Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
LEO NAKUTUKANA.
Siandi na ashakumu, leo ninakutukana,
Nikutukane dhalimu, katiba unayechana,
Kwa hii yangu kalamu, yeo mengi nitanena,
Tangu ushike hatamu, na sheria wakinzana,
Kiti unakidhulumu, hishima tena hakina,
Nauliza nifahamu, nipa jawabu la kina,
Mfalme waenda wapi?
Mawaziri 'meteua, na watu kwa kila ngazi,
Uchao wawasumbua, mithili ya vijakazi,
Kazi zao wattukua, kama wao hawawezi,
Mpishi na mpakua, watamani uandazi,
Kulla kitu muamua, zakosa ma'na teuzi,
Si kwamba nakuumbua, ila nipe fafanuzi,
Mfalme waenda wapi?
Juhudi zako adhimu, nakiri ninaziona,
Za kurejesha nidhamu, uchumi upate fana,
Watu wawe wakarimu, na kukome kunyonyana,
Ubaya wazidhulumu, kwa kufanya yasoma'na,
Hasa kuto jiheshimu, na kupenda kutishana,
Kuuliza yalazimu, nijibu pasi hiyana,
Mfalme waenda wapi?
Majipu wayatumbua, kwalo pokea pongezi,
Tatizo wasuasua, kumtumbua kipenzi,
Kwake kanwa wakenua, japo afanya uchizi,
Pia wacha kubagua, na kufanya maonezi,
Sheria unazijua, zifate bila jelezi,
Leo basi fafanua, umma utuweke wazi,
Mfalme waenda wapi?
Tetesi una sehemu, mateka wamejazana,
Ndiyo yao jahanamu, ya wasemao bayana,
Adhabu pasi hukumu, sheria wazisigina,
Mijeledi hadi damu, na makende kuwabana,
Wapo walopawa sumu, kwao hawarudi tena,
Mtesi mwenye wazimu, hebu nijibu kijana,
Mfalme waenda wapi?
Hapa mwisho ninatua, beti sita siongezi,
Mikono ninainua, kwa ina lake Azizi,
Naiomba hino dua, umguse kiongozi,
Uchunge zake hatua, mkinge na utelezi,
Mdomo akiinua, asiambe upuuzi,
Rabbi nataka kujua, hili lanipa tatizi,
Mfalme aenda wapi?
...T...A...M...A...T...I....
PICHA: Haihusiani na shairi hili au sababu za kutungwa kwake ila nampenda tu rais wangu na kwakuwa nina kapicha chake nikaona nikapost, nawe kama wampenda na una kapicha chake, basi post! Share kwa wingi ili na wenzako wasome!
27 Aprili 2017 Alhamisi 11:19
NjanoTano
Dotto Rangimoto Chamchua.
Whatspp/call 0622845394 Morogoro.