Mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite apanda kizimbani kwa utapeli ,atupwa magereza

Arusha Leo

Senior Member
Mar 12, 2012
122
72
Mfanyabiashara maarufu wa Madini ya Tanzanite mkazi wa jijini Arusha,Eliakimu Daud Molle(45),amepandishwa kizimbani katika mahakama
ya hakimu mkazi Arusha akikabiliwa na shitaka la kufanya utapeli na kujipatia madini ya thamani ya shilingi milioni 15 kwa njia ya udanganyifu.


Ilidaiwa kuwa mfanyabiashara Mollel alimrubuni mlalamikaji Banai Shininu kuwa ampatie madini hayo na kwamba angeenda kuuza kwa bei nzuri na baadae angemletea kiasi cha shilingi milioni 15,ikiwa ni thamni ya madini hayo, hatua ambayo hakufanya hivyo badala yake alitoweka kusikojulikana.



Mahakama ilielezwa kuwa mshtakiwa alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na mlalamikaji na punde anapopatikana hutoa ahadi za uongo kuwa angelipa kiasi hicho cha fedha lakini hakufanywa hivyo hadi alipokamatwa na kufikishwa mahakamani.


Baada ya kusomewa shtaka hilo la kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu,mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo .


Hata hivyo hakimu Baro alimweleza mshtakiwa kwamba dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na fedha tasilimu kiasi cha shilingi milioni 7.5,na wadhamini wawili wanaofahamika hatua ambayo mshtakiwa alishindwa kutimiza na kulazimika kwenda magereza.


 
Back
Top Bottom