Mfanyabiashara alalamika kuhujumiwa kesi ya Ardhi

waziri2020

Member
May 31, 2019
75
150
Mkuu wa mkoa wa zamani Arusha, Daniel Njolaay kwa kushirikiana na jaji Mstaafu jina linahifadhiwa ,wameingia kwenye msuguano Mkali wakituhumiwa kupanga njama na kuhujumu kesi ya Ardhi dhidi ya mfanyabiashara Philemon Mollel.

Taarifa zaidi zinadai kwamba Njolaay ambaye alikuwa pia mwenyekiti wa bodi katika hospital ya Seliani na kufukuzwa, kwa maslahi yake binafsi akishirikiana na mfanyabiashara Anselin Ninja na mbunge wa Arusha Mrisho Gambo wanadaiwa kufanya kikao Cha Siri Klabu Africo iliyopo eneo la Kimandolu jijini ARUSHA.

Inaelezwa kwamba kikao hicho ndicho kiliadhimia kubadili mwenendo wa kesi baada ya Njolaay kuahidiwa sh,milioni 100 iwapo Monaban atafanikiwa kupokonywa eneo hilo.

Waliadhimia Monabani apokonywe eneo lake lenye ukubwa wa ekari mbili alilowekeza kituo Cha mafuta Jambo ambalo jaji aliyeendesha kesi hiyo alitoa maamuzi hayo na kumpa ushindi William Taitas Mollel.

Kikao hicho kilifadhiliwa na mfanyabiashara mwenye asili ya kiarabu anayemiliki kampuni ya mafuta ya Lake oil na ndiye anataka kununua eneo hilo.

Siri ya kikao hicho imevuja baada ya mmoja ya washirika wa kikao hicho atibua Siri baada ya kubaniwa mgawo wa fedha walizoahidiwa

Monaban anaeleza kwamba amelimiliki eneo hilo kwa zaidi ya miaka 14 akiendesha shughuli za kiuchumi lakini ameshangaa mtu asiyejulikana kumfungulia kesi ya madai mahakamani wakati nyaraka zote za umiliki anazo.

Kesi hiyo kwa Sasa ipo mahakama ya rufaaa ambapo wiliam kwa kushirikiana na Njolaay wanafanya mbinu mpya kupitia jaji Mstaafu ili kuonana na majaji wa rufaa waweze kutoa ushindi kwa William Taitas Mollel kutwa eneo hilo.
 

Ulweso

JF-Expert Member
May 24, 2016
17,676
2,000
Kibano kianzie kwa huyo huyo mtoa taarifa ya kikao cha siri, na je kama angepata huo mgawo hiyo siri angeitoa?
 

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
3,794
2,000
Aisee Balozi mzee Njoolay ninayemfahamu hawezi kufanya mambo ya kushoto kabisa unless facts zipo tofauti kuhusika kwake.
 

tweenty4seven

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
12,704
2,000
Hilo eneo monaban alitapeli,unawezaje kununua eka mbili ngulelo kwa hela mbuzi yani mali ya familia wewe unampa mmoja pesa za bia....bdae unajimilikisha watu wengi walimuonya kua hilo eneo aachane nalo,yeye ni tamaa n ubabe ndio umemponza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom