Mfahamu Tupac Shakur, nabii aliyepitia maisha ya kihuni

protogonist

Senior Member
Feb 27, 2018
134
250
Nawasalimu wakuu,twende moja kwa moja kwenya Mada.

TUPAC AMAR SHAKUR alizaliwa mnamo tarehe 16 mwezi juni mwaka 1971 ni mtoto wa kiume wa mwanamama AFENI SHAKUR ambaye alikuwa ni mwana harakati wa kupigania haki za watu weusi...wakati Afeni akiwa na ujauzito wa tupac alihukumiwa kwenda jela na wakati yupo jela hakuwa akipatiwa mahitaji muhimu ya mama mjamzito, Afeni alifanikiwa kujifungua katika jiji la Manhattan Ndani ya New York City. Pia baba mzazi wa Tupac anaefahamika kwa jina la Billy Garland waliachana na Afeni wakati Tupac akiwa na umri wa miaka mitano

AFENI SHAKUR
tup mo.jpg

AFENI SHAKUR alizaliwa Alice Faye Williams ndani ya jiji la North Carolina January 10, 1947 Na alifariki May 2, 2016 alikufa kwa shambulio la moyo Afeni alikuwa mwanachama wa chama cha Black Panther Party

BILLY GARYLAND
tupac fat.jpg


BILLY GARYLAND alizaliwa mnamo mwaka June 17, 1949 alikuwa mwanamuziki,mpiga guiter mwandishi wa nyimbo pia alikuwa mwanachama wa chama cha Black Panther Party...Mahusiano yalianza na afeni katika chama hichi

MAISHA YA TUPAC SHAKUR
images.jpg

Tupac shakur alipozaliwa alipewa jina la Lesane Parish Crooks lakini wakati anatimiza mwaka mmoja mama mzazi wa Tupac alimbadilisha jina mtoto wake na kumwita TUPAC AMARU || Asili ya jina la Tupac ni kutoka lugha ya QUECHUA likiwa na maana ya ROYAL inasemekana Afeni alipata jina hilo kutoka Mwana mapinduzi kutoka nchini Peru ambaye alikuwa akipinga sheria za kihispania.

Afeni wakati akimpatia jina hilo mwanae alinuwia maneno yafuatayo na Nukuu "Nampa jina la kimapinduzi ili awe mwana mapinduzi asilia duniani ili ajue kuwa yeye ni sehemu katika dunia na sio jirani"

Mutulu Shakur alikuwa baba wa kambo wa tupac...Mutulu alikuwa akitafutwa na FBI kwa muda wa miaka minne kuanzia mwanzoni mwa mwaka 1982 ilisemekana alimsaidia Asata Shakur kutoroka katika penitentiary katika mji wa New jersey mwaka 1979 Mutulu Shakur alikamatwa mwaka 1986 alipelekwa gerezani kwa kosa tofauti kabisa lililosemekana alihusika katika robbery mwaka 1981 katika tukio hilo maaskari polisi na walinzi waliuawa.

Tupac alikuwa na kaka yake wa kambo anayefahamika kwa jina la Mopreme "Komani" Shakur pia alikuwa na mdogo wake wa kike Sekyiwa.

>>Mnamo mwaka 1984 familia ya Afeni ilihama kutoka New York kwenda Baltimore, Maryland, Wakiwa Baltimore Tupac alisoma Roland Park Middle School alikuwa daraja la nane baada ya hapo akasoma Paul Laurence Dunbar High School kwa miaka miwili, Baada ya kukamilisha mwaka wa pili akiwa katika shule ya Paul Laurence Dunbar High School Tupac alikwenda katika chuo cha Baltimore School for the Arts, ambapo alisomea Uigizaji wa filamu,uandishi wa Mashairi NK....

Tupac alishiriki katika kazi ya fasihi Shakespeare plays...Alishiriki kazi hiyo akiwa na rafiki yake Dane "mouse" Smith ambaye alikuwa akishinda mara kwa mara mashindao ya ku rap hapo chuoni na kuwa rapper bora hapo chuoni Dane alikuwa mtu anayejulikana sana chuoni hapo.

