Mfahamu mlinzi wa Tundu Lissu, Renatus Hangaya. Asema alimfahamu 2006 kumfundisha 'Martial Arts'

Nchi hii kuna vilaza wengi sana.
Ulitegemea baada ya mtu kuwa hispitali muda wote huo aendelee na marshal arts
Labda unachanganya, bonge'' yaani kuwa na mwili mkubwa ambapo ni genetics watu wanazaliwa hivyo vs unene mwili kujaa mafuta, Tundu lisu amejaa mafuta kuna tofauti hapo, huyo Komandoo wako simjui lkn kama ni kweli ni mtu wa marshal arts na ni komandoo wa Jeshi basi inawezakana ana mwili mkubwa tu ambao amezaliwa nao lkn hawezi kuwa amejaa mafuta kama Tundu Lissu.
 
Kuchorachora ukutani au chini ardhini.
Haya yooote yalikupita ajili ya Userure wa kudumu Loool!! ujui wewe!!.... JKT lazima ulikuwa Nanga hasa!! na Mtorokaji sugu!! mwizi wa mihogo, viazi miwa ya wana kijiji!!
Maafande wakiwasihi vijana Msijongo li Gwaride ni muhimu nyie ndo kwaaanza ....

mnawaita majina km Vile wanoko!! mara wanajipendekeza!! ...... Ona sasa Mzee mzima unavoumbuka! na mafunzo ulipata full course, 823 KJ Paleeee!!!! unabisha??
 
Haya yooote yalikupita ajili ya Userure wa kudumu Loool!! ujui wewe!!.... JKT lazima ulikuwa Nanga hasa!! na Mtorokaji sugu!! mwizi wa mihogo, viazi miwa ya wana kijiji!!
Maafande wakiwasihi vijana Msijongo li Gwaride ni muhimu nyie ndo kwaaanza ....

mnawaita majina km Vile wanoko!! mara wanajipendekeza!! ...... Ona sasa Mzee mzima unavoumbuka! na mafunzo ulipata full course, 823 KJ Paleeee!!!! unabisha??
Nabisha. Sikipitia 823, ila nimetoroka vizuri tu na nimeshalala mahabusu kwa utoro na nimelipia siku 30 baada ya mafunzo
 
Renatus Charles Hangaya ndio jina lake mzaliwa wa Kahama mkoani Shinyanga mwaka 1980. Alifukuzwa shuleni kwa hujuma za kifamilia sababu kuu ikiwa mali za mzee wake.

Kwenye historia amesema alikuwa kamanda wa scout wa kikosi cha Simba, walipelekwa camp Uganda 1994 na kuweza kuwika Afrika kiasi waziri mkuu wa Uganda alipofunga mafunzo jina lake lilitajwa miongoni.

KIFAA ALICHOBEBA
Kwa maelezo yake amesema kifaa hicho ni cha jadi, ikiwa ni ulinzi na mapigano kwa shujaa, haipaswi mhusika kuwa mtu wa dhulma, kifaa cha mlinzi wa haki.

Amesema kifaa hicho hamna mtu alieweza kukiona kwani ni siri lakini alikitoa kwa mapenzi yake kwa mtu wake aliemuamini, kumpenda na kumlinda kwa sababu ya mambo aliyohitaji kuyafanya pamoja nae.

Amesema watu wamekishangaa lakini mwisho wa kukishangaa ni kutaka kuelewa au kuwa muoga lakini hakipo kwa madhara yoyote.

Amesema kuzaliwa kwake yeye kulisemwa na babu yake aliyepigana vita ya pili ya dunia na amemuachia fimbo yenye asili ya mwaka 1880 na yalisemwa mambo mengi aliyokuja kuyafanya ikiwemo kurudisha utawala wake uliopotea.


KAZI YAKE KWENYE KAMPENI
''Nilipewa kazi ya ulinzi, niliwajibika kulinda kwa mikono yangu lakini hatua za mwisho niliona nichukue kifaa hiki, sio cha hatari kama ulinzi kwa wanaoshika bunduki mbele ya viongozi lakini hazijawahi kuulizwa sana ikimaanisha hakuna nguvu ya asili katika vitu vile" Alisema mlinzi wa Lissu.

KUKUTANA NA TUNDU LISSU
Anasema Lissu ana kijana wake anaitwa Adam Mohammed maarufu kwa jina la Simon. Wakati yeye akiwa mkufunzi wa martial arts, Adam alihitaji afundishwe na kwa muda mrefu alimkatalia. Alipoanza kumfundisha, perfomance ya Adam ilikuwa nzuri.

Mwaka 2006, Tundu Lissu alienda kwenye chuo cha Renatus kujiunga kama mwanafunzi wa Martial Arts na ndipo walipoanza kufahamiana kupitia kwa Adam Mohammed.

"Self defence is like Vladimir Putin, ulinzi wa kwanza uwe nao kabla ya mlinzi wa kwako. Nawezaje kuutumia mwili wangu kabla ya kuomba msaada kwenye jiwe, kisu, bunduki, kwa mtu binafsi, kwa mbwa, huo ndio ulinzi tunaouona lakini ulinzi wa kwanza unakuwa nao mwenyewe, inaweza ikawa ni maneno, macho yako, sura na matendo yako. Kimoja katika hiko kina uwezo wa kukulinda" Alisema Renatus.

Renatus amesema anafanya kazi na Tundu Lissu kama mtu aliyekuwa madhubuti kutetea harakati na watu wawili hufanana kwa misimamo, kwani hamuwezi kutembea pamoja kama msipopatana.

"Kama kuna mahali Tundu Lissu angekuwa anakuwa muongo nisingefatana nae lakini kama anakuwa ni mkweli, tumefata, sio kwamba wengine siwapendi ila hawafanani na sio kwamba hawastahili ila kipimo kionyeshe" Aliendelea Renatus

"Kuna siku nilimuita tuko wawili, niliona kuna hali fulani ambazo sikuzielewa nikahisi huenda na yeye anazibariki ili niachie kazi katikati ya kampeni, tukiwa Karagwe nilimfata, nikamwambia naomba tuongee wawili. Nikamuuliza, una mashaka na mimi? Na kuna mahali nimekosea? Boss alinijibu jibu ambalo lipo mpaka leo na akanifundisha kwa vitabu alivyowahi kuvisoma juu ya mambo ya walinzi na fitina zao dhidi ya kuwa na viongozi"

CREDIT: Mwanahalisi

Naamini mada hii imeijibu ya ndugu Mdaiwa-Sugu

=> Silaha ya mlinzi wa Lissu imenitoa ushamba

Sasa nimeelwa kwanini aliweza kukwepa risasi 40 na ushenzi
 
Mtoa mada itendee haki hii mada mbona umeiandika kama unakimbizwa?hebu urudie upya pls na weka nyama zaidi kwenye mifupa ili nami nikuelewe vema mkuu.
 
Back
Top Bottom