Mfahamu Profesa Safari anayetaka kumng'oa Prof Lipumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfahamu Profesa Safari anayetaka kumng'oa Prof Lipumba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Giro, Feb 20, 2009.

 1. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Source: Taifa Tanzania

  Chama cha CUF kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu wake Ijumaa ijayo February 27,mwaka huu ambapo Profesa Abdallah Jumbe Saffari anawania nafasi ya Uwenyekiti,nafasi ambayo kwa hivi sasa inashikiliwa na Profesa Ibrahimu Lipumba ambaye ameshika nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

  Profile:
  Profesa Safari alizaliwa June 3, 1951.

  Education background:
  1972- Secondary,
  1979- University of Dar es salaam shahada ya sheria (LLB),
  1985- Master (LLM),
  1995- (PhD) University of Sussex England.Baada ya kupata shahada hiyo
  alibaki England akawa anafundisha,
  2000- Alitunukiwa u Profesa.

  Work Experience
  1972-1974 Matafiti msaidizi katika taasisi ya Institutes of Kiswahili Research
  1974-1976 Mhariri katika kampuni ya Tanzania Publishing House
  1979-1986 Wakili wa serikali katika wizara ya sheria
  1988-1991 Afisa Mtafiti na uchapishaji katika kituo cha Uhisiano wa nje then
  Mhadhiri mwandamizi wa sheria katika kituo hicho Nyazifa(Vyeo)
  alivyowahi kushika;
  1978-1986 Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wa chuo Kikuu cha Dar es
  Salaam
  1982-1984 Mhadhiri wa sheria university of Dar es Salaam
  1983-1986 Mkuu wa Kitengo cha sheria ,wizara ya sheria
  1984-1986 Mwakilishi wa wizara ya sheria katika baraza la elimu ya sheria
  Africa Mashariki
  1990-1991 Kaimu Mkurugenzi wa masomo na program katika kituo cha
  mahusiano ya kimataifa
  1996-Hadi sasa, Mwenyekiti wa chama cha wandishi wa Vitabu Tanzania
  (UWAVITA),pia Mkurugenzi wa Masomo na programu wa kituo cha
  uhusiano wa Kimataifa
  1999-Hadi sasa, Katibu Mkuu wa Tanzania Center for Conflict Resolution,
  also Mkurugenzi wa bodi ya hakimiliki(COSOTA)

  Makongamano:
  1978-Alihudhuria mikutano kadhaa ya Kimataifa kuhusiana na mambo ya
  sheria barani Africa huko Nairobi (All African Law Students Association)
  Aidha,amewahi kuhudhuria makongamano mbalimbali yaliyohusu
  mambo ya sheria katika sehemu zifuatazo,Africa
  Kusini,Sweden,Geneva,Botswana,Uganda na Marekani.

  Tuzo alizowahi kupata:
  1991-alitunukiwa tuzo iitwayo Ford Foundation Scholarship for Doctor of
  Philosophy programme
  1999-2001, Shaaban Robert Literary

  Maisha yake:
  Ameoa na ana watoto wawili.
  Prof anasema anawania Uenyekiti wa CUF kwa kuwa anataka kuleta mabadiliko makubwa ndani ya chama ili kionekane ni cha kitaifa.Alisema bila mbadiliko chama kinaweza kufa.
  Prof hivi sasa ni wakili katika Mahakama Kuu ya Tanzania,amekuwa katika uwakili tangu 1987.
  ........................................
  Kazi kwenu wana CUF ,kuchagua nazi au koroma siku ikijiri(27/02/2009),kila la kheri katika uchaguzi wenu.
   
Loading...