Mfahamu Salum Shamte (1951 - 2020)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,839
30,168
Alizaliwa tarehe 10.7.1951

Elimu
Alisoma shule ya msingi ya Mawenge Middle School mwaka 1961 hadi 1964
1965 hadi 1965 St. Francis College Pugu
1969 hadi 1970 Shinyanga Secondary ‘’A’’ Level
1971 jeshini Oljoro
1971 hadi 1974 Nairobi University akichukua Shahada ya Biashara
1978 hadi 1979 alisoma Arthur de Little Management Education Institute, Boston, Massachusets – USA.
1975 hadi 2007 alihudhuria kozi katika mataifa ya Tanzania, UK. Netherlands, Italy katika kozi fupi za Shipping, Masoko, Utawala na Masuala ya Kisiasa za Kimataifa.

Kazi
• 1974 hadi 1975 aliajiriwa na Mamlaka ya Korosho Tanzania akiwa Manager Trainee
• Baadaye aliateuliwa na Mamlaka ya Korosho Tanzania kuwa Mtafiti wa Masoko na Takwimu
• Aliajiriwa na mamlaka ya Mkonge Tanzania mwaka 1975 akiwa Meneja Masoko Msaidizi.
• 1976 alifanya kazi tawi la TSA Dar es Salaam akiwa Meneja wa Tawi kwa miezi sita akathibitishwa kuwa Meneja Masoko mwaka 1977 -1979
• Mwaka 1980 - 1981 alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Masoko
• Mwaka 1981- 1989 alikuwa mkurugenzi mwendeshaji wa TASMA – Tanganyika Sisal Marketing Association (UK) Ltd. iliyokuwa na makao yake London akishughulika na masoko ya singa na bidhaa zake pamoja na chai, akifanya kazi katika ngazi ya kimataifa akiwakilisha Mamlaka ya Tanzania katika masuala yote ya sekta ya mkonge.
• Mwaka 1989 - 1992 alikuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko (Director of Operations and Marketing) wa iliyokuwa mamlaka ya Mkonge Tanzania.
• Mwaka 1992 – 1998 alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mkonge Tanzania aliyehusika pia na ubinafsishaji wa Mamlaka ya Mkonge Tanzania wakati serikali ilipoamua kuibinafsisha Mamlaka ya Mkonge Tanzania.
• Mwaka 1998 hadi 2017 alikuwa Mkurugenzi Mtendaji Katani Limited hadi alipostaafu kwa hiari yake mwenyewe.
• Kwa kipindi chake chote baada ya kustahafu, marehemu alikuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Katani Limited na kampuni zake tanzu zikiwemo TANCORD (1998) Ltd na MES kwa vipindi tofauti, pia alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni tanzu ya Katani Ltd ya Kilimo Engineering Services Limited (KES) hadi umauti unamfika.
Nyadhifa na shughuli nyingine za kijamii
• Skauti Tanzania 1965 hadi 1970 alipanda na kuwa Rais wa Skauti Tanzania
• 1972/1973 alikuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Nairobi
• Mjumbe wa kamati tendaji ya ISA – London Sisal Association ambayo iliwaunganisha wazalishaji, wauzaji na watumiaji wa singa za mkonge na bidhaa zake kimataifa kuanzia mwaka 1982 hadi mauti ilipomfika
• Mwenyekiti wa London Sisal Association kwa vipindi viwili mwaka 1985 -1987 na 2008 – 2010.
• Rais wa london sisal association mwaka 1987 - 1989 akiwakilisha nchi katika mikutano ya wazalishaji singa duniani kupitia – FAO Inter-Gorvernmental Group on hard fibres yenye makao makuu Rome Italia kuanzia 1976 hadi umauti ulipomfika.
• Mwenyekiti wa wataalam wa FAO IGG – hard fibres mwaka 1985
• Mwanachama wa kamati ya utendaji ya Watanzania waliokuwa wanaishi Uingereza 1987 hadi 1989
• Mwenyekiti wa FAO IGG hard fibres mwaka 1986
• Mwenyekiti wa FAO IGG on hard fibres 1990 - 1991 na 2017 hadi 2019
• Mweka hazina wa UK Business Group London 1987 hadi 1989
• Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Wakulima wa Mkonge Tanzania – SAT - Sisal Association of Tanzania 1989 - 2017
• Makamu Mwenyekiti wa SAT 1997- 1998
• Mwenyekiti wa SAT 1998 – 2004
• Mjumbe wa Bodi ya Benki Kuu 1996 haddi 2002
• Mwenyekiti wa Bodi ya TPI – Tanzania Pharmaceutical Industries mpaka umauti unamfika
• Mjumbe wa bodi wa Tanzania Foundation for Civil Society 2004 hadi 2007
• Mwenyekiti wa Agricultural Council of Tanzania 2007 mpaka umauti unamfika
• Mjumbe wa Bodi ya Biashara ya Nje – Board of External Trade 2005 hadi 2008
• Mratibu wa miradi ya maendeleo ya mkonge chini ya CFC/UNIDO 1997 – 2007
• Mwenyekiti wa bodi ya ranchi za taifa 2006 mpaka
• Mjumbe wa Bodi Ssekta Binafsi – Tanzania Private Sector Foundation 2007 mpaka umauti unamkuta
• Mwanachama wa Baraza la Biashara la Taifa – Tanzania National Business Council
• Mwenyekiti wa bodi ya baishara ya nje 2008 hadi uauti unamfika.

