Selous
JF-Expert Member
- Jan 13, 2008
- 1,325
- 144
MFANYABIASHARA maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amri Amir, amefariki dunia ghafla wakati akihojiwa na maofisa wa Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini (TRA).
Tukio hilo lililoteka hisia za wananchi wengi wa mkoani Kagera, hususan wilayani Karagwe, lilitokea juzi wakati maofisa hao wa kodi kutoka Mwanza, walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kuangalia kiasi cha kodi anachodaiwa mfanyabiashara huyo.
Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Salewi, zilisema kuwa, Amir alifariki dunia wakati akiwa katikati ya mahojiano na maofisa hao wa TRA, ambao waliamua kutimka mara baada ya kifo hicho.
"Ni kweli Amir alifariki wakati akihojiwa na maofisa wa TRA. Wakati akiwa katikati ya mazungumzo ambayo bado hatujui yalisema nini, mfanyabiashara huyo alianguka ghafla, wengi wakihisi kuwa ni presha na baadaye alifariki dunia papo hapo. Naomba uweke sawa kwamba hakupigwa, bali alianguka ghafla na kufa," alisema Kamanda Salewi.
Alisema kutokana na utata wa kifo hicho, kamanda huyo kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu, walikubali kutofanya mazishi jana ili kupisha uchunguzi uliofanyika jana.
Kamanda huyo alisema aliamuru kufanyika kwa uchunguzi wa mwili huo ili kuondoa wasiwasi ulioenezwa kuwa huenda alipigwa au amelishwa kitu chenye sumu.
"Bahati nzuri uchunguzi umefanyika leo (jana) na mazishi yamefanyika kijijini kwake, ila sijapata matokeo ya majibu kwa vile niko nje ya ofisi, tukiwasiliana kesho, nitakupa," alisema kamanda huyo.
Hata hivyo Kamanda Salewi hakuweza kutaja majina ya maofisa hao wa TRA kwa madai kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Habari zaidi kutoka Karagwe, zinasema kuwa mfanyabiashara huyo ambaye pia alikuwa mweka hazina wa CCM, wilaya, alikuwa mfadhili mkubwa wa CCM wilayani humo na kifo chake ni pigo kwa chama hicho tawala.
Mfanyabiashara huyo anayemiliki vituo vya mafuta mkoani Kagera na Mwanza, amekuwa mfadhili mkubwa wa chama hicho, kutokana na michango yake aliyoitoa mara kadhaa katika kukiwezesha, hasa wakati wa uchaguzi.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa tukio la kuanguka na kisha kufariki dunia akiwa anahojiwa, baada ya jambo kama hilo kutokea mwishoni mwa miaka ya 1990, wakati aliyepata kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba, alipofikwa na mauti wakati akihojiwa na Kamati Kuu ya chama hicho tawala mjini Dodoma.
Source: Tanzania Daima