Mfahamu member wa kwanza kujiunga, na thread ya kwanza kuanzishwa. Je member huyu ana cheo gani JF..?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,678
106,786
Salute Comrades..

Kawaida yangu hua ikifika saa nne usiku basi huo muda hua nautumia kuingiza vitu vipya kichwani kwa kutembelea jukwaa la Jf Intelligence, Jukwaa la dini, Jf International na kufukunyua mada mbalimbali zilizoanzishwa miaka ya nyuma.

Hivyo baasi..
Niliamua nijipe ka kazi kidogo (kama kipimo cha upelelezi/Intelejensia/ujasusi) wa kuchunguza
-Member wa kwanza kujiunga jf alikua nani..?
Anacheo gani..?
-Post ya kwanza kuanzishwa ilikua ni ipi..?
-Jf ilianzishwa tarehe ngapi..?

Basi
Nikaanza ujasusi wangu taratiiiibu mpaka nikagundua.

Kama tunavyojua Jf Ilianzishwa tarehe 3 feb 2006, member wa kwanza kujiunga jf ana cheo cha u - Admin anaitwa Spiderman.

Member namba mbili ambae ni member wa kawaida tu kama mm naww anaitwa Anonymous ana post #33 yaani jf ilipo be launched yeye akajiunga muda huo huo.
Swali ni je..
Huyu jamaa ni nani hapa jf? Aliijuaje jf kwa muda mfupi..?
Sometime nilitaka kumdhania kua ni Invisible lakini nikagundua huyu anonymous ni Atheist while Invisible ni Muislam kutoka Zanzibar.

Katika hali isiyo ya kawaida kwenye uzi ulioanzishwa August 2006 unaitwa "EAC Community" kuna mtu amekomenti ambae ana STATUS ya GUEST yaani hajajiunga jf na hajasajiliwa so najiuliza how aliweza comment while he is a guest..?
Anaitwa Athur Juma.

Uzi wa kwanza kufunguliwa jf unaitwa "Jf Rules" by Spider man Admin.

-Member #7 kujiunga jf ni Mkandara
#70 Mzee Mwanakijiji
#51 Nicholas

So huyu Anonymous ni nani..?

Da'Vinci
 
Back
Top Bottom