Mfahamu muuaji Jason Eric Massey na matukio yaliyopelekea hukumu yake.

the viking

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
1,170
1,371
Jason Eric Massey alizaliwa januari 7 1973 kule Ellis county,Texas.Katika umri mdogo,alipitia changamoto kubwa ya malezi kwani babake alikuwa mlevi mkubwa naye mamake alikuwa mhadhiriwa wa madawa ya kulevya.Inaaminika kwamba wazazi wake hawakuwa na makazi maalum kwani muda wote walikuwa wakihamahama,jambo lililopelekea wakati mmoja waishi kwenye gari la mama yao.

Mfumo huu wa maisha ulipelekea kijana huyu kutokamilisha masomo yake na kuwa mkosa maadili mkubwa kwani katika ujana wake tayari alikuwa amehusika na uvunjaji sheria kwa kiwango fulani.Wakati mmoja mamake alitaka kumpeleka kwa daktari wa akili alipokutana na vitabu vya kumbukumbu alivyoviandika Jason na ambavyo vilihusiana na mauaji ya wanyama kama vile paka na mbwa..
IMG_20170823_154844_212.jpg
Jason Massey

usiku wa Julai 26 1993,Jason Massey alienda nyumbani kwa mzee mmoja aliyejulikana kama Bw.King kumchukua mwanawe King ili waandamane kwenye ziara za usiku.alimkuta kijana huyo amelala nje ya nyumba anapunga unyunyu na baada ya mazungumzo kijana huyo akaingia kwenye gari na wakaondoka.kijana huyo mwenye umri wa miaka kumi na minne alikuwa James Brian King.

Siku iliyofuata,wafanyakazi wa mji huo katika harakati zao waligundua mwili wa msichana mmoja mdogo uliokuwa umefichwa chini ya magugu na ambao haukuwa na nguo.kichwa kulikuwa kimekatwa na mikono pia haikuwepo.chuchu za matiti yake zilikuwa zimekatwa pia na mwili wake kuchajwa sehemu flani flani.yapata mita tano kutoka hapo,chini ya daraja la mbao,waliupata mwili wa kijana mmoja mdogo ila huyu alikuwa na nguo zake

.
IMG_20170823_154940_194.jpg
James Brian King na dadake wa kambo Christina Benjamin

Uchunguzi ulianzishwa ila wahusika hawakuwa na udhibitisho wowote au chochote ambacho wangeweza kutegemea katika kutatua kesi hiyo isipokuwa vinywele kadhaa walivyovipata vimening'inia sehemu flani.

kama kawaida,jambo la kwanza katika kesi ya aina hii ni kubaini mwili au miili iliyopatikana ni ya nani. kwenye mfuko wa suruali ya kijana Brian King wachunguzi walipata kibeti na ndani mlikuwa na kadi ya chumba cha uhifadhi wa vitabu(library).babake Brian alipopelekewa kile kibeti alikigundua na pia alisema kwamba ule mwili wa msichana uliopatikana pamoja na mwili wa Brian huenda ni mwili wa mwanae Christina Benjamin ambaye inaaminika alikuwa ametekwa nyara na Jason siku moja kabla ya mauaji hayo kutokea.

Mwili wa msichana huyo haukuonyesha dalili zozote za unajisi na hapo majasusi waliogopa wasije wakakosa ushahidi wowote wa kumuunganisha mshukiwa na mauaji hayo.Baada ya kuchunguza miili hiyo kwa umakini,walipata unywele ambao haukuendana na nywele za Brian King wala Christina Benjamin.pia,kwenye kiatu chake Brian,walipata kiuzi flani ambacho baada ya kuchunguzwa kilikotoka walibaini kilitoka kwenye mkeka ndani ya gari zilizotengenezwa na kampuni fulani.

polisi walipokea simu kutoka kwa wakaazi wa mtaa huo kuwa Jason Massey pamoja na vijana wale marehemu walikuwa na mpango wa kuandamana kwenye ziara ya usiku..jambo ambalo ni la kawaida kabisa kwa watoto wa marekani.pia,walipokea simu kuwa kuna ndama mmoja aliyeuliwa kwa kukatakatwa na walipofika eneo la tukio hilo walimuona kijana mmoja pembeni ambaye walimgundua kama Jason Massey.

