Mfalme wa Jordan akataa kukutana na Netanyahu na hata kuzungumza naye kwa simu

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Mfalme wa Jordan akataa kukutana na Netanyahu na hata kuzungumza naye kwa simu
Aug 04, 2019 08:12 UTC
Mfalme Abdallah II wa Jordan amekataa ombi la Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel la kukutana naye na hata kufanya naye mazungumzo kwa njia ya simu.
Gazeti la al-Quds al-Arabi linaripoti kwamba, Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel aliwasilisha ombi la kukutana la Mfalme wa Pili wa Jordan au hata kuzungumza naye kwa simu, ombi ambalo limekataliwa na Mfalme wa Jordan.
Gazeti la al-Quds al-Arabi limetangaza habari hiyo huku Jared Kushner, Mshauri Mkuu wa Rais wa Marekani Donald Trump Jumatano iliyopita alianza safari ya kiduru ya kuzitembelea nchi kadhaa za Mashariki ya Kati kwa shabaha ya kuupigia debe mpango wa Marekani wa 'Muamala wa Karne'.
Baadhi ya duru zinasema kuwa, katika safari yake nchini Jordan Kushner hakupokewa vizuri na kwa uchangamfu licha ya kwamba, alifanikiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Mflalme Abdallah II wa Jordan.
Katika mazungumzo yake na Jared Kushner, Mfalme wa Jordan alimweleza kinaga ubaga mshauri huyo wa Rais Donald Trump wa Marekani udharura wa kupatikana amani ya kiadilifu na kuundwa dola huru la Palestina mji mkuu wake ukiwa Baytul-Muqaddas.
Hii ni katika hali ambayo, kwa mujibu wa mpango wa Marekani wa 'Muamala wa Karne' suala la kuunda nchi huru ya Palestina litatupiliwa mbali na mamilioni ya wakimbizi wa Kipalestina wataainishiwa makazi mengine badala ya kuruhusiwa kurejea katika ardhi za mababu zao.
Tags
ISRAEL NETANYAHU


My take:Waarab hawaaminiki hata kidogo
 
Huyo mflame ndio zake kudengua hadi abembelezwe ndio hukubali sijui ana gene za jinsia gani
 
Back
Top Bottom