Tupac alianzisha uhusiano na JADA PINKETT (mwanamke ambaye alikuwa nae hadi usiku wa umauti wake)Nukuu "JADA ni moyo wangu"-TUPAC pia aliandika shairi lililoitwa JADA pia aliandika "The Tears in Cupid's Eyes." shairi hili pia lilikuwa kwa ajili ya JADA

KUHAMIA CALIFORNIA
Mnamo mwaka 1988 Tupac na familia yake walihamia Marin City, California Baada ya kuhamia Tupac alikwenda chuo kiitwacho Tamalpais High School kilichopo karibu na Mill Valley. Tupac alichangia katika mchezo wa kuigiza wa hapo chuoni kwao katika darasa la kiingereza, Tupac aliandika Barua iliyokuwa na kichwa cha Habari "Conquering All Obstacles"(KUSHINDA VIZUIZI VYOTE) ambayo ilisema...
"our raps, not the sorry story raps everyone is so tired of. They are about what happens in the real world. Our goal is to have people relate to our raps, making it easier to see what really is happening out there. Even more important, what we may do to better our world. "

Mwaka 1989 Tupac alijiunga na darasa la uandishi Mashairi liliendeshwa na Leila Steinberg Katika mwaka huo huo Alianzisha Tamasha akishirikiana na Shakur's Group "Strictly Dope"; Tamasha liliongozwa na kusainiwa na Atron Gregory. Pia Gregory alimuweka tupac kama roadie na Backup Dancer na kundi la hip hop Digital Underground mwaka 1990

MAISHA NA KAZI YA MUZIKI

Mwanzoni mwa mwaka 1989-93 kabla ya kutumia jina lake la kwanza kama jina lake la jukwaani Tupac alikwenda alias MC New York ambapo alianzisha maisha yake ya muziki 1990s Alishiriki wimbo katika kundi la Digital Underground's wimbo ulifahamika kama "Same Song" katika soundtrack mwaka 1991 film Nothing but Trouble; Pia Alishiriki Digital Underground Tena, Katika album Sons of the P.

Tupac alishirikiana katika utengenezaji wa nyimbo na Shock G and Money-B wanaotoka katika kundi la Digital Underground katika wimbo wake unaofahimika kwa jina la "I Get around"


I GET AROUND.jpg


Mnamo mwaka 1991 Tupac alitoa album yake ya kwanza iliyofahamika kwa jina la 2Pacalypse Now album inatumika kuwa inspire wasanii wadogo wa siku za hivi karibuni pia imevutiwa na wasanii wengi kama Nas, Eminem, Game, and Talib Kweli pia album ilirekodiwa katika studio ya Interscope Records Album ilikuwa katika uangalizi wa Amaru Entertainment, Label ambayo ilikuwa ikimilikwa na Mama yake Tupac.

NITAENDELEA...
 

protogonist

Senior Member
Feb 27, 2018
134
250
Kwamba Nas,Eminem, Game, Talib kweli ni wasanii wadogo wa sasa.?
Hii post utakua umeikopi au umeioitisha google translate
album inatumika kuwa inspire wasanii wadogo wa siku za hivi karibuni pia imevutiwa na wasanii wengi kama Nas, Eminem, Game, and Talib Kweli

SOMA VIZURI CHIEF HAKUNA SEHEMU NILIYOANDIKA EMINEM,NAS,GAME NA TALIB NI WASANII WADOGO

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Abuu Kauthar

JF-Expert Member
Jul 10, 2011
3,401
2,000
Wagalatia neno nabii kwenu ni simple sana, that's why kila mtu dunia hii mkitaka mnapachika unabiii..kuvuta mibangi nakuimba ujinga ujinga ndio unabii huo?
 

jonq

Member
Jul 30, 2015
48
125
"Tupac alianzisha uhusiano na JADA PINKETT (mwanamke ambaye alikuwa nae hadi usiku wa umauti wake)Nukuu "JADA ni moyo wangu"-TUPAC pia aliandika shairi lililoitwa JADA pia aliandika "The Tears in Cupid's Eyes." shairi hili pia lilikuwa kwa ajili ya JADA"


hiyo paragraph sio kweli kuwa alikuwa na Jada usiku ule alipokuwa shooted ila kwa wakati huo walikuwa wameshaachana na alikuwa na Kidada Jones mtoto wa Quincy Jones na ndio alikuwa mchumba wake na alimwacha hotelini yeye akiwa anaenda club na Suge.

Sahihisha hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kalagabaho

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,331
2,000
Sasa kama unawachanganya Jada pinkett na Kidada Jones unachanganya birth date etc etc je . kuna sababu ya kuendelea kuisoma hii post? .. anyway endelea kujifurahisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom