Mfahamu Samia Suluhu Hassan; Maisha na Kazi

Mambo ya machifu Tanzania hayatambuliki kisheria na yalifutwa kwa sheria ya bunge.Sikuwahi kusikia Nyerere,Mwinyi au Mkapa kupewa uchifu,haya mambo yalianza na kikwete aliyeitwa Chidikula chifu wa waluguru.
Hizi hua ni kama sifa tu ya kumtukuza mtu ili kupata nafasi fulani.
 
Samia Suluhu Hassan (alizaliwa 27 Januari 1960) ni Rais wa 6 wa Tanzania na mwanachama wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi.

Maisha ya awali
Suluhu alizaliwa katika Usultani wa Zanzibar.

Alisoma shule za msingi za Chwaka (Unguja), Ziwani (Pemba) na Mahonda (Unguja) katika miaka ya 1966 hadi 1972.

Aliendelea na masomo ya sekondari shule za Ngambo, Unguja (1973-1975) na Lumumba, Unguja (1976).

Baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari mnamo 1977, aliajiriwa na Wizara ya Mipango na Maendeleo kama karani. Alifuata kozi fupi kadhaa. Mnamo 1986, alihitimu kutoka Taasisi ya Usimamizi wa Maendeleo (Chuo Kikuu cha Mzumbe cha leo) na diploma ya hali ya juu katika utawala wa umma.

Baada ya kuhitimu, aliajiriwa kwenye mradi uliofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Programme). Kati ya miaka 1992 na 1994, alisoma kwenye Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza na kuhitimu stashahada ya uzamili katika uchumi.

Mnamo mwaka 2015, alipata MSc yake katika Maendeleo ya Uchumi wa Jamii kupitia mpango wa pamoja kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo Kikuu cha Kusini mwa New Hampshire.

Kazi ya siasa
Mnamo mwaka 2000 aliamua kujiunga na siasa. Aliteuliwa na CCM kama mbunge wa viti maalum katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar akateuliwa na rais Amani Karume kuwa waziri wa utalii na bishara. Alikuwa mwanamke pekee kwenye ngazi ya mawaziri akaona alidharauliwa na wenzake wa kiume kwa sababu ya jinsia yake. Alichaguliwa tena mnamo 2005 kwenye viti maalum na aliteuliwa tena kama waziri katika wizara ya kazi, jinsia na watoto.

Mwaka 2010 aligombea kwenye uchaguzi kwa Bunge la Kitaifa, akisimama katika jimbo la Makunduchi na kushinda kwa zaidi ya % 80. Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Nchi wa Mambo ya Muungano. Mnamo 2014, alichaguliwa kama Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba iliyokuwa na jukumu la kuandaa katiba mpya ya nchi. Mnamo tarehe 30 Aprili 2021 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM akiwa mwenyekiti wa kwanza mwanamke.

Makamu wa Rais
Mnamo Julai 2015, mteule wa urais wa CCM, John Magufuli alimchagua kuwa mgombea mwenza wa uchaguzi wa 2015 na kumfanya kuwa mgombea mwenza wa kwanza mwanamke katika historia ya chama hicho. Baadaye alikuwa makamu wa rais wa kwanza mwanamke katika historia ya nchi kutokana na ushindi wa Magufuli katika uchaguzi.

Kabla ya kuwa rais kutokana na kifo cha John Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, Suluhu alikuwa makamu wa rais kwa sababu ya kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa mwanamke wa kwanza kufikia cheo hicho, akarudia baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2020.

Sasa amekuwa rais wa kwanza mwanamke na rais wa kwanza kutoka Zanzibar.

Maisha ya binafsi
Mnamo 1978 aliolewa na Hafidh Ameir aliye kwa sasa afisa kilimo mstaafu. Wana watoto wanne: binti mmoja na wavulana watatu. Binti yake Wanu Hafidh Ameir (aliyezaliwa 9 Februari 1982), mtoto wa pili, ni mbunge wa viti maalum katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Kutoka 2015 hadi 2020 na ni Mwanasheria kitaaluma alipata shahada ya awali kutoka Chuo kikuu huria cha Tanzania (Open university of Tanzania).

Samia Suluhu Hassan pia ni Chief wa Kwanza wa kike kutokea Nchini Ambapo alipewa Jina la Hangaya lenye maana ya nyota inayo ng'ara kutoka Lugha ya kisukuma. Uchifu alipewa na machifu wa kabila la kisukuma na yeye kuwa chifu wa machifu Tanzania

Historia ya Nyerere iko wazi.
Kasomi tuletee historia kamili tumjue vizuri huyu mama, labda tutajua sababu kwanini anafanya anayoyafanya.

Mfano inabidi tujue Wake wenza ni kina nani, familia zao zote, familia ya mme wake, Wazazi wake, Babu zake, watoto wote kwenye familia ya wake wanne.

Wazazi na mabibi na mababu kweny upande wa mme wale na wake wenza watatu.

Background yake itatusaidia kujua kwanini anachukua maamuzi anayochukua.
 
Sawa mkuu ngoja nijitahidi kuchunguza hayo yote ili kuweza bayana historia nzima.
 
Sawa mkuu ngoja nijitahidi kuchunguza hayo yote ili kuweza bayana historia nzima.

Poa. Itatusaidia sisi Wananchi. Hata kujua Mentality yake.

Nilisoma miezi kadhaa nyuma amepata cheti chake Salford University, CV imebadilishwa sasa ni Manchester University.

Anyway Viongozi wengi wetu elimu zao ni za kuungaunga.
 
Kweli lakini ngoja tuchunguze zaidi juu ya historia yake kiundani.
 
Elimu ya Samia ina utata kiukwel hakuna sehemu aliyopata shahada ya kwanza Zaid n diploma za kat na za juu

Utata Zaid unakuja kwenye hii shahada ya pili sjui imekaaje yaan namna ya kuiita naona Kama n shida

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Elimu yake inaonekana kuwa na utata sababu hakusoma moja kwa moja amesoma kwa kuunga unga.
 
Poa. Itatusaidia sisi Wananchi. Hata kujua Mentality yake.

Nilisoma miezi kadhaa nyuma amepata cheti chake Salford University, CV imebadilishwa sasa ni Manchester University.

Anyway Viongozi wengi wetu elimu zao ni za kuungaunga.
Itakuwa Manchester united.
 
Back
Top Bottom