Mfalme akasema atafutiwe vijana wenye akili na Maarifa

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Taifa la Israel tunalo liona leo sio taifa lililo zungukwa na vilaza. Nitaifa lenye majitu yenye akili nyingi tena sio watu wa mchezo mchezo. Nawao nitaifa kwanza sio mtu. Waziri Mkuu wa Sasa Benjamin Netanyahu ni mmoja wa viongoz wenye high IQ. Sio yeye tu ila na kizazi chao na wote ni zao la Mossad.

Nikatika taifa hili wakati fulani walipita katika kipindi kugumu na ndipo Mfalme wa wakati ule akaagiza watafutwe vijana wenye akili na maarifa ktk kila eneo kwa jili yakumshauri.

Historia inatuambia nikaktika hili kundi paliibuka most genius men on Earth Daniel. Alikuwa na akili nyingi na alinusa kutoka mbali.

Labda niwaambie msije mkafikiri wanao oma mambo yatatokea miaka mia ijayo ni manabii ktk jina ila kuna watu wanauwezo kufanya kazi yakusema kesho kinatokea nini!
Kuna watu wanauwezo kumnusa mtu nakumjuwa wapi yupo kwa maelezo au uwezo wa akili.

Hii ni bidhaa adimu sana watu wenye akili na uwezo ktk mambo yakiusalama na kila kitu. Nahapa ndipo Israel wanaipa tabu dunia na mpaka sasa hakuna.

Taifa lolote dunian nguvu yake ipo ktk usalama wa taifa imara na ktk usalamawa taifa imara unaitajikuwa na vichwa vyenye akili zaid yako hivyo nilazima ufanye kaz nao nakuwasikiliza sana.

Dakika chache baada yakudunguliwa ndege iso kuwa na rubani Marekani walitaka kulipiza kisasi kwa kishindo dhidi ya Iran. Ila huwez kuamini baada yakutoka kwenye kikao cha siri mweny nchi aliahirisha. Hiyo ndio nguvu ya CIA. Moja ya agency za usalama yenye nguvu duniani.

Kuna gharama kubwa pale taifa linakosa aina hii ya watu na ndio kisa cha shule za vipaji maalumu ambazo kuna waziri fulani aliziharibu pasipojuwa anatumaliza.

Nguvu ya familia na aina yeyote ya kampuni nikuwa na watu wenye akili nibahati mbaya unawezakuwa na watu wenye first class ila ukimsikiliza pass ndio fist class.

Nitaendelea...
 
Vipi kama usalama wa nchi husika unaendeshwa kwa itikadi ya chama kinachotawala? Hizo nchi unazozizungumzia hazifanyi uamuzi wa kitu katika mtazamo wa kiasiasa bali huenda mbali zaidi kufanya maamuzi kwa kuangalia athari za kiuchumi, kijamii etc pia hizo ni taasisi imara tofauti na nchi za kiafrika wao hutoa uamuzi kwa kumuogopa mtu au mtu anaogopa kufukuzwa kazi
 
Sisi tumempata Yusuph au Joseph kwa kimalkia anafanya njia pasipo njia na yuko poa zaidi ya wale

Nchi imenyooka kila jambo linakwenda ,jpm mungu ampe maisha marefu


State agent
 
Kabla hata hujaendelea. Mtu mwenye karama.ya kuona mambo.yatakayotukia miaka hata 50 ijayo huyo nabii. Iwe ni mcha MUNGU ama si mcha MUNGU.

Akiwa mcha MUNGU ataitwa mtu wa MUNGU na akiwa si mcha MUNGU basi ataitwa mwenye pepo la utambuzi
 
nchi zetu ni masikini kwakua hata hatujui kwanini tunakuwa masikini, kila mtu anakuja na fantacy zake, mara usalama mara raisi n.k lakini ni ujinga mtupu.

huwezi kutatua tatizo ambalo haulielewi vizuri, utaishia kubahatisha bahatisha tu.
 
Pengo lakina Nape Mwigulu January sasa linaonekana wazi na Ph D ya Mbowe inaenda kudhihirika sasa kweli Mungu ni Mwema tuyaona mengi
 
Kuna mstari hapo umeandika kitu cha muhimu, akili na maarifa aliyotupa Mungu tukitumia vizuri tunaweza kuproject future ya taifa letu na watu wake..

Dunia ya sasa mataifa yote yamewekeza kwenye vichwa vya watu kwa maendeleo ya Taifa na watu husika.. Bahati mbaya sana pande hizi inaogopwa sana kuwekeza kwenye vichwa vya watu maana ni hii inahatarisha uwepo wa watu fulani na vyama vyao..
 
Lazima kwanza wote pasipo ushabiki wa vyama tujue hasa tatizo halisi la nchi yetu, baada ya hapo tukubaliane njia sahihi ya kulitatua na lisiwepo au lisitokee tena..
 
Mfalme yupi huyo?,israel haijapata kuwa na mfalme mwenye akili wote walikuwa hopeless kwelikweli,
kidogo mfalme Josia alijitahidi na mfalme Omary,
wengine ni hopeless hakuna kitu walifanya zaidi ya kuwa vibaraka wa mataifa makubwa kama misri,babel,greece na Asyria
 
Ameongea mambo ya msingi sana ingawaje huwa nakuwa muangalifu sana ninapotaka kujadili issues za ktu kinachoitwa usalama wa taifa kutokana na mada inayoletwa na mtu kama TumainiEl !!

Kwa mataifa aliyotolea mfano (US na Israel) na intelligence agencies zao(CIA na Mossad), wakikuambia someone is a traitor or the enemy of the state basi ni traitor na/'au the enemy of the state kweli kweli!

Unfortunately, kwa mtu kama TumainiEl, watu kama akina Ben Saanane, Azory Gwanda, Zitto Kabwe, Tundu Lissu, and the like, kwake hawa ni traitors and/or the enemy of the state!!

Hata akina chige, tusio na ubavu wa kumuondoa madarakani hata Mwenyekiti wetu wa serikali ya mtaa huku Tandika, kwa watu aina ya TumainiEl nasi ni traitors, au the enemy iof the state!

Ukimtoa Gwanda ambae ni Mwandishi, wengine wote wanaoonekana kwamba ni traitors and/or the enemy of the state kimsingi wao ni critics... and most important, wao ni politicians ambao no matter what, lazima wai-challenge administration!

Look at Maria Sarung, with that beautiful and innocent looking face, kwa akina TumainiEl eti nae ni the enemy of the state!

Lakini TumainiEl kaongea jambo lingine muhimu sana:-
Na wao nitaifa kwanza sio mtu.
Akimaanisha kwamba, wa-Israeli na Wamarekani, kwao ni taifa kwanza, na sio mtu! I strongly agree with him!!

Inaelekea Tumaini nae angependa kuona Watanzania wanaoweka mbele maslahi ya nchi yao... watu wanaojitoa kwa ajili ya nchi na sio kwa ajili ya mtu!

The problem ni kwamba, I doubt ikiwa hata yeye mwenyewe anaishi ndani ya hiyo kauli/dhana!!!

Hata hivyo, sina shaka mwenyewe anaamini anaishi ndani ya dhana ya "taifa kwanza", kwa sababu sijui ni nani alituvuruga Watanzania na hatimae kutufanya tuamini serikali ndiyo nchi! Matokeo yake, wengi wanaoamini wanaishi katika dhana ya "taifa kwanza" kimsingi wanaishi ndani ya dhana ya "serikali kwanza"

Matokeo yake, yeyote atakayeikosoa serikali kwao watamuona ni the enemy of the state wakati kimsingi, anayeikosoa serikali anaweza kuwa mfia nchi mkubwa kuliko anayeitetea serikali!

Hawa hawafahamu, kama leo hii Tanzania inaingia vitani (say) na Rwanda, usishangae wale wale walio mstari wa mbele kuikosoa serikali ndio hao hao wakawa mstari wa mbele kupigana dhidi ya adui anayetaka kuvuruga taifa letu; kwa sababu serikali na taifa ni vitu viwili tofauti!

Na taifa kama Israel au US hakuna Enemy of the Government bali kuna Enemy of the State! Tanzania karibu wote wanaoitwa Enemy of the State sio Enemy of the State bali Enemy of the Government, and ijn fact, not even the Enemies of the Government, bali ni Critics of the Government!

Tena bora hata ya hao wanaoamini katika "Serikali Kwanza" manake kuna wengine wengi tu, wao ni "Magufuli kwanza!" Ukimsikia mtu kama Musiba, yule unajua kabisa kwamba kwake ni "Magufuli Kwanza" na wala sio "..Serikali Kwanza" let alone "Taifa Kwanza!"

Ni kutokana na ukweli huo ndio maana wala si ajabu kusikia watu wa aina yake wakishambulia baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa serikali ile ile wanayodhani wanaitetea!!

Kwahiyo nakaa kitako kufuatilia mwendelezo TumainiEl kwa uangalifu mkubwa!!!

Hata hivyo, kuna jambo lingine la msingi zaidi amelitaja ambalo nadhani ndio hasa linatakiwa kutawala mjadala huu kwamba:-
Nikatika taifa hili wakati fulani walipita katika kipindi kugumu na ndipo Mfalme wa wakati ule akaagiza watafutwe vijana wenye akili na maarifa ktk kila eneo kwa jili yakumshauri.
Kwa hakika, ni jambo muhimu sana kwa Decision Makers, na sio Rais peke yake kuzungukwa na watu "wenye akili"

Neno "wenye akili" nimeliweka kwenye kifunga na kifungua semi kwa kuzingatia hali halisi ya Tanzania, na uongozi tulionao! JPM kuwa na watendaji wakuu na mawaziri wenye PhD, anadhani serikali yake inaongozwa na watu wenye akili sana kwa sababu tunapima akili kwa idadi ya vyeti with vertical growth: Mwenye Bachelor Degree>>> Master Degree>>>Doctorate>>>Professor!

Kwa mifumo yenu, na inayoshadadiwa zaidi na JPM, hapo mwenye akili kuliko wote ni Profesa na Kilaza kuliko wote ni mwenye Bachelor! Ingawaje ni kweli pia kwamba huenda hamna namna nyingine ya kupima hao wenye akili wanaweza kupatikanaje patikanaje, lakini ni kweli pia mfumo wa elimu yetu hauna uwezo wa kutengenisha kati ya wenye akili kwa maana ya kuwa na akili, na wale wenye akili kwa maana ya akili ya vyeti huku wakiwa na uwezo mdogo wa kuchambua mambo kwa mapana yake!

Nakumbuka back in the days nilienda kwenye usaili mmoja serikalini! Hakuna interview niliyowahi kuulizwa maswali ya hovyo maishani mwangu kama ile, hadi nikaapa sitaomba tena kazi serikalini, manake there's no way mtu anaweza kunifanya nikeshe usiku kusoma kwa ajili ya kujiandaa na usaili wa kazi kesho yake!!

Eti "nini maana ya MKUKUTA!" "Taja aina za maadili ya umma" :"Kazi za Mkuu wa Wilaya ni zipi" WTF... maswali gani ya kipuuzi hayo!

Kwahiyo naendelea kupigilia msumari kwamba, kama serikali na decision makers wanazungukwa na wenye akili kwa maana ya akili, hakika hilo ndilo linahitajika sana!

Hawa watu wakiwamo kwenye sekta ya usalama, watakuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya Enemy of the State na Enemies Critics of the Government!

Isitoshe, unapokuwa na Vichwa pale Eagle House, na wenyewe wanaweza kuwa na impact kubwa sana kiuchumi hata kama indirectly! Ni hivi vichwa vya Eagle House ndivyo vinavyoweza kutuongoza kwenye masuala ya international cooperation, and of course, international relations.

Aidha, hao Tumaini aliowaita wenye akili wakiwamo kwenye sekta ya uchumi, pia watakuwa na uwezo wa kuchambua mambo kwa mapana na kuweka bayana ina maana gani inaposemwa kuangalia mambo kwa miaka 50-100 ijayo!!

Leo hii mtu anaweza kukuambia JPM anaangalia mbele kwa miaka 50 ijayo ndo maana, for instance, anatumia trilions ku-finance Stiegler's Gorge hata kama kwa uchumi wa sasa inaweza kuwa underutilized, na badala yake kuwa economically viable in the next 5-10 years, au pengine hata zaidi!

Wataongea hayo huku wakisahau dhana ya optimal utilization of our limited resources!!

Kwamba kwanini tutumie kidogo tulichonacho kwa ajili ya investment itakayokuja kuwa materialized in the next 5-10 years wakati kuna fursa kibao bado hazijawa exploited! Fursa ambazo zina uwezo wa kuleta impact kubwa zaidi ya kiuchumi muda mfupi tu baada ya investment kuwa imeshafanyika na hatimae uwekezaji husika ukawa ndie "mzalishaji" wa vitega uchumi vingine!

Tanzania sio kama China yenye Ghost Cities kwa sababu China hawana shida ya capital!
 
Unaambiwa hakuna nchi isiyokuwa na akina Daniel na Yusuph wake, wapo ila nafasi hawapewi, simply tuko kimaslahi binasfi zaidi, ndio maana wakina bashite na ccm aka gambas wanadunda mpaka sasa.
 
Mleta mada huwa hatofautishi taifa na serekali, kwake anayetofautiana na serekali huyo ni msaliti wa taifa na anatakiwa auliwe!!!
 
Back
Top Bottom