Mfalme mzuri hapuuzi taarifa juu ya utawala wake

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,457
12,682
Nikianza kabisa kwa kutangaza interest kuwa binafsi ni mwanachama wa CCM.

Mh. Rais wangu JPM, Wahenga waliposema "lisemwalo lipo kama halipo laja" hawakuwa wamekosa hekima. Kelele za kila kona na mbiu ya watanzania juu ya adui njaa hazipaswi kupuuzwa na kuchuliwa kama chuki kiurahisi hivyo. Ebu tumia hekima ya uongozi na upime dhamana yako kwa kila raia wa nchi hii utafute njia ya kijiridhisha na hili.

Mwalimu Nyerere alipoambiwa serikali yake ya UKATOLIKI alijua fika hajawahi kufikiria kufanya kitu hicho ila badae aliamua kujiridhisha kwa kuchunguz akidhani wenda alifanya hivyo bila kujua katika kuunda baraza la mawaziri maana kwake dini haikuwa msingi katika kuunda serikali.

Ukisoma misaafu hasa biblia maana wewe ni mkiristo matukio ya njaa ni rais kuyatabiri maana yanakiashiria kikuu UKAME kama takwimu zinaonesha dhahiri maeneo mengi ya nchi yanaukosefu mkubwa wa mvua na mazao yamekufa unategemea SHIBE AU NJAA badae??

Binafsi napenda unavyojitolea kwa ajili ya watanzania ila naamini matatizo ya kila mtanzania huwezi kuyajua bila kuambiwa, sasa wanaosema ni WATANZANI wanaonya na wengine kudai kuna njaa itakugharimu nini kukubali na ukajiridhisha kama kuna njaa kwanini serikali ingie ktk vita ya maneno na kamatakamata kuhusu suala hili??

Mwanafalsafa SOCRATE anasema ni vigumu kutoa maelezo juu ya mnyama PUNDA km PUNDA mwenyewe hajawahi kuwepo kinadharia au katika mawazo ya watu lazima picha na taswira ya punda ipo ndiyo maana kukawepo na jina Punda. Sasa hili la njaa hliwezi kutokuwepo afu watanzania watunge from nowhere nakusema kuna NJAA.

Nimalize kwa kuweka angalizo jana, mh. Waziri wa kilimo mr. C.Kizeba alitoa takwimu ila kiuchambuzi ni takwimu zisizo halisika huwezi kutoa takwimu za tani za vyakula huku kujibu hoja ya njaa huku ukijua watanzania hatuli kwa kupata chakula kwenye maghala ya serikali. Pia mjue maghala yapo ili kusaidia muda wa majanga ya njaa inapotokea sasa iweje hoja ya chakula ghalani ijibu hoja ya ukame mkali na useme hakuna njaa.
Kinachotabiriwa na watu wengi na hali ya ukame iliyopitiliza ambayo bila shaka njaa ni matokeo yake ya badae sasa kukataa hakuna njaa hakusaidii kuondoa ukweli.

NIMALIZIE HIVI: "Farao alivyoshupaza shingo mwisho wake lilivunjika"
Mh.Rais na serikali Yako/Yetu maana inatuhudumia ebu legeza shingo, nimesema haya maneno kwa kusukumwa na uzalendo kama kijana na mwanaccm na Mtanzania niliyejaa moyo wa uzalendo ninayetembea mwendo wa kitanzania na kujivunia ujasiri wa kusema ukweli.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu..!
 
Mzee hongera sana kwa uzi mzuri. Laiti kama wanaCCM wote linapokuja suala la maslahi ya taifa wangekuwa wanaweka uchama kando basi tungekuwa mbali sana, maana yake mwisho wa siku ni kwa manufaa ya wananchi.
Muheshimiwa raisi tunaomba sikia kilio cha wa watu wako kwa maana penye moshi hapakosi kuwa na moto na pia penye ukame hapatakosa njaa! Kwa sasa nchi yetu ipo kwenye ukame wa hali ya kutisha. Hii hali kwa asilimia kubwa baadae matokeo yake itakuwa ni njaa.
Eeeeh Mola tupitishie mbali janga hili.
 
Maraisi wa awamu nne zilizopita kukitokea tetesi, dalili, viashiria vya njaa kama ukame ama madai ya kuwepo njaa response yao ilikuwa, "TUNAWAKIKISHIA WANANCHI WOTE KUWA HAKUNA ATAKAYEKUFA KWA NJAA!" Walikuwa hafanyi tetesi hizo kuwa tangazo la vita ya kisiasa. Nyerere aliwahi kusema kuwa ikibidi hata kuongea na makaburu kuwa walete chakula kama janga la njaa limetokea, 'tutafanya'. Hii ilikuwa serious sana kwa kuwa kulingana na Nyerere Makaburu walikuwa maadui wakuu wa utu wa binadamu. Lakini kwa njaa, hamna budi ikibidi! Shida ya serikali yetu ya awamu ya tano ni zile kauli tata kama " serikali haina shamba!" ama " serikali haikuleta janga hili!" ama " katu serikali yangu haitawaletea chakula!" Ninaposoma magazeti ya leo wakisema kuwa eti wataanza kusambaza chakula, najiuliza kuwa ni serikali ileile au ni nyingine? Kuna hekima fulani inakosekana katika utawala huu wa serikali ya awamu ya tano!! Hawapimi kabla ya kusema wala hawachuji chakusema. Wanasema kile kinachowajilia tu. Nadhani kuna haja ya kuandikiwa hotuba na mhutubiaji awe anasoma!!!!!
 
Haya mambo sometime yanaweza kukuumiza kichwa kumbe ni politics tu ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom