Mfanyabiashara Bilionea wa China Jacky Ma yupo nchini Tanzania

Kaka Pekee

JF-Expert Member
Apr 3, 2018
336
559
Wiki Iliyopita nilipokuwa Nasafiri kwenda Serengeti na familia kupitia Mwanza, baada ya kutua na AirTanzania uwanja wa Ndege Mwanza majira ya Saa mbili kasoro Asubuhi...nilivutiwa na ndege moja Private Jet (Pichani)iliyokuwa imepaki pembezoni mwa kiwanja kwa ninavyozifahamu ndege (As Rubani wa Private small Chartered Flights) hakika ilikuwa si ya mchezo.

Nikashawishika kuuliza kwa Rafiki yangu mmoja pale uwanjani ambaye alinitonya kuwa ni ya Bilionea maarufu wa China Jack Ma (Mmiliki wa Alibaba) ambaye ameingia kuelekea Hifadhi ya Serengeti kupitia Gurumeti Migration Camp,Ikoma ambayo pia ni kambi matata kwa watu wazito na bilionea mbalimbali( Hoteli hii ndio aliyofikia Obama alipotembelea Serengeti) ambapo kuna sehemu ya camp za hadi Dola 9'000/$ kwa night. Na kwa sehemu za kawaida fee yetu kama wazawa ni Kuanzia Dola 500$ Kwa night.

Vigogo hawa huingia nchini kimyakimya (Laying Low) sababu ya Usalama lakini wakati wanaondoka tungeweza kuomba kuwatumia ili kutangaza Utalii wetu tungenufaika sana Kimataifa kutangaza vivutio vyetu.

89FCD464-2542-4C7F-9CB4-A02BE3510790.jpeg

Mwaka 2017 tajiri huyu alitembelea Masai Mara Kenya (Angalia Picha Chini) ambapo wakenya walitumia fursa hiyo vilivyo kujitangaza.
8EBDC1F6-60C0-459F-AB7D-1E130D18FCA7.jpeg
 
Sikubahatika kuonana naye kaka sababu mimi ni mtu mdogo sana, ila labda Unataka nikuambie kuwa hadi kitabu cha kusaini wageni pale VIP lounge niliona Sahihi yake. Hiyo inatosha nadhani.
Mengine ni Confidential kaka
Kwa hiyo hukuonana naye? Je kama upiingizwa chaka?
 
Futa title hiyo andika alikuwepo hili sio gazeti la ijumaa kwamba umeandika hivyo ili uvutie wasomaji
 
Wiki Iliyopita nilipokuwa Nasafiri kwenda Serengeti na familia kupitia Mwanza, baada ya kutua na AirTanzania uwanja wa Ndege Mwanza majira ya Saa mbili kasoro Asubuhi...nilivutiwa na ndege moja Private Jet (Pichani)iliyokuwa imepaki pembezoni mwa kiwanja kwa ninavyozifahamu ndege (As Rubani wa Private small Chartered Flights) hakika ilikuwa si ya mchezo.

Nikashawishika kuuliza kwa Rafiki yangu mmoja pale uwanjani ambaye alinitonya kuwa ni ya Bilionea maarufu wa China Jack Ma (Mmiliki wa Alibaba) ambaye ameingia kuelekea Hifadhi ya Serengeti kupitia Gurumeti Migration Camp,Ikoma ambayo pia ni kambi matata kwa watu wazito na bilionea mbalimbali( Hoteli hii ndio aliyofikia Obama alipotembelea Serengeti) ambapo kuna sehemu ya camp za hadi Dola 9'000/$ kwa night. Na kwa sehemu za kawaida fee yetu kama wazawa ni Kuanzia Dola 500$ Kwa night.

Vigogo hawa huingia nchini kimyakimya (Laying Low) sababu ya Usalama lakini wakati wanaondoka tungeweza kuomba kuwatumia ili kutangaza Utalii wetu tungenufaika sana Kimataifa kutangaza vivutio vyetu.

View attachment 1025140
Mwaka 2017 tajiri huyu alitembelea Masai Mara Kenya (Angalia Picha Chini) ambapo wakenya walitumia fursa hiyo vilivyo kujitangaza.View attachment 1025162
Tanzania si tunaambiwa na ufipa na kamanda lissu hakukaliki! Kaingiaje huku machafukoni?
 
Back
Top Bottom