Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 158
- 175
Mfanyabiashara jijini Mwanza Pravin Shah anatuhumiwa kuingiza sukari kwa magendo
Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, Pravin Shah anatuhumiwa kuingiza sukari kwa njia ya magendo na kuiuza kwa bei nafuu.
Shah ambaye ni wakala wa bidhaa mbalimbali anadaiwa kuingiza shehena kubwa ya sukari kwa njia ya magendo kutoka nchi jirani kwa nia ovu ya kukwepa kodi ya Serikali.
Mfanyabiashara huyo kwa muda mrefu amekuwa akiingiza sukari kwa njia ya magendo kukwepa kodi ya Serikali akishirikiana na baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Ukwepaji huo wa kodi, unatajwa kama njia yake ya kuuza sukari kwa bei ya chini huku wafanyabiashara wenzake (mawakala) wakiuza kwa bei ya juu kutokana na kufuata taratibu za uingizaji wa sukari.
Kufuatia tatizo Hilo, ni vyema Serikali kuangalia mwenendo wa biashara za Shah na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi yake.
Mbali ya sukari Shah pia ni wakala wa saruji, mabati, sabuni, vyombo vya plastiki ambapo ni miongoni mwa bidhaa nyingine huku ofisi zake kuu zikiwa barabara ya nyerere jijini humo.
Wakati huo huo, kiwanda cha nondo cha Sayona still kinachomilikiwa na Shah kinalalamikiwa kwa kuchafua mazingira kwa kutupa vyuma taka ovyo jirani na makazi ya watu.
Inaelezwa kwamba uongozi wa kiwanda hicho ulishaonywa na watalaamu wa afya na mazingira kuondoa vyuma hivyo nje ya kiwanda, lakini mpaka sasa uongozi huo umekaidi agizo hilo la serikali.
Baadhi ya wakazi jirani na kiwanda hicho kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilalamika kuhusu uchafuzi huo wa mazingira na wengine wamekuwa wakipeleka malalamiko kwa mamlaka tofauti ili kuchukua hatua kwa kiwanda hicho.
Wananchi hao wanataka vyuma taka hivyo, viondoke kwenye makazi yao ili kuwaondolea hatari ya kiafya inayoweza kusababishwa na vyuma hivyo vinavyotupwa hovyo.