Mfano wa Mkataba wa kupangisha

Karim Mussa

Member
May 6, 2019
21
5
MKATABA WA KUPANGA FREMU NAMBA……. BLOCK…………………………….
MANISPAA YA

  1. Mkataba huu umefanyika BAINA ya…………………………………………wa Sanduku la Posta……………………Morogoro ambaye katika mkataba huu ataitwa MWENYE NYUMBA kwa upande mmoja,


NA

  1. ……………………………………………………………….. WA Sanduku la Posta…………………… Morogoro ambaye katika mkataba huu ataitwa MPANGAJI kwa upande mwingine. Ambapo imekubaliwa na kushuhudiwa ifuatavyo:-


  1. Imekubaliwa na Mwenye nyumba na Mpangaji kwamba Mwenye nyumba atampangisha na Mpangaji atapanga Fremu ya biashara katika Nyumba Na……………..iliyoko……………….Mtaa wa……………………..Kata ya……………….…….Wilaya……………………….……Mkoa……………………….




  1. Muda wa Mkataba utakuwa ni………………………………………..ambapo pande zote mbili zikikubaliana Mkataba unaweza kufanywa mwingine baada ya huu kumalizika. Mkataba huu utaanza kutumika tarehe…………………………


  1. Kodi ya pango ni Tshs………………………………. Kwa mwezi na imekubalika kwamba kodi italipwa kwa…………………………………….na malipo yatafanyika……………………………………………………………………




  1. Mpangaji haruhusiwi kufanya mabadiliko yoyote katika Fremu, yawe ni matengenezo, marekebisho au nyongeza ya ujenzi pasipo kwanza kupata kibali cha Mwenye nyumba. Endapo utaonekana ulazima wa kufanya matengenezo au marekebisho au nyongeza yoyote basi MPANGAJI ataruhusiwa na Mwenye nyumba kufanya hivyo na gharama zote zitakuwa ni juu ya Mpangaji.


  1. Mpangaji atatakiwa wakati wote kuwa na mahusiano mazuri na Wapangaji wengine, majirani wanao zunguka nyumba anamopanga na watu wengine wanaofika mahali hapo au kutumia njia inayopita katika nyumba anayopanga na bila kufanya vitendo vya bugudha kwa wengine.


  1. Mpangaji atamruhusu Mwenye nyumba, Mwakilishi wake au mtu aliye katika familia yake kutembelea na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa Fremu kwa lengo la kufanyia ukarabati au matengenezo madogo madogo.






  1. Mwenye nyumba atakuwa na haki ya kufuta mkataba huu endapo Mpangaji atafanya matumizi mabaya na ya kinyume cha Sheria za Nchi, fremu ya biashara anayopanga kama vile kuhifadhi mali zinazokatazwa kisheria, madawa ya kulevya nk. Atapewa notisi ya miezi mitatu ya kufuta Mkataba huu. Mpangaji anahaki ya kuishi kwa raha na amani endapo atakuwa amekidhi mahitaji yote ya Mkataba huu.




  1. Mkataba huu utakwisha tarehe………………………………………. Hata hivyo pande zote zinaweza kuafikiana kuvunja Mkataba kabla ya tarehe ya mwisho iwapo upande mmoja utatoa notisi ya miezi mitatu kabla ukitoa sababu za kusitisha Mkataba huu.


  1. Mkataba huu umefanyika leo tarehe…………..........mwaka…………….






UMESAINIWA NA:-

Ndugu…………………. ……………………………

……………………………….. MWENYE NYUMBA





UMESAINIWA NA:


Ndugu…………………. ……………………………

…………………………….. MPANGAJI







UMESHUHUDIWA MBELE YA:-


Ndugu…………. ……………………………

……………………………….. SHAHIDI
 
Back
Top Bottom