Hayo yote Mzee Shamte alikuwa akiyafanya pamoja na kusaidia jamii katika nyanja nyingi zikiwemo za siasa, kijamii, elimu, na kwa namna ya pekee kwa kuwajali na kufikiria kuwaondoa katika dimbwi la umaskini wananchi hasa wanaoishi na waliokuwa manamba katika mashamba ya mkonge ya wakoloni,

Alianzisha kilimo cha wakulima wadogo wa mkonge Tanzania katika mashamba matano ya kampuni ya Katani Limited, ili kuwainua wananchi katika umaskini na kuongeza zao la biashara kwa wananchi wa tanga na taifa kwa ujumla.
Kilimo hiki kilianzishwa mwaka 2007 kikiwa na wakulima 720. Hadi mwaka 2020 wakulima wadogo wa mkonge wamefikia 1,200.

Katika uhai wake aliweza kuisimamia katani ltd na kujenga viwanda ili kukidhi mahitaji ya wakulima wadogo wa mkonge ili kusindika mkonge wao na pia kufufua kiwanda cha TANCORD kilichokuwa kimekufa.

Mwaka 2019 sekta ya mkonge ilipata heshima kubwa ya kuwa na Mwenyekiti wa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Ukanda wa Afrika (SADCC) ambaye ni Mwanankonge na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Katani Limited Bwana Salum Juma Shamte.

Mwaka 2019 mwezi wa oktoba Mzee Shamte na wenzake wanne walikamatwa kwa tuhuma za kuhujumu uchumi na kutakatisha pesa na kuwekwa mahabusu Chumbageni na hatimaye Gereza la Maweni Tanga, alipatwa na maradhi na baadae 23 Machi alilazwa hospitali ya Muhimbili kwenye wadi ya wagonjwa mahututi ambako alikuwa huko hadi umauti unamkuta.
Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Katani Limited, Mzee Shamte, atakumbukwa zaidi kwa aina yake ya uongozi, akiwa msikivu zaidi ya kuwa muongeaji, akiwa mpokea ushauri zaidi ya mtoa maelekezo na pia akiwa kiongozi aliyewapenda na kuwathamini wafanyakazi wote walio chini yake pamoja na wadau wote wanaoizunguka sekta ya mkonge.

Mzee Shamte alikuwa mwaminifu na mtiifu kwa nchi yake na kada wa chama tawala cha ccm na jumuiya zake na alishiriki shughuli za kichama katika ngazi zote.

Sisi tulimpenda sana lakini kwa Mwenyezi Mungu ahadi ikifika hakuna wa kuaghirisha.
Marehemu ameacha wake watatu na watoto saba, wanaume watatu na wanawake wanne. tunamuomba Mwenyezi Mungu aipe familia yake subra katika kipindi hiki kigumu.

Mungu amjalie kauli thabiti, Kiongozi, Mwalimu, Kocha, Mtaalamu Mzee Salum Juma Shamte,

Mkonge ni Tanga na Tanga ni mkonge na hatimaye Tanzania nzima itakuwa ni mkonge

SALUM JUMA SHAMTE 1951 - 2020.jpeg
 
Hapa duniani unaweza kufanya mengi sana mazuri, lakini kosa moja likafuta mazuri yote! Kosa la Salum Shamte ni conflict of interest, ni kushiriki mchakato wa kubinafsisha zao la mkonge kwa kampuni ya Katani Ltd, wakati na yeye akiwa mmoja wa shareholders na kiongozi wa Katani Ltd.
 
