Mfalme amekaa vibaya, wananchi wanamchungulia lakini wanaogopa kumwambia

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,455
29,134
Hii ni hadithi flani ya zamani nadhani nilihadithiwa mimi tu. Inamhusu mfalme mmoja alikuwa mbabe na katili na alikua hapendi kuambiwa ambalo halijui wala hataki kuambiwa. Wanachi wa mji ule wakiogopa sana maana alizuia habari yoyote mbaya kuhusu yeye na wazee wake wa baraza, kwa namna alivyokuwa akiendesha huo mji hata watu walipoona maovu waliogopa kusema maana mfalme angekushughulikia ipasavyo.

Wananchi wakawa wanaona poa maana shida pia hua inazoezwa, ikawa mfalme akivaa mavazi yake vitu vyote vipo nje basi wananchi wanaitana na kuoneshana na kucheka sana, mfalme akiona hivyo anajua wanacheka kwa kuwa amependeza. Ikaendelea mpaka baadhi ya watu wakatamani kumwambia mfalme kuwa vitu vipo nje lakini kabla hawajaongea mfalme ashashughulika nao, wakaona isiwe tabu ngoja nao wajiunge kumcheka.

Ni hadithi tu nimeikumbuka
 
ha ha ha ha ha aha aha aha aha aha ah.....................this post has made my day! nimecheka hadi machozi! Ni ukweli mtupu mfalme wetu yuko uchi ila nani wa kumwambia ????? nani hajitaki unadhani!
 
Siku moja aliwaambia wafanyakazi wake wamshonee nguo isiyoonekana hata akivaa.....ah ah ah ah ni tamu sana hyooo
 
Sawa,
Ila kwenye sherehe za mwaka 2020, ataambiwa kuwa alikaa uchi kias gan kwa miaka mitano, na sijui atamlaum nan maana hakutaka kuambiwa wala kunyooshewa kidole....!!

Hapo ndo hadithi itanoga zaid
 
Hadithi safi kabisa.

Kama unayo na ile ya abduli na kivazi cha mfalme iweke hapa mkuu.
 
Anakuja. Isije kuwa hii story inafanana maudhui na ile ya mwenyekiti wa kamati ya harusi!
Mkuu mbona kama kuna tofauti kati ya story na hadithi, au hujui ile ya kaondokea chanjagaa, kajenga nyumba kakaa, mwanangu mwanasiti vijino kama chikichi vya kujengea ukuta mwasikia sana.
Cc Pasco
 
Adithi hiyo bado haijaisha, nakumbuka inaendelea kwamba siku moja mfalme alikuwa kwenye alaiki ya sherehe fulani. Mtoto moja alipokwenda jukwaani kumpa zawadi mfalme alimnong'oneza mfalme kwamba watu wanacheka kwasababu vazi lake linaonyesha sehemu za siri. Mfalme akamfanya yule mtoto kuwa msaidizi na bodyguard wake na papo hapo akawatumbua viongozi na wasaidizi wake waliokuwa wanafiki nakumcheka huku akidhalilika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom