Mfanyabiashara jamaa ya Mbunge akamatwa na Shehena ya Madawa ya Kulevya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfanyabiashara jamaa ya Mbunge akamatwa na Shehena ya Madawa ya Kulevya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jembe Ulaya, Apr 27, 2011.

 1. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu wa mbunge anaswa na shehena ya Cocaine, Heroine

  na Mwandishi wetu

  MFANYABIASHARA anayedaiwa kuwa ni kinara wa biashara ya dawa za kulevya nchini, amenaswa na shehena ya dawa za kulevya aina ya Heroine na Cocaine.

  Mfanyabiashara huyo, ametajwa kwa jina moja la Asad na anadaiwa kuwa na uhusiano wa kindugu na mmoja kati wabunge maarufu nchini, mwenye asili ya Kiasia.

  Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema kuwa mfanyabiashara huyo alinaswa na dawa hizo za kulevya nyumbani kwake, Mikocheni na kiasi kingine kilinaswa Kabuku, mkoani Tanga.

  Mmoja wa maafisa wa polisi wanaohusika na kitengo cha kupambana na dawa za kulevya, aliliambia gazeti hili kuwa mfanyabiashara huyo alinaswa mkoani Arusha, akijaribu kuwatoroka polisi waliokuwa wakimsaka kwa muda mrefu.

  Kwa mujibu wa habari hizo, mfanyabiashara huyo ambaye ni mmoja wa vigogo wa biashara hiyo amekuwa akisakwa na polisi kwa muda mrefu na kuwatoroka mara kwa mara.

  "Amekamatwa na kiasi kikubwa cha Heroin Kabuku Tanga, alikamatwa pia na shehena nyingine ya dawa za kulevya aina ya Cocaine nyumbani kwake Mikocheni na mwenyewe amekutwa mjini Arusha akiwa kwenye harakati za kuwatoroka polisi," kilisema chanzo chetu cha habari.

  Akithibitisha kukamatwa kwa mihadarati hiyo, Kamanda wa Kikosi cha kupambana na dawa za kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kukamatwa kwa kigogo huyo.

  Alisema mfanyabiashara huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho mjini Tanga kujibu tuhuma hizo.

  Hata hivyo hakuwa tayari kueleza mahusiano ya kigogo huyo na mbunge mmoja maarufu nchini kwa madai kuwa taarifa zote zitapatikana mahakamani hapo.

  "Kweli tumemkamata na kiasi kikubwa cha mihadarati na kesho (leo) atafikishwa mahakamani mkoani Tanga. Taarifa zingine zote za uhusiano wake na mbunge uliyemtaja, mtazipata mahakamani hapo kesho," alisema Kamanda Nzowa.

  [Source Tanzania Daima]


  MY TAKE: Rostam ana mdogo wake anayeitwa Asad anayeishi Mikocheni, pia anamakazi Tanga na Arusha. Huyu alihamia Tanzania kutoka Iran kama miaka kumi iliyopita akiwa hana senti mfukoni. Ghafla ameibukia kuwa bilionea baada ya kujiunga na biashara za kaka yake. Ama Rostam anahusika moja kwa moja na hii biashara au ni mfadhili wake. Sasa tuone kama haki itatendeka au kaka mtu ataingilia na kusawazisha mambo. Tuvute subira kazi kwako IGP.
   
 2. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,414
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  kweli wamepania wameanza kumtosa hii ina maana huko nyuma biashara ilikuwa ikifanyika kama ya halali
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kesi itaota mbawa

  hakuna kitu hapo
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  haswaa,ukumbuke tanga kuna kesi ya unga wa thaman ya zaid ya billion,hadi keo haijasikika tena
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,699
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  wekeni mambo hadharani,je? Kakutwa na Kg ngapi. Rostam ndio unaandamwa mpaka ujivue gamba na kurudisha fedha zetu
   
 6. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,175
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Naamini hii kesi atashinda tuu kama kweli ana uhusiano na Rostam, maana Rostam ni mtu makini sana kama anaweza kuchangia CCM ishinde kwa ghalama yeyote ile sembuse kikesi cha madawa ya kulevya?
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi miezi kama mitatu hivi hapo nyuma si ilikamatwa shehena nyingine huko Kabuku na ilihusisha ndugu zetu wenye asili hiyohiyo? Leo tena? Wanatumaliza. Nakumbuka siku ya Ijumaa nilikuta Polisi wameweka barrier pale kabuku na kusimamisha kila gari na kuikagua, huenda waliweka mtego wa kuwanasa hao wanmihadarati. Wakamatwe tu hata kama wana uhusiano na Mungu manake wanatumalizia vijana wetu. Safari hii haponi mtu hapo manake naona Serikali imeamua na liwalo na liwe na ukitana kumuua nyani usiangalie sura!! Ukimwaga mboga tunatia mchanga kwenye ugali!
   