Walioshiriki uamuzi wa kuuza Nyumba za serikal na kupanga bei ya nyumba hizo ndio walikuwa wanunuzi wakuu wa nyumba hizo na zingine kugawa kwa 'wanaowapenda'
hapa duniani unaweza kufanya mengi sana mazuri, lakini kosa moja likafuta mazuri yote! kosa la Salum Shamte ni conflict of interest, ni kushiriki mchakato wa kubinafsisha zao la mkonge kwa kampuni ya Katani Ltd, wakati na yeye akiwa mmoja wa shareholders na kiongozi wa Katani Ltd!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa duniani unaweza kufanya mengi sana mazuri, lakini kosa moja likafuta mazuri yote! kosa la Salum Shamte ni conflict of interest, ni kushiriki mchakato wa kubinafsisha zao la mkonge kwa kampuni ya Katani Ltd, wakati na yeye akiwa mmoja wa shareholders na kiongozi wa Katani Ltd!
Laki...
Unamuhukumu kabla hujasikiliza ushahidi wake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa duniani unaweza kufanya mengi sana mazuri, lakini kosa moja likafuta mazuri yote! kosa la Salum Shamte ni conflict of interest, ni kushiriki mchakato wa kubinafsisha zao la mkonge kwa kampuni ya Katani Ltd, wakati na yeye akiwa mmoja wa shareholders na kiongozi wa Katani Ltd!
Usisahau ARV fake za shemeji yake wakati yeye ni chair Wa TPI
 
Njinjo,
Tofauti yangu na wewe ni kuwa wewe unaandika ukiwa huna taarifa ambazo mimi ninazo.
Wafanyabiashara wanahujumiana sana.

Kesi iko mahakamani tusubiri.
Tofauti yetu kila wakati ni wewe kutanguliza mahaba mbele kuliko ukweli. Mie namjua sana na hata issue ya Push Mobile. Hakuwa msafi kama weye unavyopenda kila wakati watu wahusudu na kusujudu. Kila makala zako ni za hivyo hivyo. Badilika uwe NEUTRAL ndiyo uandishi wa kuangalia pande mbili za shillingi
 
Mkuu, marehemu anahusikaje na kesi ya Push Mobile?
 
Tofauti yetu kila wakati ni wewe kutanguliza mahaba mbele kuliko ukweli. Mie namjua sana na hata issue ya Push Mobile. Hakuwa msafi kama weye unavyopenda kila wakati watu wahusudu na kusujudu. Kila makala zako ni za hivyo hivyo. Badilika uwe NEUTRAL ndiyo uandishi wa kuangalia pande mbili za shillingi
Njinjo,
Hilo la mahaba na mengineyo kama unavyonifikiria na kuwafikiria wengine ni fikra zako hakuna wa kukuingilia.

Hapa ni suala la "dawa feki," nami nimekujibu.

Sasa nakuongezea lingine labda hulijui.
Kesi iko mahakamani huu mwaka wa saba.

Kinachotakiwa ni ushahidi kuwa dawa zile zilikuwa feki.

Bado tunasubiri ushahidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa duniani unaweza kufanya mengi sana mazuri, lakini kosa moja likafuta mazuri yote! Kosa la Salum Shamte ni conflict of interest, ni kushiriki mchakato wa kubinafsisha zao la mkonge kwa kampuni ya Katani Ltd, wakati na yeye akiwa mmoja wa shareholders na kiongozi wa Katani Ltd.
Huo ndio uhujumu uchumi?
Hiyo ni tuhuma isiyo na dhamana?
Baba wa watu kachukuliwa nyumbani kapelekwa mahabusu, kisha hospitali na hatimaye akarejeshwa akiwa maiti. Kwa tuhuma ya 'conflict of interest'.
Tusemeje sasa?
 
Hapa duniani unaweza kufanya mengi sana mazuri, lakini kosa moja likafuta mazuri yote! Kosa la Salum Shamte ni conflict of interest, ni kushiriki mchakato wa kubinafsisha zao la mkonge kwa kampuni ya Katani Ltd, wakati na yeye akiwa mmoja wa shareholders na kiongozi wa Katani Ltd

Sawa hata kama unasema kosa lake ni kwasababu ya conflict of interest kwa kushiriki kubinafsisha zao la mkonge kwa kampuni ya Katani Ltd, yeye akiwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo swali ni je kubinafsisha huko kwa hizo assets alifanya yeye peke yake ? Kama hakufanya peke yeke hao wengine walioshiriki katika zoezi hilo wako wapi? Salum Shamte asingeweza kujibinafsishia hizo mali bila ridhaa ya PSRC na ofisi ya Waziri Mkuu ambao ndio walikuwa waratibu wakuu wa zoezi zima la ubinafsishaji!!! Hawa wengine mbona hawakufikishwa mahakamani? Somebody has Salum's blood in his hands!!
 
