Mfanyabiashara adai fedha zake Sh. milioni 399.8 kuchotwAi Benki ya Barclays tawi la Morogoro

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
barclays_logo_2480.jpg











Benki ya Barclays



Benki ya Barclays tawi la Morogoro imekumbwa na kashfa baada ya wafanyazi wake kwa nyakati tofauti kuchota kwenye akaunti fedha za mteja wake Sh. milioni 399.8.

Wizi huo unadaiwa kufanywa kati ya Septemba 2012 hadi April mwaka huu kwenye akaunti namba 0096000138 ya mteja huyo ambaye ni wafanyabiashara maarufu wa mjini Morogoro.

Mfanyabishara huyo, Ajay Gokal, alisema alibaini wizi huo mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuona fedha katika akaunti yake zikipungua siku hadi siku na kuamua kuomba taarifa ya fedha kwenye akaunti yake Novemba mwaka jana na kubaini kuwapo kwa upungufu wa Sh. milioni 119 na kuamua kuomba taarifa ya mwaka mzima.

Gokal ambaye ni mfanyabiashara wa moja ya kampuni ya simu ya mikononi, alisema baada ya kuomba taarifa ya mwaka alikuwa akizungushwa na uongozi wa benki hiyo hali iliyomlazimu kwenda kufungua jarada katika kituo cha polisi.

Alisema alilazimika kufanya hivyo kutokana na risiti za wateja wake walizoingiza fedha katika akaunti yake kuonyesha kuna fedha ziliingizwa, lakini kwenye akaunti hazionekani.

“Nina risti za benki hiyo kutoka kwa wateja wangu niliowapa mzigo na kuniingizia fedha hizo, lakini nikienda kuangalia katika akaunti hiyo sioni hizo fedha nikawafata wanipe taarifa za fedha wananizungusha mpaka nikaenda kufungua jarada katika kituo cha polisi,” alisema Gokal.

Alisema baada ya kufungua kesi maafisa wa Jeshi la Polisi waliamuru uongozi wa benki kumpatia taarifa hizo kwa kuwa ni haki yake, lakini cha kushangaza ilikuwa ikimpatia miezi miwili huku mingine ikirukwa.

Alisema baada ya kupitia kumbukumbu hizo toka Novemba mwaka jana hadi Aprili 13 mwaka huu, alibaini kuibiwa Sh. milioni 399.8.

Hata hivyo, alisema alipojaribu kuwasilina na uongozi wa benki, ulidai kuwa suala hilo wanalishughulikia na kumshauri asilifikishe suala hilo katika vyombo vya habari kwani haliwezi kupatiwa ufumbuzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alithibitisha kupata taarifa hizo. Alisema polisi ilianza kufanya uchunguzi baada ya uongozi wa benki hiyo kudai kuwa risiti zilizotumika kuweka fedha katika akaunti ya mteja huyo hawazitambui.

Kutokana na hali hiyo, jeshi hilo limewahoji wafanyakazi wa benki hiyo na kuwashirikilia watatu kwa tuhuma hizo huku uchunguzi zaidi ukiendelea na kwamba baada ya kukamilika jarada litapelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali ili kufunguliwa kwa mashtaka.

Meneja wa benki hiyo tawi la Morogoro, Angelo Mahembe, alipotafutwa na nipaswe kupata ufafanuzi hakukubali wala kukataa. Hata hivyo, alishauri watafutwe viongozi wa makao makuu kwa maelezo kuwa yeye siyo msemaji.
 
Yaani Nchi hii na Benki hizi kwakweli
zinafanana nadhani mpaka sasa hakuna
Benki salama Nchini isipokuwa sehemu moja
tu nayo ni:-

Pesa kuweka kwenye Kopo nyumbani kwako
Kuchimbia shamba kwenye Migomba tu
Kutembea nazo kwenye pindo la Suruali
Kuwa na Kibubu nyumbani kwako.


Kila Benki kwasasa ni wizi mtupu maana
unatafuta pesa kwa jasho sana halafu
unawapelekea watu wanakula kiulaini.
 
Kibubu ndio Sehemu salama zaidi halafu hakina Foleni wala shida ya mtandao na monthly charges
 
Vijana wamemaliza vyuo juzi tu lakini mtaani hatulali, wao kazi yao kuongeza tu mfumuko wa bei mtaani kwa kumwaga hela ovyo. Nenda Mbezi juu uone walivyoporomosha majumba kwa kipindi kifupi tu.

PCCB ipo lakini kazi yake wanaijua wenyewe. Huyo meneja wa tawi ni kuweka ndani tu. Barclays ndio Benki inayoongoza kwa kua na "Wapigaji" waliokubuhu.

Jamaa yangu mmoja alichukuaga mkopo kwao. Baada ya muda waliokubaliana kusitisha makato jamaa akaomba statement aone kama kweli balance inasoma ZERO. Jamaa alishangaa kukuta anadaiwa zaidi ya 5milion, kuchunguza kumbe benki walikua waki-divert baadhi ya makato yake!!
 
Sasa nafahamu sababu zilizompelekea bibi kupiga fundo hela kwenye kanga yake.
 
Weeh mrs R.B. Hii habari umeandika wewe originale ama? Mbona hata source unaiedit kati isijulikane? Whats up with you?!
 
Last edited by a moderator:
sasa watanzania tutakimbilia wapi vibaka mpaka kwenye mabenki!!!!ukisoma hiyo taarifa inaonyesha hata huyo meneja wa tawi anahusika ni kwa nini mteja anazungushwa kupewa statement mpaka aende polisi!!!!naona historia ijirudie pesa ficha kwenye vyungu!!!!
 
Back
Top Bottom