza bidhaa za mchele, unga wa ngano, na bidhaa nyenginezo katika soko la ndani la Zanzibar ikiwemo mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na serikali ya mapinduzi Zanzibar.
  Waliofikishwa mahakamani jana na kusomewa shitaka la kuiba fedha za Benki ya Taifa ni Juma Abass Juma (44) mkaazi wa Amani anayetuhumiwa kuiibia PBZ dola za Marekani 341,220,000 mwengine ni mfanyabiashara Ramadhan Issa Jecha (47) mkaazi wa Mwanakwerekwe ambaye anatuhumiwa kuiibia Benki hiyo fedha taslimu milioni 379, 240,000.
  Akisoma mashitaka hayo mwendesha mashitaka huyo alisema washitakiwa kwa nyakati tofauti walifanikiwa kuiibia benki hiyo kwa njia za udanganyifu vitendo ambavyo ni kinyume na sheria ya makosa ya jinai
  Mwendesha mashitaka Khamis Suwedi alieleza mahakamani hapo kwamba wafanyabiashara hao Juma Abbas Othman na Zahor Mbaraka Salum kwa kushirikiana walifanikiwa kuiibia PBZ dola za Marekani 340,000,000
  Akisoma hati ya mashitaka alisema kitendo hicho kimefanyika kati ya Machi 11 na 19 bada ya wahusika kutenda kosa la wizi na kufikishwa mahakamani hapo ambapo mshtakiwa Sleyum Mbaraka naye alidaiwa kuiibia benki hiyo kati ya Machi 12 ba 19 dola za Marekani 1,220,000
  Washitakiwa wamerejeshwa rumande katika gereza la Kiinua Miguu Kilimani Mjini Unguja, baada ya upande wa mashitaka kupinga maoni ya dhamana kwa vile kiwango cha fedha kilichoibwa ni kikubwa ba kuwepo kwao nje kunaweza kuathiri hatua za uchunguzi za kesi hiyo.
  Hata hivyo Hakimu Mkusa Issac Sepetu alisema suala la dhamana kwa washitakiwa hao atalitolea uamuzi Julai 28 mwaka huu.
  Awali wakili anaemtetea mshitakiwa Bopar Hamid Mbwezeleni aliitaka mahakama kumuangalia mteja wake kumpatia dhamana ili kuepusha shughuli zake za biashara kuathirika katika kipindi atakachokuwepo ndani.
  Benki ya Watu wa Zanzibar ndio inayotumiwa na idadi kubwa ya wakulima na wafanyabiashara kuhifadhi fedha zao lakini hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya kupotea fedha katika akiba za wateja ambapo hivi karibuni zaidi ya milini 200 ziliibwa katika mazingira ya kutatanisha kutoka katika akaunti ya mfuko wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa kambi ya upinzani waliofungua katika Benki hiyo.  SOURCE: ZANZIBAR YETU.
   
 2. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  umeipata habari hii. kwani jana ilikuwa jumamosi hamna mahakama na hamna kazi na wewe umeipost leo jumapili.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Bopar ameshawatesa saaana ndo wanamshika saivi, pana jambo hapa. Madudu ya Mfanyabiashara huyu anaebebwa na viongozi wa SMZ kwa mbeleko ya chuma, ni makubwa tu, kwanza, ni bingwa wa kuwaletea wananchi mchele na unga mbovu, mchafuzi mkubwa wa mazingira(karibuni tu iliripotiwa kuwa waziri mmoja wa SMZ alimbeba kwa kumsaidia kupata kibali cha kuingiza mifuko ya Plastiki iliyopigwa marufuku visiwani kwa uchafuzi wa mazingira), Bopar huyu anakiburi cha ajabu, bandarini akitaka hata "unga wa kokeni" ataingiza na serikali na mkemia mkuu watathibitisha na utauzwa kama wa ngano. Bopar hajasahaulika mwaka juzi Baraza la wawakilishi kupitia wajumbe wa CCM, wakiongozwa na Mh.Shamsi Nahodha(CM), walipomkingia kifua na kumtetea kwa nguvu zote asiundiwe tume ya kuchunguza uingizwaji wa mchele mbovu, na Mkemia Mkuu wa Serikali akaja na taarifa kuwa ni maguni sita tu kati ya elfu kadhaa za bidhaa hiyo yalikuwa na mchele mbovu, yaliyobakia ni saaafi tu, wananchi wakauziwa sumu ile bukheeeri wa afya!!!
  Mbaya zadi ni kuwa vikosi vya usalama vilitumika kuhakikisha kuwa bidhaa ile mbovu inatolewa salama bandarini na ikatoka.
  Kukamatwa kwake bado kunaleta maswali kwamba ni kweli?? maana haiwezekani "nyumba kubwa" isipate habari, tusubiri tuone.
   
 4. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jee chanzo cha habari hii ni wapi?
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Jamani source hamuioniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kwa 'Da Salma' kule.
   
 6. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ukiona hivyo kuna kambi yenye nguvu imemshughulikia sababu anaiunga kambi pinzani mkono katika suala la uchaguzi ujao ZNZ.
   
Loading...