Mfahamu muonjaji mkuu wa kwanza wa kahawa nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfahamu muonjaji mkuu wa kwanza wa kahawa nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280

  MSAMIATI wa neno "ufisadi" umeanza kuwa maarufu hapa nchini katika miaka ya karibuni ukiwa na maana ya watu ama viongozi wanaojinufaisha kwa mali za umma. Katika miaka iliyopita neno mbadala lilikuwa "uhujumu uchumi" na wengine kutumia lugha nyepesi ya neon "rushwa."


  Kwa sasa neno ufisadi lina nguvu zaidi ya nene uhujumu uchumi na hali hii imefanya wengi waamini kwamba vitendo vya viongozi kujinufaisha na mali za umma, umeanza katika miaka ya karibuni, hususani katika Serikali ya awamu ya tatu na ya nne.

  Aliyekuwa Meneja Mauzo ya nje wa Shirika la Kuuza Mazao nje ya nchi (GAPEX), Mzee Joas Nyamhigura Kahembe (70) anasema ukweli ufisadi ulianza tangu enzi za Serikali ya awamu ya kwanza.

  Mzee Kahembe ambaye pia alikuwa Mtaalamu Mkuu wa Kuonja Kahawa na kuweza kuzitofautisha kimadaraja, anasema alikuwa ni mmoja wa watu walioonja ‘joto la jiwe' la ufisadi enzi hizo za uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

  "VTENDO vya ufisadi vinavyoitesa Serikali hivi sasa siyo tatizo la leo. Vilikuwepo hata kipindi cha uongozi wa awamu ya kwanza," anasema Mze huyo ambaye anaonekana kuwa na ushupavu wa kueleza ukweli wa mambo.

  Anakiri kuwa ufisadi wa wakati ule ni tofauti na wa sasa hasa ukilinganisha na mazingira kutofautiana kulingana na sayansi na teknolojia.

  Lakini kimsingi anasema ufisadi wa wakati ule ni sawa na wasasa huku akitoa mfano kuwa baadhi ya viongozi walikuwa wakiwaibia wakulima wa mazao ya biashara kama vile kahawa, katani, pamba na chai.

  "Baadhi ya watumishi walijaribu kushusha bei ya mazao yetu nchi kwa makubaliano ya kupewa ‘ten percent' (bakshishi ya asilimia 10) na wanunuzi wa Ulaya," anasema Mzee Kahembe.

  Tabia ya namna hiyo anasema ndiyo iliyomfanya aache kazi mwaka 1979 kupinga vitendo vwa wenzake kujinufaisha kupitia migongo ya wakulima masikini wa kahawa nchini.

  Anasema hajutii kupoteza ajira yake kwa sababu alikuwa na msimimamo yake katika kuzingatia uadilifu na kupiga vita vitendo vya kifisadi.

  "Watumishi wakiwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidii, kila mtu atapata kipato halali na hivyo kuishi kutokana na jasho lake badala ya ujanja ujanja na ubadhirifu unaofanyika serikalini hivi sasa," anasema Kahembe.

  Anabainisha kuwa vitendo vya ufisadi alivyovikimbia GAPEX ndivyo vilisambaratisha shirika hilo mwaka 1984, miaka mitano baada ya yeye kuondoka.

  Msambaratiko huo anasema ulisababisha wafanyakazi wengi kupoteza haki zao za malipo ya mafao.

  Kulingana na uzoefu wake wa kufanya kazi serikalini, anasema vitendo vya udfisadi vilianza kuibuka nchini baada ya vita vya Kagera.

  Baada ya vita hiyo ya kumng'oa Nduli Idd Amin Dadaa, anasema vilizua matatizo mengi ya kiuchumi na hata mazingira magumu ya kimaisha katika makundi mbalimbali ya watu.

  Hali hii ilichochea baadhi ya watumishi kutumiwa na wakubwa kuhujumu fedha na rasilimali za umma kwa faida binafsi.

  Mzee Kahembe anafananisha tabia ya ufisadi miongoni mwa watumishi wa umma kuwa ni sawa na mfugaji kuanza kutamani nyama ya ng'ombe anayemkamua maziwa, kitendo ambacho kitaishia kwa kumchinja na hivyo kuwa mwisho wa maziwa.

  "Ng'ombe unayemkamua maziwa kamwe usimtamani kumla nyama kwani utaishia kumchinja na huo utakuwa mwisho wa maziwa ambayo hudumu kipindi kirefu kulinganisha na nyama inayoliwa muda mfupi na kwa haraka kutokana na ulaku wa walaji," anasema Kahembe.

  Anaongeza: "Wakati naacha kazi mwaka 1976 nilikuwa napokea mshahara wa Sh 36,000 kwa mwezi. Nilishi nyumba ya Serikali Upanga, Jijini Dar es Salaam."

  Ingawa alikuwa anaishi Dar es Salaam, anasema Serikali ilikuwa ikimkodishia ndege ya kwenda Kilimanjaro na kurudi kila Alhamisi kuhudhuria mnada wa kahawa.

  Anasema licha ya kupinga jaribio la wenzake kujiwekea fedha nje ya nchi kupitia asilimia 10 kwa kushusha bei ya Kahawa kwa wanunuzi wanje, yeye alipinga wenzake.

  Kutokana na mfutano na kutofautiana na wenzake anasema aliamua kuacha kazi ili aepukane na dhambi ya kuwaibia wakulima, ambao wengi wao hadi leo wanaishi masha ya umasikini vijijini.

  Hata hivyo, anasema uamuzi wake wa kuacha kazi ulichjangiwa pia kubaini kuwa kuna maofisa wa usalama wa Taifa ambao walikuwa wanamfuatilia.

  Hilo anasema lilijidhihirisha wazi wakati ambapo alienda Jijini Nairobi, Kenya wakati wa likizo yake, kwenda kupumzika.

  Anasema safari yake ya Nairobi ilitokana na mwaliko kutoka kwa baadhi ya wanunuzi na wauzaji wenzake wa kahawa kwenye soko la dunia ambao walionyesha kuvutiwa na utendaji wake.

  Uzoefu wake katika biashara ya kahawa, anasema iliwafanya baadhi ya wafanyabiashara kuwasiliana naye kumuomba awasaidie katika kuanzisha kampuni binafsi ya kununua na zao hilo ambalo lina soko kubwa duniani.

  "Kwa sababu kipindi kile mipaka yetu na Kenya ilikuwa imefungwa. Nilitumia usafiri wa ndege kupitia Lusaka, Zambia. Niliporejea nilikuta tayari habari zangu ziko serikalini na nikatakiwa kujieleza juu ya safari yangu ya Nairobi," anasema.

  Licha ya suala hilo la kutoomba ruhusa, alitakiwa kueleza ni sababu gani zilizomfanya asiombe fedha za kigeni kwa ajili ya safari hiyo. Anaeleza kuwa suala la safari yake nje ya nchi ilitumika kama sababu ya kumwandama baada ya kuzuia ulaji wa wakubwa.

  Anasimulia licha ya kujieleza na kubainika hakuwa na makosa, wenzake walionekana kutafuta njia za kumchimba zaidi na kutafuta visingizio vya kumuandama, lengo likiwa ni kumfukuza kazi.

  Anasema anakumbuka aliyekuwa Waziri wa Kilimo wakati huo, John Malecela alijaribu kumtetea na kumuunga mkono kwenye mapambano dhidi ya ufisadi.

  Licha ya Malecela kumtete, anasema aliona muafaka mzuri kwake ni kuacha kazi kwa akiamini kuwa maadui zake wanaweza kumtafutia sababu.

  Anasema wengi waliamini kuwa kitendo hicho kinadhihirisha kwamba amechanganyikiwa, wakiwepo wafanyakazi wenzake, ndugu na mke wake.
  Walifikiri hivyo kwa sababu mshahara aliokuwa anapokea ni mnono na asingweza kupata sehemu nyingine atakakoajiriwa.

  Mzee Kahembe anasema yeye ni baba wa watoto 10 kwa mkewe Mary Kahembe, na alizingatia msimamo wake wa kaucha kazi licha ya wanafamilia hao kumsihi asifanye hivyo. Anasema familia yake ilikumbwa na wasiwasi mkubwa kwamba wataanza kushi maisha magumu.

  Baada ya kuacha kazi anasema alipewa kiinua mgongo cha Sh 56,000 ikiwa ni mshahara wa miezi 12, (36,000) pamoja mafao ya 20,000 kutoka lililokuwa shirika la akiba la wafanyakazi (NPF).

  Anasema baada ya kupokea malipo yake alihamia Babati, enzi hizo ukiwa mji usio na umeme kulinganisha na Jiji la Dar es Salaam alikokuwa akiishi wakati anafanya kazi.

  Ni maisha mabayo hata familia yake ilikuwa vigumu kuyazoea haraka lakini binafsi ni bora zaidi kuliko kufanya madhambi kwa Watanzania wenzake.

  "Pamoja na mambo yote niligundua kwamba mfanyakazi hata akipendwa kiasi gani kazini kwake lazima iko siku aondoke. Niliondoka na nimemudu kuwasomesha wanangu hadi kiwango cha chuo kikuu. Sasa namiliki magari na kampuni ya utalii," anasema.

  Lakini jambo kubwa lililompa ujasiri wa kuacha kazi na marupurupu yote anasema ni kauli mbiu na falsafa ya ‘kujitegemea' iliyoanzishwa Rais wa wakati huo, Mwalimu Nyerere.

  Siri ya mafanikio
  Mzee Kahembe anasema katika maisha yake hatawasahau wazazi wake ambao walimsomesha kwani elimu hiyo ilimwandaa kufanya kazi yoyote halali ilimradi amudu maisha katika mazingira yoyote.

  Anasema baada ya kulipwa mafao yake na kuhamia Babati, mwaka 1980 alinunua shamba la hekari 6, ng'ombe, mashine ya kukoboa na kusaga.

  Anajisifu kwamba uwezo wake wa kibiashara ulimuwezesha kuwa mtu wa kwanza kufungua duka la dawa wilayani Babati.
  Pamoja na biashara hizo, anasema alimuhimiza na kumpa moyo mkewe naye kuendesha biashara ya mkaa.

  Anasema alimpa mtaji wa Sh3,600 na kufungua stoo ya kuunzia mkaa na biashara hiyo ilisha\miri kutokana na kuwa na wateja wengi.

  Anasema aliingia kwenye biashara ya kutembeza watalii lakini alipata masimango kutoka kwa wenzake kumwambia kitendo hicho ni kudhalilisha jamii ya kiafrika.

  "Mwanzoni wenzangu kwenye sekta ya utalii walinipinga wakidai kutembeza watalii kwenye familia za kiafrika kutatudhalilisha kwani itawawezesha kuona maisha duni ambayo baadhi yetu tunaishi, lakini hali sasa ni tofauti baada ya utalii wa utamaduni kushika kasi,"anasema.

  Akitetea kuwaonyesha watalii maisha halisi ya Kiafrika, anasema: "Mazingira, maisha na mahitaji ya kiafrika ni muafaka na sawa tofauti na hisia kwamba ni duni kulinganisha na wazungu. Ndiyo maana wakija huku kwetu wanayatamani."

  Mzee Kahembe anasema kuna makabila zaidi ya 120 nchini ambayo yanaweza kutumika kupanua wigo wa vivutio vya utalii kwa wageni badala ya kutegemea wanyama na milima Kimanjaro kama vivutio pekee nchini.

  Anasema historia ya binadamu wa kale inawahusu wote bila kujali kama ni Waafrika, Wazungu, Wahindi au Waarabu. Kahembe anatamba kuwa maisha ya Watanzania ni raha kwa mazingira na mahitaji yao kiasi kwamba watalii wanaotembelea familia za wenyeji huvutiwa.

  Wakati ameajiriwa anasema alitembelea nchi mbalimbali za Ulaya ikiwemo Ujerumani, Uingereza, Finland, Sweden, Denmark, Uholanzi na Italya. Safari hizo zote alisema mara nyingi zilikuwa ni za kwenda kutafuta masoko nah ii ikampa fursa ya kufahamu namna wazungu wanavyoishi kwao.

  Kabla ya kuwa Meneja wa mauzo ya Kahawa nje na Muonja Kahawa Mkuu, Kahembe alifanya kazi Bodi ya Kahawa mwaka 1967.
  Mzee Kahembe anasema wakati akifanya kazi na hata alipoacha, hajawahi kunywa vileo na wala dhamira yake haijawahi kumshawishi kuonja aina yoyote ya kilevi.

  Katika ujana wake anasema aliwahi kunywa pombe za kienyeji mwaka 1955. Anasema alizaliwa mwaka 1942 na kuhitimu elimu ya msingi shule ya msingi Kikukwe na baadaye kuendelea na elimu ya sekondari Mkwawa, Iringa mwaka 1964.

  Ili kumjengea uwezo na kupunguza uhaba wa watumishi serikalini kipindi hicho, anasema Serikali ilimpeleka kusomea masuala ya uchumi nchini Italy.

  Mwisho. Mfahamu muonjaji mkuu wa kwanza wa kahawa nchini
   
 2. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 848
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kumbe matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa yalianza zamani.Yaani muonjaji kahawa aiishi dar angali ofisi yake ipo moshi? Kila wiki DAR-MOSHI kwa ndege ya serikali angali inawezekana kuwa na makazi ya kudumu kikazi moshi, hii nayo ilikuwa hatari.
   
Loading...