mwandende
JF-Expert Member
- Feb 16, 2017
- 10,518
- 19,883
mkuu,, shahidi kitamshinda nn kutoa ushahidi wa uongo? hata kama kesi ni ya mauaji?Sawa mashahidi wa uongo wapo lakn sio kwa kesi ya mauaji.
Kwanza ukiwa na kesi ya mauaji serikali inakuwekea wakili wa kukutetea.
Kwa kesi ya mauaji ukipeleka shahidi ya kuunga unaweza kuumbuka maana lazma mahakama itamtaka aelezee kwa kina ni namna gani mtuhumiwa amehusika na tukio
Au anajieleza kwa kichina?au kijapani?
Mkuu ,,nenda kwanza japo mahabusu ,ulale japo siku moja.
Ukiwa mule ndani utajuwa nn namaanisha...
Kuna mke wa jirani yangu fulani,, alikuwa ana maneno maneno sana ya ajabu ajabu.
Ananifanyia vituko na visa nyumbani kwangu.
Mara kafanya kile kwangu.
Mara hiki..
Mradi tu. Anisumbuwe,, na siku ukimshtakia kwa mumewe,, basi asubuhi yake akikuona utajuta kwa matusi na kejeli.
Siku nikamwambiya mm sitaki mambo ya ajabu ajabu..
Sijazoea wala sihitaji mambo ya hovyo kwangu.
Basi akakimbilia police,, akatengeneza kesi ,,na mashahidi wa uongo.
nimemtishia kumuua kimaneno..
Aisee!! Kesi ilinisumbuwa sana..
Yule kigagula alitengeneza vigagula wenzie kama 4 ,,mashahidi wa uongo mahakamani,,kwamba nimesema nitamuua. ,kibaya zaidi hao watu sijawahi kuwaona hata siku moja kwenye maisha yangu ,,
Kama nisingekuwa mtoto wa mjini basi ningeishia pabaya..
Nilijiongeza nikaruka sarakasi nyingi. .likaisha hilo.
Kwahyo mkuu, huku Africa 30% ya walio gerezani wametengenezewa kesi. Kwa chuki, au maslahi fulani ya watu.