Mfalme wa Mwisho wa Zanzibar Jamshid atua Oman kwa mara ya kwanza

Maalim anamuwakilisha huyu , akishinda tu anarudi
Wako wakimbizi ambao wana makosa kweli na hatimae hurudi makwao kwa maridhiano na ndugu zao na viongozi walio madarakani Huyu naye ambaye hakuna mwenye ushahidi wa uovu alioufanya angependa kurudi nadhani raisi yeyote asingemzuia lakini sidhani kama atapenda kurudi kwenye nch ambayo imejaa fitna na watu wenye chuki za kijinga kama wewe hivyo.
 
Ilikuwa ni historia tu alipofikia huyo Jamshid kwani ilikuwa watawala ni wazanzibari wenye asili tofauti.Haikuwa tatizo mpaka walipofitinishwa. Mtu mwenye asili ya Oman akitawala Zanzibar tatizo liko wapi.Mbona Tanzania imewahi kutawaliwa na maraisi wenye asili ya Kenya na Msumbiji.Marekani imetawaliwa na mtu mwenye asili ya Uiengereza.Si rahisi kuwatenganisha viumbe vya Mwenyezi Mungu kwa matakwa ya kibinadamu.
Kama kuna mtu anaona ubaya ni kutawaliwa na mtu mwenye asili ya Oman basi ana dalili ya chuki za kidini.

Huyo unaemjibu pia ni muslim, sioni ajabu wapo waislamu pia wanawachukia waarabu hata kama ni waislamu! Inashangaza sana hii kitu. Kutosoma dini na kuielewa ipasavyo madhara yake ndio haya.

Binafsi anaewachukia waarabu, tena ni ndugu zetu katika imani huwa namweka katika kundi la "waislamu jina" wapo wapo tu ilimradi.,,,na wengine wanachukiana kwa ajili ya madhehebu. Ni ujinga tu
 
Acha kabisa haya maisha,wakati mwingine yanachanganya sana
Yale yalikuwa mapinduzi bandia na ya kulazimisha kwa maslahi ya mabeberu na ili kuudhuru uislamu ambapo mabeberu waliwatumia viongozi wetu wakuu wa wakati huo kuyafanikisha kwa kuuwa watu wasio na hatia.Kuna viongozi wetu waliopita ambao hupewa majina makubwa lakini kumbe walikuwa vibaraka na mbumbumbu kweli kweli.
Kama wasingejenga chuki baina ya watu kwa kuwatungia visa na visasi mpaka kundi la watu fulani likaonekana kama si watu na si wananchi basi wala kusingekuwa na mapinduzi ya sura ile.Kungetokea ugomvi wa uroho wa madaraka lakini sio wa kuwachukia watu wenye asili ya uarabu ambao walikuwa wamechanganyika mno na watu wote.
 
Jamshid tangu mwaka 1964 ni kama kwamba ni mfungwa wa kifungo cha nje.Amekuwa hivyo miaka zaidi ya 50 nchini Uiengereza na sasa anaendelea na kifungo nchini Oman. Amepewa moja ya makasri ya wafalme na anaishi chini ya ulinzi mkali.Tulitamani tuende tukamuamkie na kumhoji pale nyumbani kwake ili tumsikie sauti yake na atupe maoni yake jinsi alivyoyaona mapinduzi.Lakini hakuingiliki na huenda akafikia mwisho wa maisha yake bila kupata kauli yake.
 
Yale yalikuwa mapinduzi bandia na ya kulazimisha kwa maslahi ya mabeberu na ili kuudhuru uislamu ambapo mabeberu waliwatumia viongozi wetu wakuu wa wakati huo kuyafanikisha kwa kuuwa watu wasio na hatia.Kuna viongozi wetu waliopita ambao hupewa majina makubwa lakini kumbe walikuwa vibaraka na mbumbumbu kweli kweli.
Kama wasingejenga chuki baina ya watu kwa kuwatungia visa na visasi mpaka kundi la watu fulani likaonekana kama si watu na si wananchi basi wala kusingekuwa na mapinduzi ya sura ile.Kungetokea ugomvi wa uroho wa madaraka lakini sio wa kuwachukia watu wenye asili ya uarabu ambao walikuwa wamechanganyika mno na watu wote.

Ingia google,"Zanzibar revolution wikipedia" utatokwa machozi sheikh, waomani/waislamu walivyouawa dhidi ya hao makafiri ambao wengiwao hatukonao tena, wanamme na wakina mama wameuawa kinyama, na wengine wajawazito 😥😥 very sad. Okello, Nyrr na Karume walidhani wataishi milele.
 
Inasikitisha sana.Pamoja na hiyo google soma kitabu cha Alghasaniy cha Kwaheri kwaheri.Mimi nakichukulia kuwa ni moja ya vitabu vikubwa vya historia kwani kimezungumza na wahusika wa mapinduzi moja kwa moja na waathirika sio wale wanaokaa mezani ni kuweka ndoto na chuki zao tu,Ukiondoa yote hayo mimi binafsi ni muathirika na nimeishi na wenzangu kila mmoja akisimulia mkasa wake tofauti kabisa na chuki za kisiasa na kikabila kwenye majukwaa. Nimeishi na waliobakwa na hawakuolewa wakafa kwa kihoro na wale walioshuhudia watu walioishi nao kwa ujirani mzuri lakini siku ile wakaletewa bunduki na wakazitumia kuuwa majirani nao ambao walikuwa wakitendeana mema na hawakuwa na ugomvi nao.Lakini hiyo ilikuja katika kampeni za chini chini za miaka kadhaa na zilizopata kasi karibu na siku ya mapinduzi kwa madai kuwa hawa ni mabeberu na wanawatuma bure.Wanasema nyinyi hivi na vile.Kumbe uongo mtupu. Ukitaka kujua angalia watoto waliozaliwa walikuwaje siku baada ya siku.
 
Shukurani kwa ufafanuzi mzuri sana , Allah akujaze kheri sheikh wangu,,,Inshaallah nitakipitia hicho kitabu, na waislamu wote nawaomba wapitie hicho kitabu wapate kujua yaliyomo, google sometimes wanaficha ukweli.
 
Kuna app maalum wenyewe google wameanzisha karibuni ya kuchuja habari zilizothibitishwa kwani hii ya sasa unakutana na mambo mengi ambayo yametungwa tu wala si ya kweli.Na kwa ujumla ni vigumu sana kudhibiti japo huenda huko mbeleni ikasaidia.
Hivyo kwa mfano hicho kitabu ni bora kuliko vitabu vya Kivukoni au kile alichoandika aliyekuwa waziru wa elimu Omar Mapuri ambacho wazanzibari wa kila upande walichukizwa na uwongo wake na chumvi kutoka moyoni mwake na wakaamua kukichoma moto hadharani.
 
Ilikuwa ni historia tu alipofikia huyo Jamshid kwani ilikuwa watawala ni wazanzibari wenye asili tofauti.Haikuwa tatizo mpaka walipofitinishwa. Mtu mwenye asili ya Oman akitawala Zanzibar tatizo liko wapi.Mbona Tanzania imewahi kutawaliwa na maraisi wenye asili ya Kenya na Msumbiji.Marekani imetawaliwa na mtu mwenye asili ya Uiengereza.Si rahisi kuwatenganisha viumbe vya Mwenyezi Mungu kwa matakwa ya kibinadamu.
Kama kuna mtu anaona ubaya ni kutawaliwa na mtu mwenye asili ya Oman basi ana dalili ya chuki za kidini.
wewe wenye asili ya Kibantu mbona hujawahi kutawala Oman?
 
Wenye asili ya kibantu wanakuwaje kwa uoni wako.Na jee unajuwa historia kweli ya watawala wote wa Oman.
Na iwapo mfano hujamuona huyo unayemtaka atawale Oman,hii ligi unayotaka ina sababu gani na jee umefikia muda wa kuhoji hivyo kwa Oman.
Baada ya hapo nikujibu kuwa wapo wengi tu wenye asili ya Tanzania na Zanzibar ambao wanatawala Oman.Kumbuka ile meli iliyokuja Tanzania kama miaka 3 iliyopita iliongozwa na mawaziri wakubwa wa Oman ambao wametokea Tanzania na huko Tanzania wana ndugu wa kila rangi na makabila.
 
Nimeuliza Mbantu ama Mmanyema anayetawala Oman!
 
Back
Top Bottom