Mfahamu Komando Dogo: Jambazi aliyezua mtafaruku kati Tanzania na Burundi

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,895
22,659
April 2002 wilaya ya Ngara inapokea viongozi wakubwa wa kitaifa ni Waziri wa Ulinzi, Edgar Maokola Majogo na Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.

Hii ilikuja baada ya kuwepo na taarifa za kuaminika kutoka Wizara ya Ulinzi kupitia kitengo cha Intelijensia (M.I), Usalama wa Taifa (TISS) na Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi (OCCID) kuwa kuwa askari zaidi ya 200 wa kundi la waasi wa CNDD-FDD wa Burundi wameingia nchini kwa kuvuka mpaka wa Burundi na Tanzania eneo la Milamila na kuiba mifugo mingi ya wananchi, kuiba vyakula na kubaka wanawake.

Redio Kwizera FM ya mjini Ngara ilimnukuu Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakati huo Gen. Tumainiel Kihwelu akisema kuwa pamoja na tatizo hilo pia kuna magari yanatekwa mchana na usiku na kukiri kuwa sio kundi la majambazi bali Kijana mdogo tu anayeonekana kwa machale akivalia kininja na kufunga kitambaa chekundu. Hvyo aliwataka wananchi watoe taarifa haraka pindi watakapomuona japo (taarifa hii ilikuwa imeshasambaa sana mitaani, makazini na kwenye media kubwa) kuwapo kwa jambazi amatata anayeweza kuteka mabasi mawili peke yake na kuwapora polisi bunduki.

Kipindi hicho kilikuwa kipindi ambacho Serikali ya Rais Mkapa iliamua kufanya operation maalumu ya kuwarudisha wanyarwanda na warundi nchini mwao licha ya kukosolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa na taasisi za Haki za Binadamu hasa kuhusu Burundi ambako hali ilikuwa bado sio shwari sana kulinganisha na Rwanda ambako Serikali ilikuwa imeshasimikwa na kuleta mzozo kati ya ikulu ya Tanzania na U.N.

Kagera, Kigoma na Rukwa na silaha haramu
Mikoa ya Kagera na Kigoma na hata Rukwa ilitajwa kuwa na idadi kubwa ya silaha za kivita na hata mabomu huku wakimbizi wengi wanaume wakitajwa kujaa maporini wakijihusisha na wizi na ujambazi wa kutumia silaha. Mapori ya Kimisi, Biharamulo na Burigi yalitajwa kuwa ndio maeneo hatari sana. Habari za utekaji kila siku na unyanyasaji zilitamba. Kuna wakati watu walivuliwa nguo zote na majambazi yakiwataka wampe taarifa Rais Mkapa na slogani yake ya "Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe" hivyo kuzua hofu kubwa.

Kushutumiana baina ya Burundi na Tanzania
Kwa wale wasiokumbuka, kulikuwa na shutuma za baadhi ya vikundi inchini Burundi vikiituhumu serikali ya Tanzania kuwapendelea na kuwapa hifadhi waasi wa CNDD-FDD na kuwarusu kupitisha silaha eneo la Rasi Kibirizi mkoani Kigoma zilizodaiwa kuwa zilikuwa zikitokea Ubeligiji na kuwapo kwa kituo kilichokuwa cover up kama kituo cha wabeligiji cha kulelea watoto yatima maarufu kama “MWOCACHI” huku kikidaiwa kikihusika na upitishaji wa silaha kupitia Jeshi la Wanamaji eneo la Kibirizi. Nusu kilometa kutokea kituo hicho na kulifanya kundi hilo kuwa nguvu kuliko makundi mengine ya waasi wa nchini humo, ndo hii ilionekana kutuponza na uso wa mzee Kikwete ulionekana kujaa hasira sana kwa jambo lile.

