Mfahamu Mkuu Mpya wa Jeshi La Polisi (IGP) Simon Nyakoro Sirro

JINOME

JF-Expert Member
May 29, 2017
958
1,426
Simon Nyakoro Sirro alizaliwa eneo la Kiabakari wilaya ya Butiama mkoani Mara mwaka 1963.
Kuhusu elimu yake, Simon Sirro alisoma Shule ya Sekondari ya Ilboru jijini Arusha na Tosamaganga kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu kusoma Shahada ya awali katika Sheria.
Sirro amesoma pia seminari (masomo ya upadri) na kufikia ngazi ya juu kabla ya kuacha na kujiunga na Jeshi la Polisi.

Kamanda Sirro alisema kuwa kama isingekuwa baba yake basi leo yeye angekuwa ni Padri wa Kanisa Katoliki kwani ndiyo ndoto yake kubwa, lakini baada ya wazazi wake kumkatisha ndipo alipojiunga na jeshi hilo.

Unajua wazazi kule kwetu Musoma walikuwa hawakuelewi usipooa. Mzazi aliona mimi ni kijana mkubwa akasema haiwezekani,” alisema Sirro alipofanya mahojiano na Mwananchi kipindi cha nyuma.

Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Kituo cha Polisi Buguruni mwaka 1998, Mkuu wa Upelelezi Tarafa ya Magomeni kwa miaka 5 na Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Tabora.
Mwaka 2002 alikuwa Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam akiwa ni msaidizi wa Abdallah Zombe.

Sirro ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam wa tatu ambapo aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli Februari 15 mwaka 2016 akichukua nafasi ya Suleiman Kova aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2008. Kabla ya Kova aliyekuwa akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni Alfred Tibaigana.

Wakati Suleiman Kova akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sirro alikuwa msadizi wake ambapo baadae alirithi mikoba yake.

Kabla ya kuongoza Kanda Maalum Dar es Salaam, Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Tanzania. Moja ya opersheni kubwa alizowahi kuongozi ni Operesheni Kimbunga dhidi ya wahamiaji haramu mwaka 2012.

Lakini pia, Simon Nyakoro Sirro amewahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Mikoa mbalimbali ambayo ni Tanga, Mwanza na Shinyanga.

Wakuu wengine wa Jeshi la Polisi ni;
1.Elangwa Shahidi (1964-1970), alistaafu.

2.Hamza Azizi (1972-1973), aling’olewa na Mwl. 3.Nyerere kwa matumizi mabaya ya madaraka.

4.Samwel Pundugu (1973-1975).

5.Philemon Mgaya (1975-1980), aliachishwa kazi kwa manufaa ya umma.

6.Solomoni Liani (1980-1984), alihitimisha kipindi cha mwisho cha Mwl. Nyerere.

7.Harun Mahundi (1984-1996), alistaafu.

8.Omari Mahita (1996-2006), alistaafu.

9.Said Mwema (2006-2013), alistaafu.

10.Ernest mangu (2013-2017), atapangiwa kazi nyingine, na

11.Simon Sirro (2017-) yupo madarakani.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Nyakoro Sirro ameoa mke mmoja na ana watoto wanne
 
Asante kwa info, ingawa kuhusu kusoma Shule za Sekondari Ilboru na Tosamaganga kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu kusoma Shahada ya awali katika Sheria, halafu akasoma Seminari, ni kama umetuchanganya! Ninavyojua alianza Maua Seminari kabla hajaingia sekondari ya kawaida. Hii sijui imekaaje?...
 
Hivi seminari kuna kipi haswa cha madini mpaka kuwafanya wana usalama/shushushu kupendelea kusahili watu wa kutoka huko.?

Sitaki kuamini kama uhusiano wa ushushushu na seminari ni wa bahati mbaya.
 
Sawa, tumwombee aongeze salama kwa kuwa ni taasisi yenye changamoto nyingi hasa za kijamii na kisiasa.

Kikubwa sana ajitahidi kuliunganisha jeshi la police na wananchi ili taarifa za uhalifu zizidhibitiwe mapema. Awamulike askari wanaolipaka matope jeshi hilo kupitia:-
- kushiriki vitendo vya hujuma,
- kuomba rushwa,
- kutoa siri za jeshi letu.

Wananchi nchini toeni ushirikiano kwa jeshi ili litekeleze majukumu yake kwa ufanisi
 
Back
Top Bottom