Mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite apanda kizimbani kwa utapeli ,atupwa magereza

Arusha Leo

Senior Member
Mar 12, 2012
122
72
Mfanyabiashara maarufu wa Madini ya Tanzanite mkazi wa jijini Arusha,Eliakimu Daud Molle(45),amepandishwa kizimbani katika mahakama
ya hakimu mkazi Arusha akikabiliwa na shitaka la kufanya utapeli na kujipatia madini ya thamani ya shilingi milioni 15 kwa njia ya udanganyifu.


Ilidaiwa kuwa mfanyabiashara Mollel alimrubuni mlalamikaji Banai Shininu kuwa ampatie madini hayo na kwamba angeenda kuuza kwa bei nzuri na baadae angemletea kiasi cha shilingi milioni 15,ikiwa ni thamni ya madini hayo, hatua ambayo hakufanya hivyo badala yake alitoweka kusikojulikana.



Mahakama ilielezwa kuwa mshtakiwa alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na mlalamikaji na punde anapopatikana hutoa ahadi za uongo kuwa angelipa kiasi hicho cha fedha lakini hakufanywa hivyo hadi alipokamatwa na kufikishwa mahakamani.


Baada ya kusomewa shtaka hilo la kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu,mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo .


Hata hivyo hakimu Baro alimweleza mshtakiwa kwamba dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na fedha tasilimu kiasi cha shilingi milioni 7.5,na wadhamini wawili wanaofahamika hatua ambayo mshtakiwa alishindwa kutimiza na kulazimika kwenda magereza.
 
Sijaona ubilionea wake ikiwa ameshindwa kupata mtu wa kumdhamini kwa hiyo hela.
 
Kuwa serious mleta thread mfanyabiashara maarufu wa madini atapeli 15m? Pia kakosa wadhamini wa 7.5m wawili? Hauko serious badili heading.
 
Kwa hiyo na huku Moshi vijijini Massawe akimtapeli Mushi pesa za kahawa sh.milioni 10 nitaruhusiwa kufungua Uzi kwenye jukwaa hili?
 
Haya sasa masihara. ......7.5m inakosekana kweli?

Au sio mfanyabiashara wa ma madini ya tanzanite tunayoyajua. ....
 
Back
Top Bottom