Mfanyabiashara maarufu Arusha na Manyara atiwa hatiani kwa kuuza madini bila leseni

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Mwandishi wetu, Arusha

Mahakama ya Hakimu Mkuu Mkazi Mkoa wa Arusha imewatia hatiani wafanyabiashara wawili wa madini ya Tanzanite kwenda jela miezi 24 au kulipa faini ya jumla ya shilingi milioni 163 kwa kosa la kufanya biashara bila leseni na kuuza madini nje ya soko lililotengwa na serikali kama sheria inavyosema .

Wafanyabiashara waliotiwa hatiani ni pamoja na ,Sanare Saireku{43} Maarufu kwa jina la Mulla Mkazi wa kata ya Moita Bwawani wilayani Monduli Mkoani Arusha na mwenzake Lanaito Loiko{51} mkazi wa Nadosoito wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Mulle ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya madini ya Muller Gems Stone na mwenzake Loiko{51} ambao ni ndugu walikutwa na hatia baada ya kukiri makosa mbele ya Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Arusha,Martha Mahumbuga aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.

Washitakiwa baada ya kukiri mashitaka yaliyosomwa na Mwendesha mashitaka wa serikali,Innocent Njau kwani Muller alishitakiwa kwa makosa mawili moja alikutwa na maofisa wa wizara ya madini march 14 mwaka huu ofisini kwake Kaloleni ndani ya Jiji na Mkoa wa Arusha katika jengo na Shirika la Hifadhi ya Taifa{NSSF] kushindwa kuwa na kumbukumbu za madini aliyokutwa nayo na kushindwa kuwasilisha nyaraka kwa wizara ya madini

Shitaka la pili alilosomewa Muller ni kuwa machi 15 mwaka huu katika ofisi zake zilizopo katika jengo la NSSF alikutwa na kosa la kushindwa kutunza madini katika kasha maalumu {self} aina ya Tanzanite kilogramu 45.3 na kareti 19.3 yenye thamani ya dola za kimarekani 751 sawa na fedha za kitanzania shilingi milioni 1.7 kinyume na sheria ya madini yam waka 2018.

Mwendesha Mashitaka wa serikali alimsomea mshitakiwa wa pili Laitoi Loiko shitaka moja la kukutwa na madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilogramu 269.5 yenye thamani ya dola za kimarekani 20,500 sawa na fedha za kitanzania zaidi ya shilingi milioni 47 akiuza nje ya soko la madini katika bar ya Uzunguni City Park katikati ya Jiji la Arusha wakati akijuwa wazi kufanya hivyo ni kinyume na sharia.

Mulle na Loiko walikiri mashitaka hayo mbele ya Hakimu na Hakimu Mahumbuga alimtia hatiani Mulla kwa shitaka la kwanza la kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya shilingi milioni kumi na shitaka la pili kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya shilingi milioni kumi kama sheria inavyoelekeza.

Hakimu Mahumbuga alimtia hatiani mshitakiwa wa pili Loiko kwenda jela miezi 12 au kulipa faini ya shilingi milioni 143 kwa makosa mawili moja kufanya biashara bila ya kuwa na leseni na pia kufanya biashara nje ya soko la madini lilotengwa na serikali .

Baada ya maelezo hayo ndipo Hakimu Mhambuga alipomtia hatiani Muller shitaka la kwanza miezi sita au kulipa faini ya shilingi milioni kumi na shitaka la pili jela miezi sita au kulipa faini na shilingi milioni kumia na mshitakiwa wa pili yeye alikutwa na makosa mawili hivyo alitiwa hatiani kwa kwenda jele miezi kumi na mbili au kulipa faini ya shilingi milioni 143.

Washitakiwa walilipa faini hapo hapo Mahakamani kwa namba maalumu ya benki inayotumika kulipa faini ya jumla ya shilingi milioni 163 na kuachiwa huru na kuamsha shangwe na vifijo kwa jamii ya kimasai iliyokuwa imejazana mahakamani hapo kumsaidia mwenzao aliyekumbwa na mashitaka hayo.

Mwisho

Pichani chini: Mfanyabiashara Mulla Oleshangiki akisindikizwa na askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha kuelekea chumba cha mahakama ili kusikiliza kesi inayomkabili yeye na mwenzake.

IMG-20200327-WA0070.jpeg
IMG-20200327-WA0066.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom