MFAHAMU MNYAMA NYUMBU

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,942
3,602
[HASHTAG]#FAHAMU[/HASHTAG]:NYUMBU ni Mnyama mkubwa anayepatikana Afrika katika maeneo ya Savana mnyama huyu anatajwa kuwa ni mnyama mwenye uwezo mdogo wa kufikiri hususani katika maeneo ya hatari.
Mfano mzuri Nyumbu wanaweza kuwa na kiu wakaamua kwenda kunywa maji kwenye mto wenye mamba ,wenzao wakiliwa wao wataendelea kunywa maji hapo hapo au wakarudi siku nyingine kunywa maji nakusahau kama wenzao waliliwa katika mto huo.
Nyumbu hawana utamaduni wa kusaidiana pindi mmoja wao anapokamatwa au kufukuzwa na adui inapotokea hatari kila mmoja anatafuta namna ya kujiokoa mwenyewe.
Wanyama hawa hupenda kujichanganya na wanyama wengine kama pundamilia,nyani na baadhi ya ndege ili kujikinga na maadui.
[HASHTAG]#Taja[/HASHTAG] sifa nyingine ya mnyama huyu.
2c3cfb083da645383e4bb0d3c1f3a7fb.jpg
8eb302804ecb05c3dd532a8b8529b8f3.jpg
de41d70e5b9b35ecb948c0510bb293ef.jpg
 
Back
Top Bottom