Mfahamu Nandy wa South Korea bibiye IU

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Jina lake halisi ni Lee Ji Eun na amezaliwa mwaka 1993 alitoa wimbo wake wa kwanza akiwa na miaka 15 tu na tangu hapo hakurudi nyuma hata sekunde.

Watanzania wengi tulimtambua baada ya yeye kushiriki kwenye series Ya MOON LOVERS : SCARLET RYEO na HOTEL DE LUNA ya mwaka 2019 akiigiza kama JANG MAN WOL mmiliki wa hoteli hiyo inayopatikana Myeong Dong South Korea.

Lakini ukweli ni kwamba ukiachana na umachachari wake kwenye kuigiza IU ana sauti nzuri sana.

Anyway nisije nikamwagia sifa nyingi nikaishia kuharibu uzi, hivi ni vitu 10 ambavyo huvifaham kuhusiana na mwanadada huyu :

10) Ana uzito wa kilo 47 na urefu wa 165 cm.

9) IU jina lake la kisaniii limetokana na maneno I and You sasa badala ya YOU akaweka U.

8) IU alitoa wimbo wake wa kwanza na kuingia rasmi kwenye Tasnia ya muziki mwaka 2008 akiwa na miaka 15 tu

7) Wakorea wengi humtambua kwa jina la "Nation's Little Sister" wakimaanisha Dada Mdogo wa taifa kutokana na kuwa na umbo dogo pamoja na innocent image.

6) Rangi pendwa za IU ni Njano na Nyekundu.

5) Wakati anaanza muziki alishawahi kutapeliwa baada ya kutuma pesa alizopata kwa bibi yake kwa waliojiita ma-meneja ili apate deal na record label kubwa.

4.Tangu aanze muziki IU ameachia album 5, EP 9 na jumla ya nyimbo 47 kama singles. Hivyo basi mwambieni Zuchu asiogope kutoa EP nyingine maana wenzake wanazo nyingi tu.

3. IU yuko chini ya record labels tatu LOEN ENTERTAINMENT inayoshughulika na kazi zake za nchini Korea, EMI ya inayosimamia kazi zake nchini Japan na GOLDEN CITY TYPHOON inayosimamia kazi zake nchini Taiwan.

2. IU ni moja ya wasanii wachache wa nchini Korea ambao hawajasoma Chuo kikuu.

1 Mwaka 2014 alitoa EP inayoitwa FLOWER REMAKE ambapo alichukua nyimbo za wasanii wa zamani na kuzitengeneza upya kama cover, wimbo kama "Meaning of you". EP hiyo pamoja na kutokuwa na nyimbo mpya ilienda mpaka namba 2 huko nchini Korea.
d36bb83b28ce400fbd8f17918e6003bb.jpg
iu.jpg
iu-lilac-photo-edam-entertainment%402000x1270-1.jpg
 
Wana matatizo Sana kpop stars ..kuanzia kunyimwa kula ili wawe slim... Au kula mlo mmoja ..au kunywa maji tuu.. Kunyimwa kuwa na mahusiano. Kuzuiwa kuishi maisha wanayotaka..
Wengi wamejiua .. Wengi wameanguka stejini.

Kulazimishwa kufanya plastic surgeries ili waonekana warembo kwenye Luninga.
Kama una sura Kama ya wa stendi Huwezi kuingia Kwenye kpop industry..
Na mengine mengi .


Ova
 
Wana matatizo Sana kpop stars ..kuanzia kunyimwa kula ili wawe slim... Au kula mlo mmoja ..au kunywa maji tuu..
Kunyimwa kuwa na mahusiano.
Kuzuiwa kuishi maisha wanayotaka..
Wengi wamejiua ..
Wengi wameanguka stejini.
Kulazimishwa kufanya plastic surgeries ili waonekana warembo kwenye Luninga.
Kama una sura Kama ya wa stendi Huwezi kuingia Kwenye kpop industry..
Na mengine mengi .


Ova
🙄🙄🙄🙄🚶🚶🚶
 
Back
Top Bottom