Polisi waliandamana naye kwenye kituo na baada ya maswali waligundua kuwa ndiye aliyehusika katika kumchinjachinja yule ndama.katika kutafuta ushahidi na kutaka kuelewa akili ya mhusika,majasusi walitembelea idara fulani huko Quantico Virginia inayojihusisha na kuchunguza akili za wagonjwa wa akili wanaowadhulumu wanyama.waligundua kwamba mshukiwa alikuwa na historia ya kuwaua wanyama na kuhifadhi vichwa vyao kwenye mikebe spesheli.pia ilibainika kwamba Jason alikuwa mmoja kati ya watu wachache ambao hupata "raha ya ngono" katika mauaji(sexual pleasure).

majasusi walipata kibali cha kuchunguza makazi ya Jason na wakanyakua sampuli za nywele zake na pia wakalinyakua gari lake,ndani ya gari walipata bangiri ya mkononi yenye jina Jason.Hizo sampuli za nywele zilichunguzwa na wataalamu na kugundulika kwamba zilikuwa sawa na zilizopatikana kwenye miili ya vijana wale marehemu.mkeka wa gari ulipochunguzwa ilibainika kwamba kile kiuzi kilichopatikana kwenye viatu vya Jason kilitoka kwenye mkeka huo.

Polisi pia walipata habari kwamba Jason alionekana akiliosha gari lake kwenye car wash moja pale mtaani na baada ya kuchunguza mashine iliyotumika wakapata vinywele vingine ambavyo viliendana na nywele za Christina.Kwenye eneo la mizigo la gari ya Jason,majasusi walipata vifaa kama vile visu,panga,vyuma n.k na ambavyo vilionekana kuwa na matone ya damu.Hayo matone yalikuwa ya watoto wale waliouliwa.

jason Massey alikamatwa mara moja na kufunguliwa mashtaka ambapo alipatikana na hatia ya kutekeleza mauaji ya watoto hao.ushahidi uliopatikana ulikuwa tosha kwamba Jason ndiye muuaji aliyehusika.Polisi walifichua ile mikebe aliyohifadhia "zawadi" zake kama alivyoziita na vitabu vya kumbukumbu alivyoviita "the slayer journals"katika hivi vitabu,Jason alimtaja charles manson,muuaji mkubwa kuwahi kutokea marekani, kama mtu aliyemuiga.Ndoto yake Jason ilikuwa kuwa muuaji mkubwa na aliyejulikana sana ndani ya Amerika.Kwa jumla,polisi walipata vichwa 37 vya paka,43 vya mbwa na 27 vya ng'ombe.

Jason alipatikana na hatia,na kwa ambavyo akili yake ilijawa na chuki,mawazo ya ngono,dharau kwa jinsia ya kike na uuaji,alihukumiwa kifo kwa kudungwa sindano ya sumu.akiwa anasubiri siku ya kifo,Jason alimrudia Muumba wake na kuungama dhambi zake.Aliwaandikia barua wazazi wa wale watoto aliowaua na kuwataka radhi..Alifichua kwamba sehemu zilizokosa kwenye mwili wa yule msichana alizitupa ndani ya mto Trinity.

mnamo Aprili 3 2001,Jason alidungwa sindano ya kumuangamiza ndani ya jela kuu ya Huntsville huko huko Texas.wazazi wa watoto waliouliwa walipewa nafasi ya kushuhudia kifo chake.alizikwa Texas.
IMG_20170823_155123_794.jpg
alikozikwa Jason Massey.
 
Interesting!
By the way muuaji mkubwa aliyewahi kutokea Marekani alikuwa ni Gary Ridgway "The Green river killer".
Manson ni cha mdoli kwa huyo jamaa.
wapo wengi tu..the zodiac killer,the hitchhiickers'killer,akina ted bundy wote ni wauaji waliowahi kutekeleza mauaji ya kutisha..ila huyu Zodiac killer kinachomfanya kuwa outstanding ni uwezo wake wa kuficha ushahidi wowote ambao ungepelekea kugunduliwa..hadi wa leo,mauaji yote 37 hayajawahi kutatuliwa na kesi hiyo bado iko wazi ila karibuni itaweza ku expire..
 
Kula tano mkuu

DPP
haya mainshu husisimua sana na pia kutufunza mengi..kwa mfano hapa tumeona malezi mabaya yanavyoweza kuwa na adhari mbaya kwa watoto..pia mwishoni tumeona kwamba mtu yeyote,hata awe muovu anaweza kubadilika na kuwa mtu mwema.Jason aliokoka na ukisikiliza au kusoma barua zake za mwisho mwisho utaweza kugundua ni mtu ambaye alikuwa amebadilika na kuwa mtu mwema.
 
Pia kuna Chikatiko, The night Stalker, na Ted Bundy
wapo weeeeengi mkuu.ila nilimchagua huyu kwa vile story yake iko tofauti kidogo.katika mauaji,mambo mawili huwa ya kawaida sana,mapenzi au pesa..ndiyo mambo ambayo huwasaidia majasusi sana katika uchunguzi wao..kwa kiingereza wanaiita "motive"

ila kwa Jason hakukuwa na motive yoyote..
 
Back
Top Bottom