Mfalme aliyepinduliwa Z,bar (Jemshid)alikuwa ni mzaliwa wa Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfalme aliyepinduliwa Z,bar (Jemshid)alikuwa ni mzaliwa wa Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Dec 10, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Ujamaa uliziunganisha Tanganyika na Zanzibar

  Fidelis Butahe

  JAMHURI ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa rais wa Tanganyika, Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa rais wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar.

  Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi, Aprili 26 hadi 27, 1964.

  Jina la "Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar" lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa

  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria namba 61 ya mwaka 1964 ya Jamhuri ya Muungano.

  Ilivyokuwa

  Vyanzo mbalimbali vya habari vinaeleza kuwa Watanganyika kama ilivyokuwa kwa wananchi wa nchi nyingine za kiafrika, hawakukubaliana na utawala wa kikoloni.

  Tangu mwanzo waliwapinga huku upinzani mkubwa ukionyeshwa na kabila la Wasambaa wakiongozwa na Kimweri dhidi ya Wajerumani.

  Wahehe wakiongozwa na Mkwawa kupigana dhidi ya Wajerumani na wakati wa vita vya Maji Maji chini ya uongozi wa Kinjekitile, Mputa na Kibasila.

  Kukosekana kwa umoja kati ya wapigania uhuru wa mwanzo na uimara wa majeshi ya wakoloni yaliyokuwa na silaha bora za moto, kulidhoofisha mapambano ya uhuru na kusababisha hasara kubwa na kupoteza maisha ya watu.

  Kama ilivyokuwa kwenye makoloni mengi ya kiafrika, hisia za utaifa ziliendelea kuimarika katika Tanganyika baada ya mwaka 1945.

  Alama za utaifa zilianza kuonekana mara baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia, kwa kuanzishwa kwa vyama mbalimbali vya Waafrika kwa upande wa Tanganyika na Zanzibar.

  Kwa upande wa Tanganyika, African Association kilianzishwa mwaka 1929 kama kikundi cha mijadala baina ya wasomi na ilipofika mwaka 1948 chama hiki kikawa Tanganyika African Association (TAA).

  Baada ya vita ya pili ya Dunia, wanachama wa Tanganyika African Association (TAA) waliendeleza wimbi la utaifa.

  Mwaka 1953 chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere, TAA ilitambuliwa kama chama cha siasa na kuelekea moja kwa moja kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954, chama kilichotumika kama chombo cha kisiasa cha watu katika kutoa vilio vyao vya kudai uhuru.

  Kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954, ulikuwa ndio mwanzo wa mbio za kupigania uhuru.

  Baada ya miaka saba ya mapambano ya kisiasa, Tanganyika ilikuwa huru chini ya chama cha TANU, kilichoimarishwa na vyama vya wafanyakazi na vya ushirika.

  Kwa upande wa Zanzibar
  Kwa upande wa Zanzibar, chimbuko la Jumuiya ya Waafrika ilikuwa ni vilabu vya mpira wa miguu vilivyoanzishwa mwanzoni mwa miaka
  ya 1930.

  Ilipofika mwaka 1934, Jumuiya ya Waafrika ilianzishwa rasmi na kupewa jina la African Association (AA).

  Baada ya vita ya pili ya dunia kama ilivyokuwa katika sehemu nyingine za dunia, kulikumbwa na uhaba mkubwa wa chakula, ubaguzi na mgawanyiko baina ya jamii.

  Kutokana na matatizo hayo ya ubaguzi, kulianzishwa Jumuiya ya Washirazi (Shirazi Association) kwenye visiwa vya Unguja na Pemba, lengo likiwa ni kudai kupatiwa haki mbalimbali za kijamii na kulinda utambulisho wao.

  Kuundwa kwa chama cha ZNP (Zanzibar Nationalist Party) mwaka 1957, kulifanya viongozi wa Jumuiya ya Waafrika (African Association) na wale wa Shirazi Association waone umuhimu wa kushirikiana.

  Waligundua kuwa Serikali ya kikoloni na chama cha ZNP walishirikiana kuendeleza dhuluma dhidi ya Waafrika.

  Viongozi hao waliona ulazima wa kuungana kuwa kitu kimoja kupigania uhuru.

  Katika kutekeleza azma hiyo, viongozi wa Jumuiya hizo walikutana na kukubaliana kuunganisha Shirazi Association na African Association mwaka 1957.

  Muunganiko huo ulisababisha kuundwa kwa chama cha Afro- Shirazi Union ambacho baadae kiliitwa Chama cha Afro-Shirazi chini ya uongozi wa Sheikh Abeid Amani Karume.

  Vuguvugu la kisiasa
  Kati ya mwaka 1957, mara baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza na mwishoni mwa mwaka 1963, kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964, Zanzibar ilitawaliwa na vuguvugu na mivutano mikali ya kisiasa.

  Mapambano haya ya kisiasa yalikuwa kati ya Chama cha Afro-Shirazi kilichoungwa mkono na Waafrika na kile cha ZNP kilichoungwa mkono na Wakoloni, Sultani pamoja na jamii ya Waarabu.

  Chama cha ZNP baada ya kushindwa uchaguzi, kilianzisha kampeni za kushawishi wenye mashamba na mabepari wengine waliokuwa wakimiliki njia kuu za uchumi kuwafukuza kazi au kutowaajiri wafuasi wa ASP.

  Chama cha ZNP kiliwatafutia kazi na kuwabakisha mashambani waafrika wote waliokubali kukiunga mkono.

  Wakati wa mvutano huo wa kisiasa kati ya ASP na ZNP ukipamba moto, kulijitokeza tofauti miongoni mwa viongozi wa ASP.

  Tofauti hizo zilichangiwa na uroho wa madaraka, ubinafsi na kutokuwa na msimamo imara miongoni mwa baadhi ya viongozi wa chama hicho.

  Pia, Serikali ya Sultani nayo ilichochea migogoro hiyo ili ijinufaishe kisiasa.

  Migogoro hiyo ilisababisha kujitoa kwa baadhi ya viongozi wa ASP ambao walifanya mkutano na baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa ASP huko Pemba, Novemba 1959 na walikubaliana kuanzisha Chama kipya cha siasa cha Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP).

  Wakati vyama vya ASP, ZNP na ZPPP vikiwa katika malumbano makali ya kisiasa, serikali ya Kikoloni ilifanya matayarisho ya uchaguzi wa pili.

  Uchaguzi ulifanyika Januari 16, 1961 ambapo siku moja kabla ya uchaguzi huo, serikali ilitangaza kuwa chama kitakachoshinda kitaunda serikali na wizara zote zitakuwa chini yake.

  Katika uchaguzi huo ASP ilishinda kwa kupata viti 10, ZNP kilipata viti 9 na chama cha ZPPP kilipata viti 3.

  Kutokana na kuenea kwa chuki za kisiasa miongoni mwa Wazanzibari, Vyama vikuu vya kisiasa vilifikia muafaka wa kumaliza hali hiyo.

  Hatahivyo, ASP haikufikisha zaidi ya nusu ya kura na hivyo haikuweza kuunda serikali.

  Njia pekee iliyobakia ilikuwa ni kuishauri ZPPP ichanganye viti vyake na chama kimoja kati ya ASP na ZNP.

  ZPPP na ZNP viliungana na iliamuliwa kuwa iundwe serikali ya muda na kusubiri uchaguzi mwingine uliopangwa kufanyika Juni, 1961. Waingereza walitoa uhuru kwa Serikali ya Mseto ya ZNP/ZPPP ya waziri mkuu, Muhammed Shamte.

  Chini ya ushauri wa Waingereza, Shamte aliwatenga ndani ya Serikali yake baadhi ya viongozi wa ZNP wenye msimamo wa Kikomunisti wakiongozwa na Abdulrahaman Babu, na hivyo kutokea kutofautiana kwa baadhi ya viongozi wa ZNP na Serikali ya ZNP/ZPPP.

