Mfahamu Mmiliki na Mwanzilishi Wa simu za Tecno na Infinix

kweli kabisa wachina wako vizuri kwenye technology hata Jose chameleon nae alikuwa anazo pikipiki zilizotengenezwa kwa jina lake
alikuwa na soko zuri tu Uganda sijui kama siku hizi bado zipo
Nenda karikoo hapo pikipiki kibao tu zinamajina ya kikinga, achana na jinsi, viatu na nguo mbalimbali.
 
Wikipedia hata wewe waweza andika sio reliable source.
Lete source ambayo ni reliable ,achana na blog za Nigeria na zote zimeandika kila kitu kimefanana neno kwa neno Na Wikipedia sio rahisi Ku edit kama unavyofikiria ndio maana imekuwa moja ya reliable source za information duniani kote
 
Lete source ambayo ni reliable ,achana na blog za Nigeria na zote zimeandika kila kitu kimefanana neno kwa neno Na Wikipedia sio rahisi Ku edit kama unavyofikiria ndio maana imekuwa moja ya reliable source za information duniani kote
Anzisha uzi wako uandike unachofahamu uweke na source zako. Tatizo lipo wapi watu watasoma wata comment pia. Acha ujuaji, kusubiria embe juu ya mnazi.

Mama yangu kumbe nuelimisha....nitajipa tabu. See u bro
 
Lete source ambayo ni reliable ,achana na blog za Nigeria na zote zimeandika kila kitu kimefanana neno kwa neno Na Wikipedia sio rahisi Ku edit kama unavyofikiria ndio maana imekuwa moja ya reliable source za information duniani kote
Na kwakuwa unahtaji utomas sio mbaya.
A Story About The Founder Of Slot Everyone Must Read

Nairametrics wenyewe hao waliomuhoji, au nayo blog unataka Wikipedia
 
Wanavifanya wao kivipi? iPhone inaundwa na kampuni ya kichina inatwa Foxconn.
Components zote hawatengenezi wao, wako involved kwenye design tu ya baadhi ya parts sio kwenye utengenezaji.

ti_graphics_where-your-iphone-comes-from-v02.png
hii ni manufacturing mkuu

trick kubwa ya electronic device ipo kwenye kudesign kifaa husika, uzuri na ubaya unachangiwa sana na jinsi utakavyodesign hicho kifaa.

kampuni nyengine hazi design kabisa zenyewe zinaenda china na kuchukua vifaa na kubandika logo hii ni tofauti na mtu anaedesign kifaa chake na kupeleka china kufanyiwa manufacturing.

ndio maana unakuta kwenye simu hizi zinazobandikwa logo tu vitu kama virusi, app kujipa root acess na ujinga ujinga mwengine upo mwingi sababu mtengeneza malware yeye anahack design moja tu ambayo imetumika na brand zaidi ya 100.

Angalia pikipiki za GSM, simu za GSM, Tiles za monalisa, Battery za tiger, etc vyote vinamilikiwa na wabongo na vina logo za kibongo lakini vimeekwa tu logo hawajahusika kwenye design wala manufacturing.

bahati nzuri nimewahi kufanya kazi kwenye kampuni ya namna hio kama mtu ana dola 10,000 tu hapa baada ya mwezi unaletewa bidhaa yako unayoitaka kwa brand yako, hakuhitaji jitihada ya aina yoyote.

nampongeza tu huyo jamaa wa Tecno kwa upande wa biashara ila upande wa technology? hapana hajafanya kitu cha sisi kushangaa.
 
Balaa
Siku zote lipo tumaini katika hali yeyote mtu anayokutana nayo Maishani. Umasikini au hali ngumu ya Maisha sio vitu anavyodumu navyo mtu siku zote.

Nnamdi Ezeigbo, ndie Mwanzilishi na mtendaji mkuu (CEO) wa kampuni maarufu ya Slot System Limited na pia Mwanzilishi mwenza wa (Co-founder)wa kampuni ya simu ya Tecno na Infinix moja ya simu zinazouza sana na kukua katika soko la Afrika.
fe27753b545ea5f41f1a47f7a40252c7.jpg


Kutoka katika kutafta kazi bila mafanikio ikamplekea Nnamdi kuwa fundi wa kompyuta kwenye kichumba kidogo huko Nigeria. Biashara ikakubali, leo ni moja ya mifano kwa vijana wengi wa Naijeria na Afrika kwa Ujumla.

Mafanikio yake yamethibitisha kile wasemacho walimwengu, fursa inapokutana na maandalizi, mafanikio ni hutokea.

JINSI ALIVYOANZA

Nnamdi Ezeigbo ni asili yake ni Umahia jimbo la Abia, alizaliwa tarehe 04/08/1966 jimbo la Delta Nchini Nigeria. Baada ya masomo ya sekondari alijiinga na Chuo cha Teknolojia cha Yaba mwaka 1988, ambapo alisoma Asta-shahada (Diploma) ya uhandisi wa vifaa vya umeme (Elecronical Elecronics Engeneering).

Kati ya mwaka 1996 na 2001 alijiunga na Chuo kikuu cha Lagos ambapo alisoma Shahada ya uhandisi wa kompyutana Elecronics akahtimu na Upper Second Class, Baada ya kumaliza masomo ya diploma Nnamdi Ezeigbo alitafta kazi bila Mafanikio na mwishowe aliamua kijiajiri kama fundi wa kompyuta. Ukarimu, kujali wateja kulimpa umaarufu na kumtunuku wateja wengi sana.

KONA YA MAFANIKIO

Siku moja mteja wake wa siku nyingi alifika katika kibanda chake cha kitengenezea kompyuta, huyu mteja akamwambia angependa apanue eneo lale la biashara ili wateja wapate huduma nyingi zaidi za kompyuta, huyu mteja alimletea printer ili awe anaziuza, hiyo ilimpelekea Nnamdi kuanzisha duka lingine kwaajili ya kuuza kompyuta na vifaa vyake. Biashara ikakubali ikakua na hapo wateja wakaanza kuhtaji na bidhaa za simu.

Bwaba Nnamdi Ezeigbo akaiona fursa mpya akaongeza bidhaa za simu na simu katika duka lake. Duka hili lilikuwa maarufu kwa jina la slot.
1796e5683411e5842ad920044d34f994.jpg


Akiwa hana taaluma ya kuendesha biashara kubwa Nnamdi aliamua kujiunga na Shahada ya Uzamili katika masomo ya biashara (MBA program) katika Chuo kimoja cha biashara Lagos huku akihudhuria mafunzo mbalimbali ya Ujasiliamali. Miaka mi 5 baadae SLOT ilikua na lilikuwa ni jina maarufu karibu Nchi nzima wakiwa kama wauzaji wa simu za rejareja (retailer Sellers).
f21959275b1ecb6031d4b615bef7298e.jpg
3f5f3c941cf7da29084e70c6f58efc3e.jpg


Kutokana na kukua mawasiliano ya simu za mkononi (Mobile phones) ilikuwa ni fursa kubwa katika soko la Nigeria lakini huduma hafifu za mitandao ilipelekea Wanaijeria wengi kununua simu zaidi ya moja ili mtandao mmoja unapokuwa na tatizo aweze kutumia mtandao mwingine.

Nnamdi aliona hili ni tatizo hivyo aliamua kufanya mawasiliano na kampuni ya Nokia akiwashawishi watengeneze simu za laini mbili kwa ajili ya soko la Nigeria, walikataa kwakuwa kwao watu kununua simu zaidi ya moja ilikuwa ina maanisha biashara.

Kupitia Mahojiano yake na "Nairametrics" NNAMDI alisema
"Hivyo nilienda China, nikakuatana na Bwana mmoja aliewahi kufanya kazi katika kampuni moja iliyojulikana kama Bird. Bird ni watengenezaji wa simu, walipata mtikisiko wakapoteza hisa zao sokoni"

Anaendelea "Hivyo nilipokutana na huyu Bwana nilimuomba tufanye kitu. Nilibuni jina na nikaisajiri, nanikaja na yule bwana hapa Nigeria, hiyo ilikuwa ni mafanikio ya hali ya juu ya biashara yetu. Tulikuja pamoja na nikabuni simu ya kwanza ya tecno, Tecno T101. Tulianza lakini soko halikutukubali lakini pia tulikuwa na tatizo kwa upande wa laini mbili hazikuwa zikifanya kazi kwa wakati mmoja, hivyo ilitupasa kufanya marekebisho tukaja na tecno T201 na kwa kiasi ilikubalika sokoni. Na kwakweli tulikuwa tukiwapa wauzaji kwa mkopo hii simu na wanapouza ndipo hutulipa, nami nilikuwa nikigharamia utengenezaji wake mwenyewe".
dc5eda7fb1544e2cd2a177afe31efc32.jpg


Nnamdi Ezeigbo, anasema kwakuwa alikuwa akigharamia mwenyewe uzalishaji wa simu alipata ugumu kuzalisha simu nyingi za kupeleka sokoni mpaka pale soko lilipoanza kukubali bidhaa zao ndipo alibadili mfumo kutoka kuziuza kwa mkopo na sasa wauzaji na wasambazaji walipaswa kununua kwa oda maalumu. Anasema "We started Using their money to order the products, this was around 2007" (Tulianza kutumia pesa zao kuagiza bidhaa, hii ilikuwa kwenye mwaka 2007).

MAFANIKIO YA TECNO NA KUIBUKA KWA SIMU NYINGINE YA INFINIX

Nnamdi katika mahojiano yake na Nairametrics alinukuliwa akisema "Kama nilivyosema, Tecno ni mwanangu na tumekua tukikua. Nilijua ipo siku watu wa daraja la kati wangeikubali tecno. Mwanzo ilikuwa simu ya watu wa kipato cha chini lakini kutokana na maboresho yetu na kuupangilia vizuri mchezo watu wa daraja la kati waliikubali na uchumi uliposhuka mwaka 2008 ilisaidia tecno kwenda katika mafanikio.

Nguvu ya manunuzi ya pesa ilishuka, hii iliwafanya watu kutafuta kitu chenye nguvu sawa lakini nafuu, hivyo kwa kiasi cha Naira 15,000 uliweza nunua Smartphone. Ahsante Mungu kwa mtandao wa 3g kwa hakika uliisaidia tecno kukua, Hivyo wanafunzi ambao hawakuweza kununua Smartphone kwa Naira 30,000 waliweza nunua kwa N15,000 na kufurahia sifa zilizo ndani ya Smartphone kama Facebook, Twitter, Whatsapp n.k" alisema Bwana Nnamdi.

Akizungumzia kuanzishwa kwa simu nyingine yenye jina la Infinix alisema, "sasa tecno imezaa Infinix, unaweza kuona jinsi tecno ilivyobadilika, na kwakuangalia haraka unaweza kuona kuwa itafika siku Tecno itatumiwa na watumiaji wa juu kabisa (Premium Customers)".

Leo tecno na Infinix ni simu zinazouza sana Nigeria na sehemu kubwa ya Afrika zikiwa na wapenzi, umaarufu na heshima kubwa kwa watumiaji wake.

Pamoja na stori hii ya kuvutia ukweli ni kuwa ukinunua Tecno au Infinix na hata Itel umenunua kampuni moja inayomilikiwa na Muafrika Nnamdi Ezeigbo.

5e1216b7b097e7c22c3707d6fb143dfe.jpg

Kampuni yake ya SLOT ina matawi zaidi ya 40 nchi nzima ya Nigeria, kwasasa Bwana Nnamdi Ezeigbo anaendesha programu za ujasiliamali katika Chuo Cha Harvad (Harvad University).

-Dumelang
Imetafsiriwa kwa Msaada wa Mitandao.

Update: pitia link hapa ya Nairametrics, maana kuna matomaso wanataka Wikipedia, mengi sikuyaandika yapo hapa yanaweza kukifunza kitu, struggle n.k

A Story About The Founder Of Slot Everyone Must Read
 
Naona unataka kuleta ubishi usiokuwa na sababu. Nimeongea hivyo kwa sababu maalum. Ukiwa na kiwanda maana yake kuna faida nyingi utazipata. Utaweza kuwa na kitengo chako cha research and development, utaweza kuwa na confidentiality ya bidhaa zako, utaweza kumonitor na kucontrol quality ya bidhaa zako, na pia bidhaa zako utazipa touch unayotaka wewe.

Sasa vitu vyote hivyo kwa sasa Tecno hana.
Wengi hawana huo uwezo wa kuwa na kiwanda jombaa, thats why mbadala ndo huo mkuu!

Hayo ya kuwa na viwanda wanaweza kina Dewji pekee wengine tuige mfano wa jamaa wa Techno nukta.
 
Siyo kweli TECNO, INFINIX NA ITEL zinatengenezwa na Transission holding Company ya Hongkong. Hii story ya huyu bwanaa inapatikanaga facebook kuwapa promo wa Nigeria na kwa sababu yeye ndo aliingiza bidhaa za itel na tecno huko kwao Nigeria.
 
Acha uwongo zpo znazotengenezwa china na Marekani kwa wamiliki wnyw
Hakuna iPhone inayotengenezwa Marekani, nilipoandika hiyo post zote zilikuwa China sasa hivi wameanza kutengeneza India na Vietnam pia ila hakuna Marekani hadi leo.
 
Back
Top Bottom