Mfahamu kondoo maarufu aliyejulikana kama Dolly Parton

MalcolM XII

JF-Expert Member
Mar 19, 2019
5,176
14,043
05 July 1996, mwanasayansi wa Kiskotishi aliekwenda kwa jina la Keith Campbell pamoja na wenzake walifanikiwa kukamilisha jaribio la kisayansi (Reproductive Cloning) lililofanyika kumuunda kondoo aitwaye Dolly Parton.

Hiyo ilikuwa ni baada ya kufeli kwa majaribio zaidi ya 20, na mwishowe kufanikiwa kumuunda Dolly.

Dolly anakuwa ni kiumbe wa kwanza kuundwa kwa process ya reproductive cloning kwa njia ya nuclear transfer.

Dolly ametokea kwenye process iliyohusisha Mama watatu (3). Wa kwanza alitoa yai, wa pili akatoa DNA (Genetic Material) na wa tatu akamueka tumboni mpaka alipozaliwa tarehe 05 July 1996.

Ilitegemewa aweze kuishi miaka 11 hadi 12, lakini kwa bahati mbaya alikuja kufariki 14 February 2003 akiwa na umri wa miaka 6 tu.

Katika kipindi cha uhai wake, Dolly Parton alifanikiwa kupata watoto sita (6).

Wa kwanza alimpata April 1998, aliitwa Bonnie. Mwaka ujao akazaa watoto mapacha (Twins) waliokwenda kwa majina Sally na Rosie. Na ilipofika mwaka 2000, Dolly alijifungua mapacha watatu (Triplets) waliokwenda kwa majina Lucy, Darcy na Cotton.

Mwishoni mwa mwaka 2001, Dolly aliugua kansa ya mapafu (Lung Cancer) iliyopelekea kifo chake tarehe 14 February 2003.

IJUMAA YA WIKI HII ya 14 Feb 2020, WANASAYANSI WATAKUWA NA KUMBUKUMBU YA KUMKUMBUKA DOLLY PARTON KAMA KIUMBE WA KWANZA KUUNDWA KWA NJIA YA REPRODUCTIVE CLONING.

images (3).jpg
images (2).jpg
images (1).jpg
images.jpg
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom