Uchaguzi 2020 Mfahamu Yeremia Kulwa Maganja. Mgombea Urais wa NCCR-Mageuzi

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
1597397007662.png

1. Jina YEREMIA KULWA MAGANJA

2. Alizaliwa tarehe 24/12/1967 huko Bunda Mara

3. Alisoma shule ya msingi Balili Bunda na Mlimani Bariadi

4. Kidato cha nne alisoma Iliboru Sekondari huko Arusha. Shule ya vipaji maalum.

5. Kidato cha sita alisoma shule ya Tosamaganga huko Iringa.

6. Ndugu Maganja ana shahada ya uzamili ya Usimamizi wa Biashara kutoka chou kikuu Mzumbe Dar es salaam

7. Pia alipata Shahada ya kwanza ya masuala ya usimamizi wa biashara toka Chuo kikuu cha Tumaini hapa Dar es Salaam

8. Aidha ndugu Maganja amesoma masomo ya computer ngazi ya diploma katika Kituo cha Taifa cha Computer (NCC-UK) cha Uingereza.

9. Ndugu Maganja amefanya kazi mbalimbali hapa nchini na kimataifa. Amefanya kazi na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya -URT katika Kitengo cha Bajeti za Utawala na kitengo cha fedha na mikataba kwa Zaidi ya miaka 18

10. Ndugu Maganja ni mmiliki wa kampuni ya Ushauri na Biashara katika uwekezaji (ANDEL Consultants) ambapo yeye ni Meneja Mkuu.

11. Ndugu Maganja amepata mafunzo mbalimbali katika nchi mbalimbali barani ulaya na afrika ikiwemo Ubeligiji na Kenya

SIASA
• Maganja amekuwa Mjumbe wa kamati ya Wataalam wa M4C ya CHADEMA kanda ya Serengeti ya mikoa ya Mara,Simiyu na shinyanga.

• Ndugu Maganja amekuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo kabla ya Maalim Seif.

• Aidha amekuwa mwenyekiti wa kamati ya oganaizesheni na mafunzo na wanachama ACT wazalendo

• Mjumbe wa kamati ya ukaguzi wa fedha ACT

A. Nafasi hizi za kisiasa zimempa Ndugu Maganja fursa ya kuzunguka nchi mara nyingi Mikoani, Wilayani mpaka vijijini na kuziona shida za Watanzania maskini.

B. Ndugu Maganja ni mzoefu mbobezi kwenye siasa kwa Zaidi ya miaka 10. Analimudu jukwaa ni msomi mzuri sana na nayejua namna ya kujenga taasisi za kisiasa

C. Katika uongozi wake kwenye vyama Ndugu Maganja ameisaidia ACT kupata hati safi za ukaguzi wakati wa uongozi wake. Maganja ana msimamo dhabiti usioyumba yumba na yuko tayari kwa ajili ya kampeni za kuisaka dola mwaka huu 2020

D. Maganja ni muumini wa ushirikiano wa vyama kwa maslahi ya mama Tanzania.
 
Ameifanyia nini NCCR MAAGEUZI
maana umetaja CHADEMA na ACT angali yeye ni mgombea NCCR
 
Back
Top Bottom