 8. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  duh Rostam amewashiwa indicator anatakiwa either achepuke or avute sox , ila pa kuchepukia ndiyo ishu hv chama gani kitampokea ?
   
 9. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  TIME WILL TELL and now has started to TELL, who is real R.A
   
 10. m

  mang'ang'a JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
   
 11. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #11
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama Ndugu Yake na Rostam ni usanii wa CCM kutaka mkutishia ili ajivue Mwenyewe magamba kwani wameshindwa kufanya hivyo.HATUTKI ,Kama kutoswa atoswe kwa ufisadi wa. Ccm EPA ,Richmund,Dowans,kagoda vinginrvyo CHANGA LA MACHO
   
 12. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  JK v RA ... Round 2.. FIGHT!
   
 13. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  This is best strage ... to xpose filth game plaid by Rostam Aziz
   
 14. X

  XLP New Member

  #14
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Shida kubwa tuanyoipata ni namna ya kujinasua kutoka kwenye shamba la bibi na kuanza kumiliki shamba letu wenyewe. Kesi kama hizi haziwezi kufikia muafaka hata siku moja ikiwa asilimia kubwa ya viongozi ni wafanyabiashara kwani wanalindana hawa... Kwa hiyo tukiweza kurudisha nchi kwa wamiliki ambao ni wakulima na wafanyakazi, kulindana kutapungua kwa kiasi kikubwa.
   
 15. The Kop

  The Kop JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 208
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  JK alisema wafanyabiashara wa madawa ya kulevya anawafahamu, na alisema anawapa mudawajirekebishe...hapo kama kuna mkono wa RA hakuna kesi ni usanii tu....lets wait an' see....!
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yalipaswa kufanywa siku nyingi sana. kikwete amekuwa akijua haya mambo siku zote lakini hamna hatua yoyote, kuna yule Mbunge wa Singida Mjini sijui anauza nini yeye? Hata Ubunge wake sijui ni wa nini?

  Anyway hata kama wamechelewa lakini kama wameanza hatuna budi kuwaunga mkono katika kila jambo jema.

  Shime Polisi kama Wana-siasa hasa Rais hata waingilia tena na pia nanyi hamta tuuza tena kufidia mishahara yenu midogo, Mt: Polisi kuweni sehemu ya jamii katika kudai haki maana ndio msingi halisi wa kazi zenu, katika nchni iliyojaa haki waarifu pia upungua mara dufu.
   
 17. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mwenzenu nina ndoto yangu iko hivi, ntachukua fisi mkubwa tu na mzimaaa wa afya tele na kumweka kwenye gunia akiwa mzima akikukuruka haalafu nampeleka pale ktkt ya kariakoo na kutangazia walala hoi wenzangu kuwa nimempata RA na kumtia chini ya ulinzi na ndiye huyu ndani ya gunia hili...nimemleta hapa mtoe uamuzi...... je fisi wangu huyo ndani ya gunia atapewa muda wa kujitetea kwamba yeye sio RA?
  NI NDOTO TU!
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,613
  Likes Received: 5,783
  Trophy Points: 280
  mkuu akuna kitu hapo mchanga wa macho jamaa wanamshikilia huku wanafanya makubaliano huyo mkuu wa madawa ya kulevya ni mshenzi tu mwingine wa serikalini kaama wangejua anachangia sana kueendelza magonjwa ya madwa haya..kwanza hata kuteuliwa kwenda airport lazima uwe na idhini yake na ufwate masharti yake ikiwemo hawa unaona leo wamekamatwa wamesindikizwa sana sana na polisi mpaka kwenye ndege ndani ..so huo upuuzi aupotezee tuuu asitulete wenye uelewa
   
 19. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  angekuwa ni mlalahoi kaiba kuku fasta angepigwa miaka. kwa vile kaka yake mtuhumiwa alikuwa ndio gamba ambalo limevuliwa tutaona atakavyoshughulikiwa. wafanya biashara haramu wote mwisho wao hauwezi kuwa mzuri
   
 20. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ni mbunge ambaye bunge lililopita hakuuliza swali hata moja wala kuchangia na akashinda kwa kishindo. wakati wa kampeni nakumbuka msanii alimshika mkono akasema wanaomuita fisadi walie tu, yeye ni msafi na ccm tunajua usafi wake. Ghafla Nape anaimbaimba bongo fleva za wavuta bangi
   
Loading...