Mfano wa mpiga kura na mfuga mbwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfano wa mpiga kura na mfuga mbwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nsololi, Sep 15, 2010.

 1. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45

  Ukifuga mbwa akiuma watu njiani unashtakiwa wewe mfugaji.

  Sasa ukichagua viongozi wabovu, wezi na wasiojali umma wa watanzania kama inavyoonyesha, utakuwa umeshiriki moja kwa moja kuharibu nchi yako mwenyewe!


  Wakiiba hela dawa zikakosekana hospitali watoto wakafa, ni wewe mpiga kura umeua watoto hao. Elimu ikidumaa ni wewe ndio umeidumaza.

  Vifo vya kina mama vikiongezeka, wewe ndo umewaua wamama! Dawa zikikosekana hospitali wewe ndo unahusika.

  Na siku ya mwisho, damu za wezi hao (maana wewe ndo umewawezesha kuiba na
  ulijua ni wezi lakini ukawapa madaraka!) na za wote waliopotea kwa sababu yako zitakuwa mikononi mwako.

  Afadhali ungekuwa hujui kuwa ni wezi, ungesamehewa! Lakini tazama unajua kabisa mambo yote yanayoendelea na unataka kukosea tena kwa makusudi! Na utadaiwa mbele ya haki!

  Amua sasa kuitendea haki nchi na taifa lako uepuke hukumu!!
   
 2. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ukimrudisha mgonjwa magogoni akifia pale ww ndio wa kupata hukumu kwani ulijua kuwa ni mgonjwa......kwanini umemrudisha?
   
Loading...