Mfanyabiashara Maarufu Arusha, anyongwa hadi kufa nyumbani kwake

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mfanyabiashara maarufu wa mchele katika Jiji la Arusha anayefanya shughuli za bidhaa hiyo katika mtaa wa Ndovu katikati ya Jiji, Benadeta Chuwa {74} ameuawa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi juzi usiku nyumbani kwake kwa kunyongwa na shuka yake hadi kufa na kuporwa fedha ambazo hazijajulikana idadi yake.

Kwa mujibu wa ndugu na majirani wa marehemu nyumbani kwake Kaloleni mita 200, Jijini Arusha walisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 usiku juzi kufuatia majambazi wapoingia ndani ya nyumba ya marehemu kwa kuruka uzio na kujificha kabla ya kufanya mauaji.

Majirani walisema mfanyabiashara Chuwa huwa na tabia ya kuacha funguo kwa jirani mwenye kibanda cha vinywaji vikali na kawaida ikiwemo bia {Grocery} na kwenda katika shughuli zake za kibiashara mtaa wa nduvo na kurudi kila siku majira ya kati ya saa 1.30 hadi saa 2 usiku.

Ndugu na majirani walisema majambazi hao ambao inaonekana walikuwa wakifuatilia nyendo za marehemu walisema walifika katika kibanda hicho cha bia majira ya saa 1 usiku na kuanza kunywa kumbe walikuwa na lao jambo la kumsubiri marehemu.

Mmoja wa ndugu wa marehemu Chuwa alisema kuwa maraehumu alifika majira ya saa 2.30 usiku na kuchukua funguo zake na kuingia ndani baadae alitoka na kwenda katika kibanda hicho kunywa bia lakini alirudishia mlango kwa kuwa ni karibu sana na alipokuwa akipata kinywaji.

Alisema majambazi wawili walitoka eneo la kinywaji na kuingia kwenye nyumba ya marehemu na kujificha ndani ya nyumba hiyo lengo likiwa kutenda walichokusudia kwa mfanyabiashara Chuwa.

Majirani walisema majira ya saa 4.30 usiku marehemu Chuwa alipopata bia na kukata kiu aliaga na kwenda kulala ili kesho aweze kuwahi majukumu ya kikazi kama kawaida yake.

Alisema aliingia na kufunga mlango baada ya dakika 15 hivi majambazi hao yalimvamia akiwa kitandani na kumtisha wakitaka awapatie fedha lakini bibi huyo alikuwa mbishi kwa kutoa fedha kidogo ndipo jambazi mmoja alipoamua kuviringisha na shuka yake na kuanza kumnyonga hadi mauti na kufanikiwa kutoweka na pesa na vitu vyenye thamani ambavyo thamani yake bado haijajuliana hadi sasa.

Baada ya tukio hilo kufanyika na wahusika kutoka katika nyumba ile na kukimbia hovyo waliokuwepo katika kibanda cha bia walishtuka na walipoingia ndani kwa marehemu walimkuta tayari ameshakufa na walifanikiwa kutoa taarifa polisi na majira ya saa 8 usiku polisi walifika eneo la tukio na kubeba mwili wa marehemu na kuhifadhi katika chumba cha maiti cha hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.

‘’Ni tukio la kuhuzunisha marehemu hana shida na mtu ni mtu mkarimu san ana asiyekuwa na makuu na hawa wauaji walikaa sana hapa nje kwenye kibanda cha bia kumbe wanayao ‘’alisema jirani wa marehemu

Mmoja ya wajukuu zake waliokuwa wamelala.katika chumba kingine katika nyumba ya marehemu alidai kwamba alisikia mtu akijibishana na marehemu Bibi yake akitaka apatiwe fedha lakini marehemu alitoa sh,elfu kumi tu ndipo baadaye alisikia kelele za Bibi na baadaye alimwona mtu huyo akitoka kwenye chumba Cha marehemu na kuja kwenye chumba chao na kuchungulia na baadaye akitoka nje na kuruka ukuta.

Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Justini Masejo hakuweza kupatikana kuzunguzia zaidi tukio hilo kwani simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa muda wote.

Mwisho
 
Alisema aliingia na kufunga mlango baada ya dakika 15 hivi majambazi hao yalimvamia akiwa kitandani na kumtisha wakitaka awapatie fedha lakini bibi huyo alikuwa mbishi kwa kutoa fedha kidogo ndipo jambazi mmoja alipoamua kuviringisha na shuka yake na kuanza kumnyonga hadi mauti na kufanikiwa kutoweka na pesa na vitu vyenye thamani ambavyo thamani yake bado haijajuliana hadi sasa((MAREHEMU NDIYO ANAELEZEA AU??))
 
Mimi mwenyewe nimeshangaa sana.

Haya maelezo either yanatokewa na marehemu ama mtu aliekuwepo kwenye tukio.

Marehemu kuacha mlango wazi, jambazi 2 kutoroka kwenda kuingia ndani na kujificha, majambazi kunywa bia.

Marehemu kua mbishi, kunyongwa na hadithi zote hizo ni lazima anaezitoa awe marehemu ama mmojawapo ya majambazi.
 
Alisema aliingia na kufunga mlango baada ya dakika 15 hivi majambazi hao yalimvamia akiwa kitandani na kumtisha wakitaka awapatie fedha lakini bibi huyo alikuwa mbishi kwa kutoa fedha kidogo ndipo jambazi mmoja alipoamua kuviringisha na shuka yake na kuanza kumnyonga hadi mauti na kufanikiwa kutoweka na pesa na vitu vyenye thamani ambavyo thamani yake bado haijajuliana hadi sasa((MAREHEMU NDIYO ANAELEZEA AU??))
Me nimeshindwa kabisa kuyaelewa hayo maelezo. Yani matukio yanavyosimuliwa kama walikuwepo😃
 
Mbona kama msimuliaji alikuwepo from A to Z mpaka mpango wa tukio anaujua fika.

Watu wawili wanaingia ndani na kujificha yeye yupo kimya tu!! Haya bibi yake anakuja nae kuingia hapo hapo walipoingia majambazi nae yupo kimya tu hata kumstua!!

Daah inasikitisha sana R.I.P bibi
 
Alisema aliingia na kufunga mlango baada ya dakika 15 hivi majambazi hao yalimvamia akiwa kitandani na kumtisha wakitaka awapatie fedha lakini bibi huyo alikuwa mbishi kwa kutoa fedha kidogo ndipo jambazi mmoja alipoamua kuviringisha na shuka yake na kuanza kumnyonga hadi mauti na kufanikiwa kutoweka na pesa na vitu vyenye thamani ambavyo thamani yake bado haijajuliana hadi sasa((MAREHEMU NDIYO ANAELEZEA AU??))
Jambazi aliyefanya mauaji ndiyo aliyeleta huu uzi
 
Back
Top Bottom