Sasa, kitendo cha waasi wale kuingia Tanzania na kuvuka mpaka kilionekana kama tishio na mtoto kumgeuka baba na kuanza kumshika machoni. Hapa ileweke kwamba bado mikataba ya amani ya makundi haya inaendelela mjini Arusha - Tanzania huku kundi kama Palipehutu -FNL likionekana kustukia mchezo.

Kwa kuweka kumbukumbu vizuri, ni kuwa CNDD-FDD ni kundi lililoasisi na Hussain Rajabu awali akijifanya mtanzania aliyekuwa mkaazi wa Kigoma Ujiji kabla ya kurudi kwao Burundi kipindi cha machafuko kwa msaada wa Brussels na amehudumu kama mwenyekiti mpaka alipokuja kugombana na marehemu Nkurunziza na kufungwa jel miaka mingi kabla ya kuokolewa na vijana wake wenye utisho kama Komando Dogo nitakayemuelezea kwa undani.

Waziri Kiwete na Majogo (wakati huo) walikuta kesi kibao ubaoni hali tete ya usalama wa raia na mali zao, ubakaji, uwezo mdogo wa Jeshi la Polisi maana lilizidiwa na waasi walijipenyeza na kujichanganya na raia; usambaaji wa silaha/biashara ya siraha, wizi wa mifugo na hofu kubwa kwa jamii.

Mipaka ya Mulusagamba na Milamila ndio ilionekana kuwa njia na hapa ilibidi kuongeza askari wa JWTZ kutoka maeneo mengine kama 23KJ na 22KJ Biharamulo kukaa deti ya uhakika kuruhusu kushambulia haraka kama italazimika na kuwapa onyo. Cha kushangaza mifugo yote iliyoibiwa na waasi ililejeshwa haraka kwa makubaliano kuwa eneo hilo libaki salama na pande zote mbili zipeane taarifa za kiusalama!

UJAMBAZI
Kama nilivyoeleza hapo juu, kuliibuka wimbi la ujambazi lakini aliyetisha ni jambazi huyu mrundi maarufu kama “Komando Dogo” na kiukweli alikuwa dogo miaka kama 22-24 hivi ambaye aliweza kuteka mabasi peke yake na kufanya unyama wa kutisha. Kama utajaribu kumu-engage aliogopwa kwa kuwa alikuwa na sifa za ziada za askari wa kawaida kama zifauatazo:

1) Aliweza kuibuka na kutoweka bila kumuona ina maana alikuwa na mediation kubwa kama Gen. Mayunga

2) Alikuwa na timing za hali ya juu unaweza ukadhani movie za Hollywood; akipanga kufanya tukio anakuja muda muafaka na kupotea muda muafaka

3) Alikuwa na shabaha ya uwezo mkubwa (sharpshooter wa kiwango cha juu)

4) Alikuwa peke yake (one man operator ) na aliweza kuwa katikati ya misitu minene

5) Aliweza kubadili eneo kwa umbali mkubwa. Saa 5 akiteka Ngara, saa 6 anaweza kuteka Biharamulo na mkabaki midomo wazi alifaikaje na alitumia nini

6) Polisi walidai risasi hazipenyi ngozi yake kwamba amegangwa!

Hii ya kutopea kama upepo na kutokupenya risasi iliwaogopesha sana askari sio Polisi tu hata JWTZ kuwa alikuwa mtu wa tofauti ingawa mediation aliyokuwa nayo ni somo la commandos wote duniani ila hili la kutopitisha risasi lilitia wasiwasi wa nani aingie in front kumsaka.

KISA KAMILI: Je, Komando Dogo alitokea wapi na mwisho wake ulikuwaje?

Nitaendelea...
 
Nakumbuka pori la ushirombo tupo kwenye cruzer tukaona magari kwa mbaali yemetekwa.dereva akaichekecha gari yetu fasta kurudi runzewe. Waliachia risasi kadhaa lakini hatukudhurika.

Wale majambazi wa kirundi na Rwanda wanavalia kijeshi kabisa mpaka mabomu ya mkono wanakuwanayo.
 
Back
Top Bottom