  Baada ya kutengwa na Serikali hiyo, ZNP walijitoa na kuanzisha chama cha umma. Chama hicho kilivunjwa mara tu baada ya mapinduzi ya mwaka 1964 huku viongozi na wafuasi wake wakijiunga na Serikali ya ASP chini ya uongozi wa Abeid Karume.

  Zanzibar ilikuwa na wakati mgumu katika kupigania uhuru, Waingereza walijikita zaidi kwa madhumuni ya kibiashara na kwa nia ya kukomesha biashara ya utumwa, walifanya hivyo kwa sababu walitaka nguvukazi rahisi ambayo ilikuwa inapotea.

  Waingereza walifikia makubaliano na Sultani mwaka 1822 ili kukomesha biashara ya utumwa, lakini ilichukua zaidi ya miaka 50 hadi utumwa kutokomezwa.

  Makubaliano ya Waingereza na Wajerumani ya mwaka 1890 yalifanya Zanzibar kuwa koloni la waingereza ambao walimshirikisha Sultani katika utawala wao.

  Waingereza waliainzisha ubaguzi wa rangi Zanzibar kwa wazungu na waarabu kupendelewa kuwa tabaka la juu na Waafrika la chini. Waingereza walifanya Zanzibar kuwa ni koloni la Waarabu na ilipofika Desemba 1963, Sultani alipewa mamlaka kamili ya kutawala Zanzibar.

  Januari 12, 1964, aliyekuwa Sultani wa Zanzibar, Jamshid bin Abdulla, aling'olewa madarakani katika mapinduzi yaliyokuwa yameandaliwa kwa usiri, ustadi na ujasiri mkubwa wa wanamapinduzi wa ASP na Jamhuri ikatangazwa.

  Muungano
  Muundo wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa nchi ya Tanzania kama ulivyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, una vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji ambavyo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Pia ina vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ambavyo ni Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Pia kuna vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma ambavyo ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, na yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara na serikali ya mapinduzi ya zanzibar inayoshughulikia mambo yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanzania Zanzibar.

  Muungano wa Tanzania ni tukio la nadharia iliyotafsiriwa katika vitendo, kwani kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ni hatua ya watu walio wakweli.

  Ni ushahidi unaojitosheleza kuwa wananchi wa Tanganyika na Zanzibar wakiongozwa na viongozi wao wa mapambano ya kudai uhuru, walitoa kauli zilizokuwa zikimaanisha walichofikiri na kuazimia na sio kwa sababu ya kusombwa na jazba za kisiasa.

  Sababu za Muungano
  Sababu za muungano huo ni pamoja na kuwepo kwa mahusiano ya karibu ya kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa ya TANU na ASP.

  Moyo wa kuwa na muungano wa Afrika kwa kuanzia na Shirikisho la Afrika Mashariki ulianza hata kabla ya uhuru wa Tanganyika. Mwalimu Nyerere pamoja na viongozi wengine waliokuwa wakipigania utaifa katika ukanda wa Afrika Mashariki walikuwa na matarajio ya kuwa na Muungano wa Afrika.

  Mwalimu Nyerere alipenda kuwepo muungano wa Afrika kwa kuanzia na mashirikisho ya kikanda. Baada ya kushauriana na viongozi mbalimbali wa iliyokuwa Jumuiya ya Wapigania Uhuru wa Afrika Mashariki na Kati (Pan- African Freedom Movement for East and Central Africa – PAFMECA) Mwalimu Nyerere alitoa tamko wakati wa mkutano wa nchi huru za Afrika uliofanyika Addis Ababa mwaka 1960.

  Katika mkutano huo Nyerere alizungumza mambo mengi na baadhi yalinukuliwa katika gazeti la Tanganyika Standard, Novemba 1964).

  Alisema, "Wengi wetu tunakubaliana bila kikwazo kwamba Shirikisho la Afrika Mashariki litakuwa ni jambo zuri. Tumesema na ni kweli kwamba mipaka inayotenganisha nchi zetu imewekwa na mabeberu na sio sisi wenyewe na kwamba tusikubali itumike dhidi ya umoja wetu…lazima tuzisumbue ofisi za wakoloni kwa nia si ya kudai uhuru wa Tanganyika, kisha Kenya, na Uganda halafu Zanzibar lakini kwa nia ya kutaka uhuru wa Afrika Mashariki kama Muungano mmoja wa Kisiasa".

  Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari, 1964 yalifanyika wakati Mwalimu Nyerere akiwa ameshachoshwa na kukatishwa tamaa na mazungumzo ya Shirikisho la Afrika Mashariki.

  Mapinduzi hayo yaliiweka madarakani serikali ya chama cha ASP kilichokuwa na mahusiano ya karibu na TANU kwa upande wa Tanganyika, mwaka 1977, TANU iliungana na ASP na kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Kutoka Mwananchi newspaper
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Dec 10, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,969
  Trophy Points: 280
  ..Sultani wa kwanza wa Zanzibar alikuwa "mwekezaji" ktk biashara ya watumwa.

  ..sasa nuksi yote ilianzia huko na kuleta ubaguzi, ubwana na utwana, ktk kila nyanja za maisha Zanzibar ikiwemo siasa.

  ..haijalishi kama Sultani alikuwa amezaliwa Zanzibar.
   
 3. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Kuwa Mzanzibar kwanza halafu ndio ujadili mambo ya Zanzibar, utumwa ilikuwa ni mbiashara ya wazungu kipindi hisho ikiwa warabu waliuza basi wazungu walinunua.

  Hivi sasa kinachozungumzwa Zanzibar ni Uzanzibar kwanza halafu jinsigani gani ya kujizongomowa na Mkoloni mweusi Tanganyika.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Dec 10, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,969
  Trophy Points: 280
  Kakke,

  ..wazungu pia walikuwa wanauza watumwa ktk maeneo ya Msumbiji na Angola.

  ..nilipotaja Waarabu "wawekezaji" ktk biashara ya utumwa sikuwa na maana kwamba wazungu hawahusiki.

  ..tena unaweza kuzama zaidi kwa kubainisha kwamba wapo Waafrika waliokuwa wakishiriki ktk unyama wa kukamata wenzao na kuwauza utumwani.

  ..sasa kilichomleta SULTANI wa kwanza wa Kiarabu ktk ardhi ya waafrika hapo Zanzibar na pwani ya Afrika Mashariki ni hiyo biashara ya WATUMWA.

  ..suala la kuzaliwa hapo Zanzibar siyo la msingi sana. Hata MAKABURU wa Afrika kusini, na WALOWEZI wa Zimbabwe nao walikuwa na hoja hizohizo kuwa wamezaliwa Afrika.

  ..kama nilivyokueleza matatizo ya Zanzibar asili yake ni Sultani aliyetoka Oman na kuja kujisimika kuwa mtawala wa Waafrika na ku-promote biashara ya utumwa, na ubaguzi wa rangi, na masuala ya ubwana na utwana.
   
 5. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Wakuu mnaongea msichokijua. Ubwana na Utwana haukuwepo ZNZ. Mmelishwa historia mbovu.
   
 6. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu punguza misokoto bange siyo sigara nzuri
   
 7. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kitu mbaya walichokifanya warabu ni kuhasi watumwa weusi na kutobaki kizazi cha watu weusi uarabuni kinyume na wazungu walivyowaacha waafrika weusi waendelee kuzaana kama Brazil, marekani, visiwa vya carebian na visiwa vya pacific. si kweli kuwa warabu walikuwa wanauza tu bila wao kubakia na watumwa. Na ile ya mke wa mwarabu kutaka kuona mtoto anavyokaa tumboni na mwanamke mweusi mjamzito kutumbuliwa kumridhisha mke wa mwarabu. Suala la sultani kuwa mzawa wa Zanzibar na hivyo aendeleze usultani zanzibar halina substance. machifu bara walikuwa wazawa haswa na sio wazawa walowezi kama sultani walipigwa stop mbona. waswahili hawakuwa na shida na Jemshid - walikuwa na taabu na usultani.
   
Loading...