Alizaliwa tarehe 10.7.1951

Elimu
Alisoma shule ya msingi ya Mawenge Middle School mwaka 1961 hadi 1964
1965 hadi 1965 St. Francis College Pugu
1969 hadi 1970 Shinyanga Secondary ‘’A’’ Level
1971 jeshini Oljoro
1971 hadi 1974 Nairobi University akichukua Shahada ya Biashara
1978 hadi 1979 alisoma Arthur de Little Management Education Institute, Boston, Massachusets – USA.
1975 hadi 2007 alihudhuria kozi katika mataifa ya Tanzania, UK. Netherlands, Italy katika kozi fupi za Shipping, Masoko, Utawala na Masuala ya Kisiasa za Kimataifa.

Kazi
• 1974 hadi 1975 aliajiriwa na Mamlaka ya Korosho Tanzania akiwa Manager Trainee
• Baadaye aliateuliwa na Mamlaka ya Korosho Tanzania kuwa Mtafiti wa Masoko na Takwimu
• Aliajiriwa na mamlaka ya Mkonge Tanzania mwaka 1975 akiwa Meneja Masoko Msaidizi.
• 1976 alifanya kazi tawi la TSA Dar es Salaam akiwa Meneja wa Tawi kwa miezi sita akathibitishwa kuwa Meneja Masoko mwaka 1977 -1979
• Mwaka 1980 - 1981 alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Masoko
• Mwaka 1981- 1989 alikuwa mkurugenzi mwendeshaji wa TASMA – Tanganyika Sisal Marketing Association (UK) Ltd. iliyokuwa na makao yake London akishughulika na masoko ya singa na bidhaa zake pamoja na chai, akifanya kazi katika ngazi ya kimataifa akiwakilisha Mamlaka ya Tanzania katika masuala yote ya sekta ya mkonge.
• Mwaka 1989 - 1992 alikuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko (Director of Operations and Marketing) wa iliyokuwa mamlaka ya Mkonge Tanzania.
• Mwaka 1992 – 1998 alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mkonge Tanzania aliyehusika pia na ubinafsishaji wa Mamlaka ya Mkonge Tanzania wakati serikali ilipoamua kuibinafsisha Mamlaka ya Mkonge Tanzania.
• Mwaka 1998 hadi 2017 alikuwa Mkurugenzi Mtendaji Katani Limited hadi alipostaafu kwa hiari yake mwenyewe.
• Kwa kipindi chake chote baada ya kustahafu, marehemu alikuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Katani Limited na kampuni zake tanzu zikiwemo TANCORD (1998) Ltd na MES kwa vipindi tofauti, pia alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni tanzu ya Katani Ltd ya Kilimo Engineering Services Limited (KES) hadi umauti unamfika.
Nyadhifa na shughuli nyingine za kijamii
• Skauti Tanzania 1965 hadi 1970 alipanda na kuwa Rais wa Skauti Tanzania
• 1972/1973 alikuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Nairobi
• Mjumbe wa kamati tendaji ya ISA – London Sisal Association ambayo iliwaunganisha wazalishaji, wauzaji na watumiaji wa singa za mkonge na bidhaa zake kimataifa kuanzia mwaka 1982 hadi mauti ilipomfika
• Mwenyekiti wa London Sisal Association kwa vipindi viwili mwaka 1985 -1987 na 2008 – 2010.
• Rais wa london sisal association mwaka 1987 - 1989 akiwakilisha nchi katika mikutano ya wazalishaji singa duniani kupitia – FAO Inter-Gorvernmental Group on hard fibres yenye makao makuu Rome Italia kuanzia 1976 hadi umauti ulipomfika.
• Mwenyekiti wa wataalam wa FAO IGG – hard fibres mwaka 1985
• Mwanachama wa kamati ya utendaji ya Watanzania waliokuwa wanaishi Uingereza 1987 hadi 1989
• Mwenyekiti wa FAO IGG hard fibres mwaka 1986
• Mwenyekiti wa FAO IGG on hard fibres 1990 - 1991 na 2017 hadi 2019
• Mweka hazina wa UK Business Group London 1987 hadi 1989
• Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Wakulima wa Mkonge Tanzania – SAT - Sisal Association of Tanzania 1989 - 2017
• Makamu Mwenyekiti wa SAT 1997- 1998
• Mwenyekiti wa SAT 1998 – 2004
• Mjumbe wa Bodi ya Benki Kuu 1996 haddi 2002
• Mwenyekiti wa Bodi ya TPI – Tanzania Pharmaceutical Industries mpaka umauti unamfika
• Mjumbe wa bodi wa Tanzania Foundation for Civil Society 2004 hadi 2007
• Mwenyekiti wa Agricultural Council of Tanzania 2007 mpaka umauti unamfika
• Mjumbe wa Bodi ya Biashara ya Nje – Board of External Trade 2005 hadi 2008
• Mratibu wa miradi ya maendeleo ya mkonge chini ya CFC/UNIDO 1997 – 2007
• Mwenyekiti wa bodi ya ranchi za taifa 2006 mpaka
• Mjumbe wa Bodi Ssekta Binafsi – Tanzania Private Sector Foundation 2007 mpaka umauti unamkuta
• Mwanachama wa Baraza la Biashara la Taifa – Tanzania National Business Council
• Mwenyekiti wa bodi ya baishara ya nje 2008 hadi uauti unamfika.

Hayo yote Mzee Shamte alikuwa akiyafanya pamoja na kusaidia jamii katika nyanja nyingi zikiwemo za siasa, kijamii, elimu, na kwa namna ya pekee kwa kuwajali na kufikiria kuwaondoa katika dimbwi la umaskini wananchi hasa wanaoishi na waliokuwa manamba katika mashamba ya mkonge ya wakoloni,

Alianzisha kilimo cha wakulima wadogo wa mkonge Tanzania katika mashamba matano ya kampuni ya Katani Limited, ili kuwainua wananchi katika umaskini na kuongeza zao la biashara kwa wananchi wa tanga na taifa kwa ujumla.
Kilimo hiki kilianzishwa mwaka 2007 kikiwa na wakulima 720. Hadi mwaka 2020 wakulima wadogo wa mkonge wamefikia 1,200.

Katika uhai wake aliweza kuisimamia katani ltd na kujenga viwanda ili kukidhi mahitaji ya wakulima wadogo wa mkonge ili kusindika mkonge wao na pia kufufua kiwanda cha TANCORD kilichokuwa kimekufa.

Mwaka 2019 sekta ya mkonge ilipata heshima kubwa ya kuwa na Mwenyekiti wa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Ukanda wa Afrika (SADCC) ambaye ni Mwanankonge na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Katani Limited Bwana Salum Juma Shamte.

Mwaka 2019 mwezi wa oktoba Mzee Shamte na wenzake wanne walikamatwa kwa tuhuma za kuhujumu uchumi na kutakatisha pesa na kuwekwa mahabusu Chumbageni na hatimaye Gereza la Maweni Tanga, alipatwa na maradhi na baadae 23 Machi alilazwa hospitali ya Muhimbili kwenye wadi ya wagonjwa mahututi ambako alikuwa huko hadi umauti unamkuta.
Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Katani Limited, Mzee Shamte, atakumbukwa zaidi kwa aina yake ya uongozi, akiwa msikivu zaidi ya kuwa muongeaji, akiwa mpokea ushauri zaidi ya mtoa maelekezo na pia akiwa kiongozi aliyewapenda na kuwathamini wafanyakazi wote walio chini yake pamoja na wadau wote wanaoizunguka sekta ya mkonge.

Mzee Shamte alikuwa mwaminifu na mtiifu kwa nchi yake na kada wa chama tawala cha ccm na jumuiya zake na alishiriki shughuli za kichama katika ngazi zote.

Sisi tulimpenda sana lakini kwa Mwenyezi Mungu ahadi ikifika hakuna wa kuaghirisha.
Marehemu ameacha wake watatu na watoto saba, wanaume watatu na wanawake wanne. tunamuomba Mwenyezi Mungu aipe familia yake subra katika kipindi hiki kigumu.

Mungu amjalie kauli thabiti, Kiongozi, Mwalimu, Kocha, Mtaalamu Mzee Salum Juma Shamte,

Mkonge ni Tanga na Tanga ni mkonge na hatimaye Tanzania nzima itakuwa ni mkonge

Pia alikuwa mwajiriwa wa ile idara pendwa.
 
Back
Top Bottom